Iko hivi...Congo War 1 ilikua kati ya mwaka 1996-1997. Kuna makundi manne( Mobutu Sseseko, Laurent Kabila, Paul Kagame, Yoweri Musseveni) yaliyopigana vita hii na kila kundi lilikua na interest zake tofauti.
Vita hii ilitokea DRC kipindi hicho ikiitwa Zaire ilianzia pronvince za kaskazini mashariki Nord na Soud Kivu, ikaelekea Kisangani mpaka DRC magharibi then Kinshasha ilipoisha na kuondolewa madarakani kwa Rais wa kipind hicho Mobutu Seseko, nchi ikatwaliwa na Laurent Kabila aliyebadili jina la nchi kutoka Zaire na kuwa Democratic Republic of Congo.
Kwa kifupi ni kwamba wakati vita hii inaanza Mobutu ndiye alikuwa rais halali wa DRC na Laurent Kabila Sr ndiye alikuwa muasi akipigana kutoka msituni mashariki ya Kongo. Kabila alipata msaada wa kijeshi kutoka kwa majeshi ya Rwanda na Uganda chini ya Kagame na Mseveni. Lengo la Kagame si kwamba alikua sympathizer wa movement au uasi wa Kabila bali lengo lake lilikua ni kuwamalizia mbali wahutu na interahamwe wote waliokimbilia Congo baada ya genocide ya 1994 na pia aliona fursa kwenye madini adhimu ya Congo.
Museveni ye hakua interested na wahutu bali ye pia aliona fursa kwenye madini. Sasa basi majeshi ya Rwanda chini ya Gen James Kabaerebe, uganda pamoja na vikosi vidogo vya waasi wa congo wakiongozwa na Laurent Kabila walivamia Congo mwaka 1996 na kuanza kuuwa interahamwe , kushambulia majeshi halali ya Congo ya Mobutu, wakasonga mbele Toka Goma, kwenda Kisangani, kindu, kinanga mpaka walipofanikiwa kuuzingira mji mkuu wa DRC Kinshasha na kumuondoa madarakani Mobutu Seseko, na kufanikiwa kumuweka kibaraka wao Laurent Kabila kama rais mpya wa DRC. Kabila aliwatunuku vyeo jeshi maafisa waandamizi wa majeshi ya Rwanda ilhali hawakua raia wa Congo.
Ambapo Gen wa kitutsi James Kabarebe aliyeongoza vikosi upande wa Rwanda akipewa cheo cha mkuu wa majeshi CDF. Kilichofuata hapo ni historia ilikua ni kuchota madini tu na kuuwa wahutu/interahamwe wote waliokua wakionekana kama threat kwa serikali ya Rwanda chini ya Kagame. Na pia ndipo kipindi hiki wakasimikwa waasi wa Kitutsi mashariki ya DRC wanaoisumbua serikali ya DRC mpaka leo hii.
Madini yalichotwa na wahutu waliuuwawa mpaka sense ilipomuingia Laurent Kabila ambapo katika kujaribu kutokomeza hali hii akamfukuza na kumvua vyeo vyote CDF wake wankinyarwanda Gen Kabarebe mwaka 1997.
Hali hii ilimchukiza Kagame na swahiba wake Museveni ndipo mikakati ikaanza ya kumng'oa madarakani Laurent Kabila iliyopelekea vita iliyokuja kupewa jina ya Congo War 2.
Ni historia ndefu ila kwa kifupi tu ni kwamba zilitafutwa mbinu nyingi za kivita na za kiinteligensia za kumuondoa Kabila Sr mpaka walipofanikiwa kwa msaada wa CIA ambapo mwaka 2001 Laurent Kabila akiwa ofiain kwake Ikulu Kinshasa alipigwa Risasi na Bodyguard wake karibu, na Bodyguard wake pia akapigwa risasi na mpambe wa Rais (ADC) Eddy Kapend, naye pia kabla ya kuwekwa nguvun katika ile taharuki akapigwa risasi na mlinz mwingine aliyetokomea kusikojulikana. Mpaka leo mauaji ya Rais Kabila Sr yanabaki kuwa ni mystery maana walioshuriki katika kufyatua risasi nao pia waliuawa kama cover up.
Baada ya kufanikiwa katika mauaji haya, Joseph Kabila ambaye ni mtoto wa kambo wa Kabila( si mtoto wake by birth) mwenye asili ya kitutsi akakabidhiwa madaraka ya DRC kama Rais. Joseph kabila ni mtusti, mzaliwa wa Rwanda na ni mpwa wa Gen Kabarebe. Alilelewa na Kabila Sr toka akiwa mdogo baada ya baba yake ambaye alikua member wa jeshi la waasi wa Kabila mashariki ya Kongo alipofariki katika umri mdogo, Laurent Kabila Sr akamchukua Joseph na kumlea kama mwanaye, ila Joseph Kabila si mtoto wa kuzaliwa na Laurent Kabila .
Toka mwaka 2001 baada ya Rais Joseph Kabila Jr kuchukua madaraka rasmi kama Rais, plunder na looting ya madini kutoka DRC na kusafirishwa kinyemela kwenye mataifa ya magharibi kupitia Rwanda Kigali inaendelea na itaendelea mpaka kesho as long as Kagame yuko madarakani.
Pichani chini ni Joseph Kabila akiwa na Uncle ake Gen James Kabarebe (ambae amehudumu kama CDF na minister of defence katika serikali ya Kagame kwa miaka mingi toka 2000 mpaka 2018).
Huyo mrefu katikati mwenye sare ya Jeshi ndo Gen Kabarebe na kulia kwake ni Joseph Kabila , hapo walikua Kigali 1998.
View attachment 1384017