Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Hapa namuona Niyonzima vs Kagere niwatu wawili tofauti kabisa
 
Daah Dunia ilikuwa wapi, UN mlikuwa wapi, AU je ilikuwa wapi wakati mito ya damu ikitiririka Rwanda?
Wakati wanawake wakibakwa kwa sababu tu ya “ kosa” la kuzaliwa kama mbari fulani?
Wakati watoto wakitungwa kama mishikaki na kutwangwa kwenye vinu?
Wakati vijana wakichinjwa kama kuku?
Hivi UN ilisema nini baada ya yote haya!

Kwa kweli NEVER AGAIN.
 
Mkuu MTAZAMO asante kwa Media ambayo tayari alubati alinitonya tangu jana pamoja na stori nzima "Our lady of Kibeho" Zote nimezipitia upya, hazina maudhui mapya yanayoweza kufuta kile nilichokiona Kibeho kwa macho yangu. Naweza kusema bila kuwa na nia ya kukufuru kuwa hii stori imekuzwa sana tu, haina tofauti na zile harakati za waumini wa dini ya Katoliki Tanzania, kutaka mchakato wa kumfanya Mwl. Nyerere mtakatifu. Nimefika Kibeho nikimsindikiza mtu wangu wa karibu ambaye alienda kwa nia ya kuhiji huko akiwa hapa Afrika.
 
Mi ananishambulia kinoma[emoji23][emoji23].nahisi kuna wilaya haipo sawa kwenye moja ya mikoa ya mwili wake..[emoji23][emoji23]hasa kule kaskazini unguja[emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Ana fangasi so zimepanda mpaka ubongoni!

Ana Uzi wake humu akiomba dawa za fangasi wanatafuna chiu yake!

So don't waste ur time mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaendelea...........

EeeeMRND ......eeeeee...MRND..eeeee..MRND ....eeeeee...MRnd.. ishaka rya banyarwanda , eeeee...eeee
Eeee MRN ishaka ryubumng'e na mahoro na majambele ya rubanda tweshe turagushigikie ...eeeeMRNd ikomera.×2

Huo hapo ni wimbo wa kinyarwanda wa chama tawala Cha MRND nikaona kabla hatujamalizana na rwanda wote muujue huu wimbo ,Kama nilivyosema mwanzoni kipindi hicho ulikuwa unapigwa redioni masaa 24 kwa siku hakuna kupumzika .nachotaka kusema hapa ni kwamba wimbo huo ulipigwa maksudi ili kuwakaririsha watu waamini kuwa hakuna chama kingine Cha kuwaletea maendeleo zaidi ya chama cha MRND na hakuna mbadala ,huu wimbo ulipigwa redioni Hadi wazungu wakawa wanaujua achilia mbali watoto ukabadilika ukawa Kama wimbo wa taifa yani unaweza kukamatwa na interahamwe ukalazimishwa uimbe huo wimbo Kama ukishimdwa unakula vibao vya kufaa mtu ikalazimika Sasa lazima kila mtu aukariri uujue angalau beti hiyo moja huwa si usahau Hadi Leo (matumiz mabaya ya redio yakawa yameniathiri ) haijalishi we ni mwenyeji au mgeni.imbaaa

Haya Sasa tumalize na Rwanda.......

Tukawa tumelala pale boda usiku asubuhi tukawa tunasogea kwenye kidirisha Ila uongo mbaya sikumbuki sawasawa Kama siku ile nililala usingizi au vipi huwa sina kumbukumbu sawasawa nilistukia tu kumekucha watu Wana nawa nyuso nami nikaenda kunawa uso tukawa foleni kugonga passports zetu kuwahi kupanda maroli upande wa pili ,taratibu zikakamilika

Saa mbili kamili nikawa tumeiacha ardhi ya Rwanda rasmi tunaingia ardhi ya Burundi nikasema ASANTE MUNGU ,safari ikaanza kwenda bujumbura safari ikaanza huku tukiwa na baadhi ya warundi tukawa tunapiga stori kuhusu zile maiti za mtoni usiku Ila wao wakawa wanasema zile maiti zimetoka mbali Sanaa vijiji vya mbali Burundi bado Hali sio mbaya Sanaa japo kulikuwa na tension kubwa rais wao nae alikuwa kwenye ndege iliyomuua rais wa Rwanda Habyarimana. nikajiapiza kuwa kamwe haitotokea Mimi nikanyage ardhi ya Rwanda Tena hadi nakufa hata Kama Vita itaisha nikaambiwa nirudi kazini tena ,hata ningeteuliwa kuwa balozi kamili na ndo ingekuwa mwisho wa hiyo kazi siko hiyo .( Ila miaka ya 2000' ) nilitembelea Kigali tena zaidi ya Mara mbili kibiashara lakini mwenyewe.)

tukaingia Burundi MAROLI yakaenda kupaki eneo la Gitega Kama sijakosea Ila ise nako kulikuwa na kituko ambacho kiliniacha hoi yani niliona magari kadhaa yanapishana mjini yakiwa na matundu ya risasi na polisi hawana time nayo magari ya raia tu nikawa nawaza hapaNapo sipo.tukalala asubuhi safari ikaanza rasmi kuelekea boda ya Tanzania tukavuka boda nikawa ndani ya motherland nikavuta pumzi ndefuu nikasema uuuuaaahhhhhh Asante mungu.
Kuna kitu sitaki kumaliza bila kukisema baada ya kumaliza kuvuka boada ya tanzania Kuna kamwendo kakutoka boda Hadi kuna sehemu madereva huwa wanakula na Kama kupumzika kunaitwa kwa MAMA SHILINGI Sina uhakika Kama bado kupo Kuna mgahawa hivi Sasa pale watu tukawa tunashuka ili kula nikakosa sahani ya kulia ya kuwekea ubwabwa ikabidi yule mama muuzaji anipe kikombe cha chai ili nitumie Kama Sahank na kweli nikachotewa ubwabwa nikawekewa nikawa na kula huwa nikikumbuka nachekaa sanaAaaaa...ubwabwa kwenye kikombe duuuhhh.

Nafikiri Sasa nikawa ndani ya Tanzania ..rasmi ya Rwanda yakawa yameishia hapo.

Sasa kwakuwa niliahidi kuwaletea stori yangu hadi kufika Tanzania,kuacha kazi,kujiingiza katika biashara ya chuma chakavu huko Zambia ,kufungwa jera Ndola n.k Basi niwaombe Kwanza nitengeneze simu yangu kwanza ikiwa imepona Basi ntaiendeleza Kama sehemu ya pili ya maisha yangu kujifunza tu.

Mwisho naomba niwashukuru wote kwa kunifuatilia,kunikumbisha,hata wale mliinidhihaki lakini mkawa mnanifuatilia Kiaina,Asante Sanaa..

Stori hii naamini itakuwa imewavutia wengi sio mbaya kuipeleka kokote Kama sehemu ya kujifunza lakini usisahau kutoa credit kwa Bossless mwenyewe ambae ndo mmiliki wake halali.

Asante kwa viewers na comments za kutosha. USIKU MWEMA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante [emoji120][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakukubali sana mzee wangu. Sema kuna vitu vingi tu umeviacha kusimulia vya huko rwanda...hii ni kutokana na pressure ya wasomaji. Naomba hii stori ukae chini uandike vizuri uweke kwenye kitabu.
 
M 7 tena kama yule mke wake ndo kabisa tutsi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ebhana babu la mababu, Mungu akubariki sanaa, ila ingekua vyema ukatupa mrejesho wale mabinti wa balozi wako wapi sasa, mlivyovuka boda la bongo walikua wanaonekanaje? Walikua na furaha? Bila shaka sasa iv wameshakua wamama watu wazima.
 


😇😁😅😂🤣😂😅😆
Yaani story watu walikua wanaishobokeeeea ndio imeisha hivo.
Story za kukopi na kupaste utazijua tu.
 
Huyu PK aliandaliwa Tanzania na Mwalimu kisha alipigana vita ya Tanzania na Uganda akiwa TZ na akina Museveni. Baada ya Mu7 kuingia madarakani UG, PK ndio alikuwa mkuu wa Usalama UG.

Kumbuka huyo Bossless aliposema lile defender kalikuta mpakani mwa Burundi askari wamevaa kombat za TZ na vumbi hadi kopeni. Unadhani walikuwa wanafanya nini na eneo hilo muda ule lilidhibitiwa na askari gani. PK aliandaliwa kumtoa Habyarimana na Kabila aliandaliwa kumwondoa Mobutu. Ni stori ndefu anyway ila mkakati ulikuwa unaenda kwa awamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…