Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

We Bossless acha ufala nawe nae! Kisa hawa waropokaji ndio ukatishe uhondo, haya mangapi huko mtaani unakutana nayo, hebu leta stori mzee tusikerane dingii!!

Nimejitahidi kusoma nipate mwendelezo, halaf nakutana na hii comment yako, bila shaka we ni mkubwa wangu ila haki ya nani vile ungekuwa karibu ningekupiga mbonge wa mbichwaaa!! [emoji13][emoji23]🤣

Leta mambo bwana usiwe kama vile una pumbu moja mkubwa wangu [emoji848][emoji13][emoji23]🤣

Halafu safari nyungine iandike yoote kisha utupie hapa na sie tutiririke nayo moja kwa zoote!

Ahsante saana!
 
Asante mkuu kwa mwendelezo,ila nna mawasali hivi kati ya hao wa tutsi na wahutu ni yupi alianza kumbagua/kuua mwenzie?na kati ya hao yupi ni mkatili kuliko mwenzie?
Jibu lako nikujibu kama ifuatavyo don't trust rwandese ,mtusi akiwa madarakani mhutu anapata cha mtemakuni kama ilivyo sasa japo now inafichwafichwa kidikteta na mzee PK so ukitembelea magereza yote ya rwanda waliojazwa humo ni kabila la Wahutu, Watusi ni asilimia chache sanaa na mhutu akiwa madarakani cha moto anakiona mtusi mfano enzi za habyarimana hayo mengine ya miaka sijui ya 50's na 70's huwa nasoma tuu kama wewe unavyoyasona kwenye stori za rwanda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We Bossless acha ufala nawe nae! Kisa hawa waropokaji ndio ukatishe uhondo, haya mangapi huko mtaani unakutana nayo, hebu leta stori mzee tusikerane dingii!!

Nimejitahidi kusoma nipate mwendelezo, halaf nakutana na hii comment yako, bila shaka we ni mkubwa wangu ila haki ya nani vile ungekuwa karibu ningekupiga mbonge wa mbichwaaa!! [emoji13][emoji23]🤣

Leta mambo bwana!
Story ishaendelea na iko mbali sana tafuta humu humu kwwnye comment
 
Asante mkuu kwa mwendelezo,ila nna mawasali hivi kati ya hao wa tutsi na wahutu ni yupi alianza kumbagua/kuua mwenzie?na kati ya hao yupi ni mkatili kuliko mwenzie?
Watusi ni akina Kagame ambao leo ndo watawala, ukiconnect dots, ni kama vile kabla watusi hawajashika hatamu na kuonyesha ubabe wao kama malipizi, tayari walinyanyasika kiasi cha kutosha. Ngoja mzee wetu aendelee kumimina matukio...

Wenzangu na mimi mnaojifunza Kinyarwanda twende pamoja:
Mugore (mke/demu)
Amakuru (Mambo/habari yako)

Niliona Niyonzima wa Yanga ana binti mrembo, nitakuwa na pa kuanzia nikitupa ndoano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu kwa mwendelezo,ila nna mawasali hivi kati ya hao wa tutsi na wahutu ni yupi alianza kumbagua/kuua mwenzie?na kati ya hao yupi ni mkatili kuliko mwenzie?
Hebu google ... ni historia ndefu ..acha atupe simulizi tu..hiyo simu unaitumiaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LIKUD,
Mbona inaonekana wewe ndiye una haraka? Wengi tunafahamu kwamba vita imeanza mwezi huo wa nne hadi wa saba tena mwaka 1994.

Yeye ameanza na mwaka aliomaliza masomo ya stashahada mwaka 1989 na kupata kazi kwenye ubalozi huko Rwanda. Bado anaendelea na background hajafikia kipindi vita imeanza.
Kama ni hivyo aunganishe na vita ya Guba ya uajemi miaka ya 1990 mathafanta huyu
 
Ninavyopenda story hapa nimeshawaka... leta vitu Mkuu.
Halafu hii tabia ya watu kuvamia story na kukashifu kuwa ni uongo, ya nini? Kama unaona story ni ya uongo si uachane nayo?
Ustaarabu ni jambo la msingi linalowashinda wengi, hakika.
Hakuna ustaarabu humu.....
ww binuka staili unayoona inakufaa...
 
Inaendelea.........

Habari za mchana wandugu ,sasa tuendelee leo ntajikita kuelezea matukio mbalimbali ya unyanyasaji, uonevu, mauji, uporaji ulianza kujitokeza . nitajitahidi kuelezea niliyoyashuhudia kwa macho yangu ya yaliyotutokea sisi kama sisi maoneo ya kazi... (ubalozini). Haya matukio yamejaa kichwani kwangu kwa kipindi cha mda wa miaka mingi hadi huwa yananikoseha raha wakati mwingine naota kabisa hadi na weweseka vibaya ndugu zangu msiombe vita narudia tena usiombe vita ( utasikia kijana humu anasema bora kinuke aise tema mate chini).

Tukio la kwanza -: hii ilikuwa kipindi hicho hicho mwaka 1992 kama sijasahau mwezi wa nne hivi kama unavyojua mpaka hapo tayari nimeshakuwa na Demu mweupe mfupi kiasi ila alikuwa mzuri ( hapo naona vijana wa mambo yetu wanaanza kutabasamu hhhhaaaa ...) nikiwa nae kwenye mahusiano kama miezi minne hivi sasa kukawa kuna sehemu moja hivi town kulikuwa linapigwa disco kama lile lilokuwa linapigwa pale mikocheni (blue palm eneo dogo lakini weekend wanakaa watu nyomi hatari mziki unapigwa balaa,kwaa taarifa tu eneo lile lilikuwa haliguswi na Askali yeyote yule au interahamwe au kwenda pale kuanzisha vurugu unajua kwanini? Eneo lile ni la Kada wa eneo lile mtemi na msumbufu aliitwa Nyihibilazi (balozi) na disko la kwake sasa mnanza aje? Kwanza mlangoni ukiingia unakuta Askali wake wana AK 47 na magrouneti yapo nje nje.

Basi disko likapigwa kufika mida kama saa kumi hivi nikamwambia demu wangu tuondoke enzi hizo tunakula Mai hatari (pombe) kwa kwenda mbele mzee unakula primus hadi unazima watu wanakubeba kukurudisha nyumbani, basi mtu mzima nikashika chombo( demu) yangu kiuno nikawa nashuka nayo lami kutokea ukumbini kama kuna kilima unashika unaenda lami kuu ndo unasimamisha texi ya kurudi home ,ile namalizia tu kilima kile kwa mbele kidogo nikaona Toyota hilux inakuja wamejaa interahamwe tupu na mabunduki i yao .
Kufika tu mbele wakasimama wakawa wanarudi nyuma aise asikwambie mtu pombe inaleta ujasiri,nikamwambia demu wangu hakuna kuongea chochote hata akiuliza jina lako labda aulizwe kwa kiingereza au kiswahili ndo ajibu, siku hiyo alivaa tisheti yangu zile za watalii zimeandikwa HAKUNA MATATA zilikuwa sinatengenezwa kenya kama sijasahau, basi majama yakawa yamefika pale kwanza wakaanza kukoki mibhnduki yao ebwaanae nikasema sasa tumekwisha lakini niwaambie mwanaume kama una mapenzi na demu wako aise hata itokee hatari gani lazima unamtetea tu hata kama kuna hatari kiasi gani basi swala la kwanza wakatuuliza tulipitokea niliwajibu disko wakasikia refudhi yangu ya kiswahili wakasema nyinyi ni waswahili? Nikamjibu ndio wakauliza watz yani watanzania wanafupisha nane tz nikasema ndo kumbuka nilimwambia demu asiongie hata akipigwa kibao, moja anaiuliza na huyu mugole? (Mugole-ni mwanamke nikamjibu mke wangu) kumbuka hapo kinyarwanda nimeshaanza kukipata pata ila kuongea ikawa shida kidogo, sasa ikatokea ubishi miongoni mwao baadhi yao wakawa wanahisi yule si mtz ni mnyarwanda wengine wakawa wanananiamini mimi hapo sasa ndo kimbembe kilipoanza

Vuta ni kuvute kumlazimisha demu aongee demu anasem na mimi nawaambieni huyu hawaelewi nyinyi huyu ni mtz kwanza haelewi mnaongea nini wakaomba ID ninatoa passport jina moja wakaomba ID ya demu ikiwaambia ipo ubalozini kama vipi twende nikawaonyeshe wakagoma ,demu waNgu yupo kimyaa, sasa ipo hivi yule demu naweza mfananisha na kama msanii Menina ya ni mweupe ana sifa zote za kitusi ila pua lake tu ni pana kidogo kama unavyomuona Menina ,sasa wakawa wanashindwa wafanye nini kumchukua hawawezi wanahisi ni mtz sasa mimi wakati huo nachapa kiswahili hatari na vijimaneno vya hapa na pale ghafla ukaingia ujumbe kwenye redio call yao nikasikia maneno flani nikaona wanaitana wakapakiana kwenye gari na kuondoka pale pale nikawahi texi tukarudi nyumbani na sikumpeleka kwao nilienda kulala( ikawa furaha tosha kwetu kwa usiku huo naona vijana wanatabasamu hapa hhhaaaaa.....) hakika yule demu alinipenda sanaa kwa lile tukio akaja akawa anawahadithia ndugu zake pale mtaani tukawa vile mke na mume aise anakuja nyumbani anytime mungu amsaidie huko aliko kwani tulipoteana tu uenda simu zingekuwepo au mitandao tungetafutana ( jina kapuni) ntaalezea baadae tulivyopoteana vita.. vita ...vita ..baba mbaya sanaa sasa sijui yuko hai au alishakufa ? Maisha yakaendelea...

Tukio la pili-: nilishuhudia saa nane mchana eneo la birjogo( tamka bijogo) hiace nzima ya abiria watu wakashushwa wanapigwa fimbo wakachambuliwa wakatolewa INYEZI ( inyezi maanake mende yani Watusi) wakatandikwa virungu vya kufaa mtu sasa hapo niliona kada (balozi )hilo analisimamia mwenyewe, sasa utamtambuaje balozi katikati ya interahamwe? Yeye anakuwa amevaa belleti nyekundu na shati la chama aisee wale watu walipigwa walikatwakatwa na mapanga huku watusi wakipata mateso makali sanaa ,unajua kwanini ?nilikuja kugundua baadae sanaa kwanini Watusi wanateswa. Sasa ipo hivi wakati Rpf wanaanza chokochoko walikuwa wanapewa taarifa na Watusi wa ndani n baadhi ya ndugu zao wanaume walikuwa wanaenda kwa siri kupata mafunzo maeneo mbali mbali karibu na walipokuwa waasi sasa taarifa hizo zikawa zinawafikia mabalozi mbalimbali nao wanazisambaza kwa interahamwe sasa usiku unashangaa unavamiwa na hao jamaa wanakula kisago halafu wanaondoka na wewe ni ndo imetoka hakuna anaejali basi wakawakatakata mapanga wale Watusi pale shell kituoni cha mafuta hadi leo picha hii huwa hainitoki akilini kuua kwa mapanga zaidi ya watu 12 wanauawa machoni mwangu kweupe pakavu jua la saa saba mchana then nobody care .

Nimesema hapa leo naweka matukio....ya kinyama.

Itaendelea jioni hii......................... Msichoke.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole kwa kupoteana na mtoto mzuri cheupe.
Nilipofika kusoma hapo, nimesikitika sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni juzi tu weekend nilikuwa naangalia "SOMETIMES IN APRIL", so touching. Kila nikiangalia ile movie nilikuwa najiuliza nini kiliwaingia hawa watu, yaani unyama unyamani, whoever engineered the massacre in Rwanda anastahili kuchapwa risasi mwili mzima.

Mkuu wewe endeleza story, tupo interested kupata picha halisi za mtu aliyeishi huko, humu tupo wa aina tofauti, na umri wako hutakiwi kuweka vitu rohoni, kuna kiharusi na shinikizo, sio vitu vizuri hivyo.
 
Bossless,

We Muongo, ulienda mwezi WA sita hahahaha.

Vita imeanza mwezi WA nne imeisha mwezi WA Saba but wewe ulipata KAZI mwezi WA sita wakati serikali ya Rwanda imevurumishwa na Rpf na kukimbilia Gisenyi Kwa kina Haruna Niyonzima huku mapigano makali yakiendelea.

Anyways wakati unapata hiyo KAZI Rais wa Rwanda alikuwa anaitwa Nani?

Jibu huna Mpira uishie hapa.

" falsus in uno falsus in omnibus" false in one thing false in every thing.

@moderators futeni uzushi huu unachafua hadhi ya jf
Alfu eti kapanda bus to kahama,mfanyakazi wa embassy unapewa elfu 60tsh then na kupanda bus?eti nikapiga Sim! Urikua unatembea na Sim ya fix?
 
Back
Top Bottom