Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Wakati hii vita inatokea kule Soviet napo kulikuwa na mapigano ya kujitenga na urusi, nadhan ndo yalipewa sana airtime , Rwanda zilikua siku 90 tu za Hofu na mashaka , na inasemekana watu zaidi ya milioni moja waliuwawa ndani ya siku hizi tisini.

Sent from my SM-A207F using Tapatalk
Lakini ajabu dunia ilifahamu ikapuuza. Bikira Maria hadi alitokea kuonya kinachokuja lakini wale mabinti waliotokewa walipuuzwa! Ila yale mauaji ya Rwanda sijui nini kiliikumba dunia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna cha nini kiliikumba dunia, mbona hapa duniani mauaji mengi tu hutokea kuanzia kule kwa Denis sassungweso Congo brazavile mpaka kwa Seleka na antbaraka pale Africa ya kati ukiacha ule ujinga wa Syria, Iraq na Afghanistan.. Kifupi duniani tuko wengi ila wenye dunia wako wachache na hao wachache ndio wameshika remote...
 
Halafu ninachojua mimi ni kwamba asilimia kubwa ya vifo havikutokana na risasi bali majambia na silaha zingine za jadi.

Kuna maelezo ya Afisa mmoja wa jeshi la Ufaransa aliyekuwa mlinda amani huko chini ya mwamvuli wa UN alidai kwamba alitoa taarifa ya tahadhari kwa wakubwa baada ya kuwepo uingizwaji na ugawiwajwi wa majambia kwa jamii fulani pekee kabla hata Vita haijawa rasmi.

Na kuna uwezekano haya yakawa ndiyo mauaji ya kikatili zaidi kuwahi kutokea ambayo yaliuwa watu wengi kwa muda mfupi,Nagasaki&Hiroshima inasubiri interms ya ukatili though ndiyo matukio yanayotajwa kuua watu wengi kwa muda mfupi zaidi kwenye historia.

Heri risasi na mabomu au concentration camps za Hitler,kifo Cha kuchinjwa ni ukatili wa ajabu sana nashindwa hata kujua hiyo chuki ilipandikizwaje kwa jamii yote hadi watu wakafikia kiwango hicho cha hasira.
 
Hitimisho lako nilakijinga sana, huna tofauti na bashite wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza kunifananisha na Bashite sio tusi hata chembe, yaani mimi simchukii mtu hata kama tunatofautiana kimtazamo ama itikadi. Lingekuwa tusi zito ungenifananisha na wewe mwenyewe! Hakika ningeumia sana.

Ebu jifunze ku-edit fikra zako kabla ya kiziweka katika maandishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna cha nini kiliikumba dunia, mbona hapa duniani mauaji mengi tu hutokea kuanzia kule kwa Denis sassungweso Congo brazavile mpaka kwa Seleka na antbaraka pale Africa ya kati ukiacha ule ujinga wa Syria, Iraq na Afghanistan.. Kifupi duniani tuko wengi ila wenye dunia wako wachache na hao wachache ndio wameshika remote...
Mkuu Rwanda within 90 days watu milioni walidondoka kikatili!!! Yapo majiji hapa Tanzania hayana watu milioni 1!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Askari wa UNAMIR ni kama hawakufanya kitu cha maana kuzuia mauaji yasitokee ilihali tangu 1993 walikua wanajua kua kuna mauaji makubwa yanaandaliwa. Na wakati mauaji waliweza kulinda raia wachache tu waliokua wamekimbilia kwenye hotel moja na uwanja wa mpira. Inasemekana walipewa maelekezo kutoka makao makuu kua hio haikua sehemu ya mission yao.
Mkuu! wakati raia wanauawa hovyo hawa askari wa UNAMIR walikuwa kimya tu bila kufanya kitu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila kuingilia simulizi know the following: ni kweli uliyoyasema yalitokea ila mauaji yaliandaliwa, kuhamasishwa na kuhakikisha yanatekelezwa na viongozi wa jeshi, serikali na chama chao.
Raia wa kitutsi na kihutu walikuwa adui.hivyo wale raia wa kitutsi walioko ndani ya rwanda walikuwa wanapenda wanajeshi wa kitutsi ( kina kagame) washinde vita ili nao wawe na power.maana walikuwa wanateseka na manyanyaso ya wahutu.ndio maana hapo msimuliaji alisema kwamba kulikuwa na watutsi wanatoroka kimya kimya wanakwenda msitunni kukutana na waasi.wanapewa mafunzo kisha wanarudi mtaani.na katika hizo safari walikuwa wanatoa siri ya mambo yaliyokuwa yanaendelea ndani ya nchi.hivyo hutu wakaona kuwa wanaishi na wasaliti mtaani.wakaona tutsi wote lao moja na waasi..ndio maana wakapanga kuwapoteza wote ...( mfano ikitokea jirani hakupendi anaenda kwa balozi wa kihutu..anamwambia mzee fulani wiki nzima hayupo mtaani ..ndio karudi leo naskia alienda polini kwa waasi..balozi atawasiliana na kiongozi wa jeshi..hapo watakuja home kukuchomoa na ndio unakufa hivyo.) ...samahani kwa kuingilia simulizi..

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom