Sintofahamu ya Sukari

Sintofahamu ya Sukari

pumzihaiuzwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2015
Posts
3,273
Reaction score
3,083
Sukari imeadimika, sukari imekua adimu, sukari zimefungiwa kusiko julikana je ni ukaidi wa bei elekezi au nikweli viwandani production imepungua.

Wajuzi wa mambo mtujulishe wapi machimbo tunaweza kupata bidhaa hii iliyo adimika ghafla.
 
Kinachoamua bei ya sukari au bidhaa yoyote ni soko. Mfano sisi wakulima kuna miaka tunauza mpunga gunia Tsh 50,000 na kupata hasara wakati kunakipindi tunauza Tsh 100,000 au zaidi.

Mwaka juzi na mwaka jana combine harvestere zilikua chache tulivuna kwa Tsh 400,000, mwaka huu zipo nyingi tunavuna kwa Laki tatu tu kwa hector.

Kwahiyo suala hili lilitakiwa liamuliwe na soko.
 
Sukari imeadimika, sukari imekua adimu, sukari zimefungiwa kusiko julikana je ni ukaidi wa bei elekezi au nikweli viwandani production imepungua.

Wajuzi wa mambo mtujulishe wapi machimbo tunaweza kupata bidhaa hii iliyo adimika ghafla.
Mm jana nimenunua kilo kwa sh.2700/=Huku Kilosa morogoro na maduka ya kawaida wanauza 3000 je huko ilikoadimika ni wapi mkuu???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaarabi tunusuru. Tunarudi miaka ya 80. Ukitaka sukari unaamka saa kumi na moja asubuhi na kupanga foleni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku Arusha viongozi wapo makini sana kiasi kwamba hakuna anayethubutu kuuza sukari tofauti na bei elekezi, kwa hiyo kila duka ukiingia sukari hakuna.
 
Yaarabi tunusuru. Tunarudi miaka ya 80. Ukitaka sukari unaamka saa kumi na moja asubuhi na kupanga foleni

Sent using Jamii Forums mobile app
Miaka yote kipindi cha masika viwanda vya sukari husimamisha uzalishaji kwa sababu kuu 2: 1)kiwango cha sukari kwenye muwa(sugar content) huwa kilo chini, 2) miundombinu ya kuleta miwa toka mashambani huathiriwa na mvua. Kipindi hicho hutumiwa na viwanda kufanya matengenezo ya mitambo.

Mwaka huu mvua zimenyesha kwa muda mrefu na viwanda kushindwa kuanza uzalishaji. Hapa sasa wakunyoshewa kidole ni serikali. Inajua matumizi ya vyakula vyote kwa nchi lakini mikakati ya kuhifadhi ni kidogo.

Bunge ni mipasho kwa wapinzani na kuisifia serikali lakini muda wa kuishauri kwa mipango ya maana haupo.

Taarifa ya kuendelea kwa mvua walikuwa nayo lakini wahusika wako busy na kupanga madili badala ya kutoa vibali vya kuagiza sukari kufidia upungufu. Kila kiongozi yuko busy na corona utadhania ni tabibu au sangoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm jana nimenunua kilo kwa sh.2700/=Huku Kilosa morogoro na maduka ya kawaida wanauza 3000 je huko ilikoadimika ni wapi mkuu???

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nimeinunua tegeta 4000 tena baada ya kuzunguka maduka mengi nikawa nikiuliza wananishangaa kama nimeuliza nyara za serikali, hata aliyeniuzia aliniuzia baada ya kuwa na uhakika mimi siyo snitch
 
Back
Top Bottom