Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Lakini ajabu dunia ilifahamu ikapuuza. Bikira Maria hadi alitokea kuonya kinachokuja lakini wale mabinti waliotokewa walipuuzwa! Ila yale mauaji ya Rwanda sijui nini kiliikumba dunia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna cha nini kiliikumba dunia, mbona hapa duniani mauaji mengi tu hutokea kuanzia kule kwa Denis sassungweso Congo brazavile mpaka kwa Seleka na antbaraka pale Africa ya kati ukiacha ule ujinga wa Syria, Iraq na Afghanistan.. Kifupi duniani tuko wengi ila wenye dunia wako wachache na hao wachache ndio wameshika remote...
 
Halafu ninachojua mimi ni kwamba asilimia kubwa ya vifo havikutokana na risasi bali majambia na silaha zingine za jadi.

Kuna maelezo ya Afisa mmoja wa jeshi la Ufaransa aliyekuwa mlinda amani huko chini ya mwamvuli wa UN alidai kwamba alitoa taarifa ya tahadhari kwa wakubwa baada ya kuwepo uingizwaji na ugawiwajwi wa majambia kwa jamii fulani pekee kabla hata Vita haijawa rasmi.

Na kuna uwezekano haya yakawa ndiyo mauaji ya kikatili zaidi kuwahi kutokea ambayo yaliuwa watu wengi kwa muda mfupi,Nagasaki&Hiroshima inasubiri interms ya ukatili though ndiyo matukio yanayotajwa kuua watu wengi kwa muda mfupi zaidi kwenye historia.

Heri risasi na mabomu au concentration camps za Hitler,kifo Cha kuchinjwa ni ukatili wa ajabu sana nashindwa hata kujua hiyo chuki ilipandikizwaje kwa jamii yote hadi watu wakafikia kiwango hicho cha hasira.
 
Hitimisho lako nilakijinga sana, huna tofauti na bashite wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza kunifananisha na Bashite sio tusi hata chembe, yaani mimi simchukii mtu hata kama tunatofautiana kimtazamo ama itikadi. Lingekuwa tusi zito ungenifananisha na wewe mwenyewe! Hakika ningeumia sana.

Ebu jifunze ku-edit fikra zako kabla ya kiziweka katika maandishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Rwanda within 90 days watu milioni walidondoka kikatili!!! Yapo majiji hapa Tanzania hayana watu milioni 1!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Askari wa UNAMIR ni kama hawakufanya kitu cha maana kuzuia mauaji yasitokee ilihali tangu 1993 walikua wanajua kua kuna mauaji makubwa yanaandaliwa. Na wakati mauaji waliweza kulinda raia wachache tu waliokua wamekimbilia kwenye hotel moja na uwanja wa mpira. Inasemekana walipewa maelekezo kutoka makao makuu kua hio haikua sehemu ya mission yao.
Mkuu! wakati raia wanauawa hovyo hawa askari wa UNAMIR walikuwa kimya tu bila kufanya kitu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila kuingilia simulizi know the following: ni kweli uliyoyasema yalitokea ila mauaji yaliandaliwa, kuhamasishwa na kuhakikisha yanatekelezwa na viongozi wa jeshi, serikali na chama chao.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…