Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Hv ni kwanini yanafahamika kama mauaji ya kimbari?? Kimbari ni jina la eneo au nini hasa??

Sent using Jamii Forums mobile app
Kimbari nadhani neno lilitumika kumaanisha" azimio la kuua idadi kubwa ya watu hasa wenye mlengo wa aina fulani..mfano nchi.dini.kabila.e.tc..kwa rwanda waweza sema ni azimio la kuua idadi kubwa ya watu wa kabila la kitutsi.( hii ni tafsiri yangu..niko " teyari" kusahihishwa.).

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Dah nimecheka [emoji3] jamaa tayari yuko halijojo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki ndio ninachokijua slim shade anatembelea kick ya genocide sympathy wakat yeye anafanya unyama maradufu ya ule na hausemwi inasikitisha sana
 

Hii anayosimulia jamaa ni genocide ya pili kwao. Iliwahi kutokea miaka ya nyuma sana, ndo ikatokea tena 1994. Tuombe Mungu kwa kweli awasimie Jirani zetu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Bossless,
Heshima kwako. Katika umri huu wa 55 napenda kukupa pole na dhoruba za maisha ya kiutafutaji. Kiukweli umepitia mengi...umeona mengi, mazuri, mabay na habari za kutisha kama hizo hapo. Mungu azidi kukunemeesha uishi siku nyingi.

Dunia haijawahi kua eneo lenye isawa wa viumbe hai (binadamu) kuishi. Habari za mlango wa nyuma zinatisha sana...dunia ina matukio makubwa ya kutisha na kuogofya.

Mkuu napenda kukupa hongera nyingi sana kwa kutuletea simulizi ya uhakika kabisa. Mm tu niseme usiyumbishwe na maneno ya watu. Waty tumeumbiwa kuongea, kwa hiyo vinywa vyetu usivipe nafasi kabisa...ww fanya liipendezayo nafsi yako. Nasfsi zetu sisi ni kuona haufanikiwi kweny malengo yako..ukituskiliza sisi walimwengu utapote. Shusha nondo mkuu wangu...tema cheche...tema nyongotukusaidie kubeba huo mzigo ulipo kwenye kifua chako angalau ubaki na furaha uweze kulionanjua siku nyingi kadrii alivokujaalia maulana.

Kudos mkuu. 🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 

Soma historia yao, mwaka 1959-1964 waliuana pia japo hawakua watu wengi. Watutsi wengi walikimbilia uhamishoni.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
andika story yako ukauze kama unaona ni rahisi
 
Muanze kujiandaa kisaikilojia Sasa mmesikia ndo wanaingia Burundi Zen Tanzania uwanja wa Vita n Rwanda ndo washaondoka hvyo.

Sio mje muanze ooh mbona imeisha, jiandaen kisaikolojia
Nliwaambia tokea Jana mjiandae kisaikolojia Mana Uzi unasema mauaji ya Rwanda na msimulizi kaadithia yote ya Rwanda na mwisho kasema wapo border to Burundi Sasa mnajiuliza nn Tena.
 
Haya mauaji yalifumbiwa macho na kila mtu hata nchi na mashirika ya kimataifa walikuwa kimya utafkir hawaoni au kuskia kinachotokea.

Haikuwa siri kila mfuatiliaji wa habari hasa za kimataifa alisikia hizo habar za jamaa kuchinjana.

Nakumbuka redio kama bbc, channel afrika ile redio ya sauzi zilitangaza sana hii ishu lakini cha ajabu hakuna aliyeonekana kusikia wala kuingilia ni kama watu walitiwa ganzi hivi kuingilia nazan kwa sabab ya ugeni wa aina yenyewe ya vita kwa sabab tumezoea vita za nch na nchi.hawa walikua wanachapana wenyew kwa wenyew.

Ila kiukweli kipindi hicho dunia ilikua ya moto sana hata ulaya kwenyewe kuna maeneo walikuwa wanachapana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nliwaambia tokea Jana mjiandae kisaikolojia Mana Uzi unasema mauaji ya Rwanda na msimulizi kaadithia yote ya Rwanda na mwisho kasema wapo border to Burundi Sasa mnajiuliza nn Tena.
Kwa jinsi tulivyo na wakat uliopo sishangai kama atakua hajaambiwa awape version watu flani waihakiki maana mjamaa ujue alikua ubalozini kabisa na ni nguli so wenyewe wanaifanyia editing.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwili wote unasisimka [emoji119][emoji119][emoji119][emoji119].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka hata wakati Mobutu anapinduliwa radio za kimataifa zilikuwa zinatangaza kuwa wanajeshi wa banyamulenge walikuwa wanaongea kiswahili safi!

Baada ya mapinduzi General Mboma mkuu wa JWTZ na Jakaya ndio walikuwa watu wa kwanza kuunga mkono yale mapinduzi kupitia BBC! Ndio maana pamoja na Mobutu kupewa msaada kijeshi na marafiki zake bado alichezea kichapo cha nguvu! Tuiheshimu sana nchi yetu! Hii nchi ina watu, Nyerere alipanda mbegu vyema!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati hii vita inatokea kule Soviet napo kulikuwa na mapigano ya kujitenga na urusi, nadhan ndo yalipewa sana airtime , Rwanda zilikua siku 90 tu za Hofu na mashaka , na inasemekana watu zaidi ya milioni moja waliuwawa ndani ya siku hizi tisini.

Sent from my SM-A207F using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…