Sintofahamu zote hizi tuangalie tulipojikwaa ili tusonge mbele kuokoa taifa letu.

Sintofahamu zote hizi tuangalie tulipojikwaa ili tusonge mbele kuokoa taifa letu.

HANGAYA THE CHIEF

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2021
Posts
330
Reaction score
962
si kila mtu anaweza kuwa kiongozi, na wote hatuwezi kuwa viongozi lakini kiongozi mzuri ni yule mwenye haiba ya (stewarship) kutunza rasilimali za watu wake, lakini pia kukubali kukosolewa na kuwa tayari kutumia karama za wengine na kuchanganya na zake ili aweze kusaidia watu anaowaongoza;
Putin aliwahi kusema; "Afrika ina rasilimali nyingi lakini ina shida ya uongozi? je ni kweli, ; kwa mtazamo wake anaamini Afrika ina kila kitu ila imekosa viongozi wenye nia thabiti na ya kweli wenye kutaka kusaidia watu wao."


Condoleeza Rice; mwana mama shupavu, the 1st woman as head of NSC, secretary of state of USA, aliwahi ulizwa kwa nini mmevamia nchi za watu, sisi hatuvaamii tu tunaangalia "american interest first' anatuma ujumbe kuwa viongozi wa marekani kazi yako kubwa ni kuangalia maslai mapana ya nchi zao.

Makamu wa Rais Zanzibar: heemed Abdula: akihojiwa na wasafi alitabainisha kuwa sisi zanzibar hatukodishi bandari mpaka tuone maslai mapana ya wazanzibar. ( nini maana ya maslai mapana), nadhani ni kuangalia namna nzuri ya kuhodhi uchumi, (win-win situation)

Rais Paul Kagame; wakati fulani aliwahi kumdhihaki mkuu wetu wa nchi wakati fulani kuwa angekuwa na bandari kama tulinavyo watanzania, basi angeweza kuongoza nchi yetu na yake bila kuomba mkopo wowote pale duniani.ujumbe kuwa tuna rasilimali ambayo sisi kama taifa hatujui thamani yake, na ukizingatia ni lango la uchumi kwa nchi zaidi ya 8 zinazotuzunguka;

viongozi wengi duniani wanaangalia uchumi wa kujitanua (expansionism) wanakwenda kuwekeza kwenye nchi zingine, wanaangalia fulsa za miaka mia au mia mbili, sio kwa sababu wataishi miaka hiyo bali wanaangali urithi wa vizazi zijavyo, ili kuwaachia nguvu ya kuwatalama mataifa mengine;, ndio maana DP world ni kampuni ya manispaa ya Dubai imeweza kulaghai na kusaini mkataba wa milele na nchi yetu.


unadhani Mkataba wa JMT na DP world ulivyokaa ni kwa bahati mbaya?
kwa upande wa Tanganyika; niungane na wasomi wa sheria na wasomi mbalimbali waliopaza sauti juu ya mkataba huu, ni ukweli usiopingika hata kama tukiandaa makongamano nchi zima, tukaanzisha semina za nchi zima, tutafute walimu tuwafundishe uzuri wa mkataba ule, ni wazi haitoshi kwani vinywa nyetu na akili zetu zitatofautiana kupokea kuwa mkataba kati ya JMT na DPW ni Mzuri na una maslai mapana kwa nchi yetu; kwa upande wetu tuwe wazi unaitwa (loose loose situation), kama alivyosema shivji, sisi kazi yetu ni wajibu na hatuna haki kwenye mkataba ule;

kwa upande wa dubai: mkataba ule ni wa uwekezaji, ni turufu kubwa kwa nchi ya dubai, na kampuni yao, kupata eneo potential kama letu, tena bila uwekezaji wowote, unakuta kila miundombili ipo tayari, na kwa muda unaotaka kwa masharti ambayo bila shaka yametoka dubai ili kutubana, ina maana wana uhakika wa kuendesha nchi yao kwa kutumia bandari zetu, wana uhakika wa kufanya biashara na nchi zaidi ya 8, bila control yoyote kutoka nchini kwetu, kwa maana ukisoma mkataba utaona wazi ni {win win situation).

dubai anaitaka zaidi Bandari kuliko sisi tunavyomhitaji, kulijua hilo angalia watz alivyolumbana wenyewe kwa wenyewe, ingekuwa ni busara wangejitoa kwanza kupisha mzozo uishe tukisharidhiana ndio wawe tayari kuja kuwekeza kama nia ni nzuri na kwa manufaa ya tanganyika, lakini si kweli bandari ina manufaa yao, ndio maana wameshikiria bomba iwe mvua iwe jua lazima mali wapewe wao.

wapi tumejikwaa?
kama taifa, tukiri wazi, hatujapata mifumo mizuri ya kuandaa viongozi wazalendo, wenye uchungu na taifa lao, ambao wana upeo wa kuangali miaka mia au mia mbili kwa ajili ya Tanzania ijayo. masuluhisho (solution) nyingi ni short plan ( malengo ya muda mfupi); ukiwauliza kwa nini wameamua kuuza bandari sasa, ( mapato madogo, watz wezi, ticks walikupowe wamefanyavibaya, tunapata bilioni 1, lakini tutapata bilion 2, serikali haiwezi kufanya biashara, tutaongeza ajira na n.k na n.k) ( all these are short plan answers), Mwalimu nyerere alipokuwa na short plan solution alishindwa kubinafishija migodi ya dhahabu, akawaambia subirini watanzania wakisoma na kupata elimu watachimba, lakini baadae walikuja viongozi wakauza na madhara mnayajua mpaka sasa, geita yamebaki mashimo na vumbi la kongo, lakin Hayati alikiri kuwahi kufanya makosa kwenye kitabu chake katika ubinafishaji.

swali hilo hilo ukiligeuza na kuwauliza Dubai na DPW, kwa nini mumeamua kuwekeza Tanzania,? majibu yao yatakuwa tofauti, na focus yao ni tofauti; ( ningeweza kuwa na projection, .............. lakini nakuachia wewe msomaji.

wapi tumejikwaa?

sehemu kubwa tulipojikwaa Waafrika, na kwa namna ya pekee Tanzania, ni kwenye uongozi, bila kupepesa macho, hatuna mifumo mizuri ya kuandaa viongozi, pia hata viongozi wakichaguliwa wanakuwa miungu hatuwezi kuwaeleza, kuwa kwa ili ulifanya hapana, hata kama jambo alilofanya ni baya na manufaa kwa taifa basi tutalikingia kifua

mifumo ya siasa zetu inaliua sana taifa letu, tunadhani watanzania wote ni wanasiasa, kumbe tunakuwa hatuwatendei. na hivyo watu wote wamekimbilia kwenye siasa, kwa sasa ili ufanikiwe vizuri ni razima uwe mwanasiasa, mtu yuko radhi asijihusishe na kitu chochote cha kuzalisha yuko radhi asubiri miaka tano, kumi ili agombee ubunge, udiwani, urais na kadhalika.

mbaya zaidi, tunatengeneza kizazi cha tegemezi, vijana wengi wamekuwa machawa wa wanasiasa, kila mbuge, diwani na hata Rais aliwahi kusema ana chawa wake mtapambana nao.

maswali kwa viongozi wetu:
1. wana mpango gani kwa taifa letu miaka mia au mia mbili baada ya kizazi chetu kwisha?
2. Nini malengo yao ya muda mrefu, na muda mfupi kwa rasilimali za taifa?
3. wakati wowaote wanaposimama kuliwakilisha taifa, je,nwako upande gani?

nihitimishe kusema kuwa:
taifa linaitaji viongozi, wazalendo wenye wivu mkubwa wa nchi yao wasio warafi wa madaka na wasio wezi wa mali za umma kwa manufaa ya vizazi vijavyo. kibaya zaidi katiba yetu haijatoa nafasi kwa mgombea binafsi, nadhani ni wakati sasa wa kuruhusu hata watu binafsi ili uwanja wa kuangalia viongozi usiwe kwenye mifumo dhalimu ya vyama vyenu vyote vya siasa. tunaitaji viongozi wapenda nchi, wasiorubunika na wenye utayari wa kuliandaa taifa kwa miaka mia na mia mbili mbele.
mungu ibariki afrika na watu wake
 
Back
Top Bottom