GE2025 Sintofahamu yaibuka kabla kuanza kwa Kampeni za Mgombea Urais CUF Tabora

GE2025 Sintofahamu yaibuka kabla kuanza kwa Kampeni za Mgombea Urais CUF Tabora

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Sintofahamu imeibuka katika eneo la Usinge Jimbo la Kaliua Mkoani Tabora kabla ya mapokezi ya mgombea urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF Gombo Samandito Gombo baada ya baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kufika kwenye eneo hilo na kuanza kufanya matangazo ya kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM jambo ambalo ni kinyume na ratiba kutoka Tume Huru ya Uchaguzi

Kwa mujibu wa ratiba kutoka Tume huru ya uchaguzi inaelekeza chama cha wananchi CUF kuwa ndio wanapaswa kuwa Mkoani Tabora kwajili ya kufanya kampeni zake katika Wilaya zote

Akizungumza baada ya kufika katika eneo hilo la Usinge mgombea Urais Gombo amesema kwamba amesikitishwa na kitendo hicho kilichokwenda kuibua vurugu katika eneo hilo huku akiwataka wanachama wa CCM kufuata sheria kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa

"Nataka niwaambie chama cha CUF kimesimamia haki hatuhitaji haki hiyo ivunjwe na chama chochote wala mti yeyote Tanzania sisi ni watanzania wote kama chama cha mapinduzi wanatubeep kwa kutufanyia fujo tutawapigia nataka nitoe angalizo kwa ccm kupitia mkutano huu na Tanzania nzima isikie tunasema ccm wafuate sheria, haki na kamahawataki haki sisi tunao uwezo wa kuwajibu, "alisisitiza Gombo

"Ccm ina haki ya kufanya mikutano na sisi CUF tuna haki na vyama vingine vina haki kama ccm wamechoka hiyo haki na hiyo amani Cuf tunao uwezo wa kujibuna nyinyi muwe tayari kujibu muache unyonge unyonge hawezi kuja mtu akakuchania bendera, akakuchania picha ya mgombea wako halafu ukamtizama tu mimi nasema hivi hatujaajiri bado lakini naomba na vyombo vya dola visikie ccm wasijisahau vyombo vya dola museme, "ameongeza Gombo

Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo la Kaliua kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF Magdalena Sakaya ameiomba Tume huru ya uchaguzi ihakikishe inasimamia uchaguzi uwe wa huru na wa haki ikiwa ni pamoja na kufanya kazi yake kikamilifu


1757839158621.png





1757839243239.png


CHanzo: EATV
 
Back
Top Bottom