Mudi Salah
Member
- Jul 5, 2022
- 57
- 55
Kwahiyo wanakwenda kukaa na kuwaridhisha viongozi pekeeHao viongozi wa TUCTA wakitoka kupigwa sound wanakuja kuwapa moyo wafanyakazi, then from there hizi hasira za siku mbili zinayeyuka maisha yanaendelea na nyongeza zinazoeleka.
Katiba Mpya [Rasimu ya Warioba ] ndio dawa ya matatizo mengi yanayoikumba jamii yetu, angalau pawepo na sheria zitakazowalazimu watawala kuzifuata, wasipozifuata ni mahakamani.
Kuwa na taasisi imara ni muhimu sana, mfano hao TUCTA wanaweza kuwa chachu ya mabadiliko ya nchi hii, lakini kwa udhaifu wao wamewekwa mfukoni na watawala.
Vyama kama TUCTA nchi nyingine vinaheshimiwa sana na serikali zao kwa sababu ya nguvu waliyonayo, ajabu hapa kwetu walimu nao hutumika kwenye kuiba kura ili hao watawala wanaowaonea waendelee kubaki madarakani!.