Sintokaa nitumie huduma za kibenki tena. Rasmi narejea kwenye miamala ya simu

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,367
Reaction score
11,604
Walichonifanyia eniembii kinatosha. Nilifungua account lao mwaka Jana November, nikawa naweka tu elfu mbili tatu kama saving, simalizi wiki, nanyofoa pesa zangu, mambo mengine yanaendelea

Mwezi Feb mwaka huu nikaweka 85k, cha ajabu leo nimejaribu kutoa 80k wakaleta ujumbe wa insufficient balance. Nikajaribu kutoa 75k wakaleta ugaigai. Nilivyowapandia hewani wakaleta habari za makato ya Kila mwezi eti 800 na makato ya mwezi Desemba na Machi 4500@ kwa lengo la kufanya anniversary na porojo nyingine kibao. Nimeona mambo yasiwe mengi, nikatoa 70k, nikavunja kadi lao kama nilivyofanya mwaka juzi kwenye siaradibii

Ukiweka 100,000 MPesa, hata ukae miaka 10, utaikuta hiyo hiyo. Maisha ni kuchagua

Ila wameniudhi sana
 
Pole Mkuu πŸ˜‚
Dah! Inaumiza sana mkuu, halafu nawapigia simu wanieleze kwa kina. Wanapokea baada ya dakika 33 huku wameniwekea kamziki kanakoimba NMB Benki yako Bora, mara karibu yako zaidi. Nikaconnect kwenye bufa nikaumbonji mpaka niliposikia "Naitwa Onesmo kutoka Daslam, naongea na nani..."
 
Unaikuta hyo hyo lakini huwezi kutoa hyo hyo
 
Umewaambia kama umevunjaa kadi yao πŸ˜‚?
 
Vichenchi kama hivyo sio vya kuweka benki ni kuweka tu mfukoni au chini ya godoro.
 
Utasikia CEO anasifiwa na mpambanaji analeta faida ,kazi za bank ni utapeli mtupu , wananyonya watu hawana kipya zaidi ya kuchukua pesa maskini.
Dah! Kuliko kupeleka pesa Benki, ni mara mia kuungana na akina mama kwenye michezo ya vikundi. Huu ujinga sirudii tena. Ni utapeli uliokithiri
 
Kuna baadhi ya card πŸ’³ hazina makato, ila Wewe ndo ulikurupuka mkuu kufungua hiyo card..
 
Vihela vidogo vidogo kama hivyo nikuweka tu chini ya godoro la sivyo unakuwa unawafaidisha mabepari wa mabenki
 
Bank wanakadi zao maalum kwa ajili ya Savings.

ATM zinatakiw maintenance, Bank Branch kuna watumishi, kuna kampuni za Ulinzi.. mifumo ni ya kulipia.. bado hasara mbalimbali..

Lazima wakukate tu, ikiw ww ni Maskini usiweke hela huko. Maan sh 800 kwa mwezi si hela ya kupigia watu kelele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…