Inaendeleaaa...........
Nilipoishia nikiwa IMhala hoteli najiandaa sasa namna ya kuwahi kuamka mapema kuwahi kituoni kwangu kuripoti asubuhi. Mapema tu nikaamua nikajianda safi kabisa nikaanza safari ya kuelekea kituoni kwangu, nikashudia kitu cha ajabu ambacho sikukizoea .Dar ukiamka saa kumi na moja alfajiri kwa miaka hiyo hata kwa sasa ukifika stand utakaa tu kidogo hadi saa kumi na mbili au nani nusu hivi unaweza kuwa umepata usafiri na kuondoka iwe kwa texi au daladala wanyarwanda swala la kuamka mapema hilo kwao hapana labda sijui kama wamebadilika kipindi hiki, basii mtu mzima nikawa stand barabarani nasubiri daladala huwezi amini hadi saa moja moja kamili asubuhi hakuna cha daladala wala nini nikamuuliza jirani yangu pale stand hii ukoje akaniambia mabasi yanaanza kufika saa mbili kamili au na nusu nikamuomba anionyeshe texi nipande akaniambia hakuna stand ya texi Unachotakiwa kufanya unasimama barabarani unapungua gari lolote dogo mkono itakayosimama basi hiyo ndo taxi mnaelewana bei anakupeleka, mimi nikafanya hivyo kweli nikawa nimepata usafiri tukaelewana (sikukumbuki tulikabiliana bei gani ila alipeleka hadi ubalozini getini) nilishuka nikajitambulisha kwa mlinzi akiniruhusu kuingia ndani nikaingia hadi mapokezi nikatoa barua yangu ya ajira nikapokelewa safii kabisa na watumishi wenzangu sasa hapo nikawa majihisi nipo nyumba tunaongea lugha moja tunaelewana safii mzee nikapumzishwa sebule ndogo kumsubiri balozi afike nijitambulishe ili sasa taratibu zingine zifuatwe.
Muda si mrefu balozi akafika alikuwa mwanamama mweupe kama mpemba mama mtu mzima( naomba nisilitaje jina lake) akanikaribisha tukaongea maeneo ya hapa na pale ikawa baadae akaaga nikabaki na wasaidizi wake sasa ndo nikawa nimeingia mzigoni rasmi nikiwa na mabegi yangu yote( ikumbukwe kule hotelini niliaga kuwa sirudi hivyo niliondoka na kila siku changu hadi ubalozi).
Iko hivi ubalozi wowote lazima uwe na baadhi ya vyumba vya siri na wazi hivyo vya siri( naomba nisivizungumzie na kazi yake ni nini kwa kuwa sio lengo) basi katika vile vyumba viwili nikakabidhiwa chumba kimoja kwa ajili ya kupumzika mimi na mizigo yangu nikawa naishi pale ubalozini kwa muda kama week mbili hivi nalala naamka nafanya shughuli ndogondogo za ofisi mda wa kazi ukiisha watumishi wenzangu wananitembezA mjini ,taratibu nikaanza kuzoea mjii mawazo ya kupanga uswahili yakaanza kuingia akilini mwangu ,baada ya muda nikaomba kuhamia mtaani nikakubaliwa bila shaka ( hili niliweka sawa kwanza madhumuni ya vyumba vy pale ubalozini sio kufanya kuwa makazi ya kudumu unakaa kwa muda unajipanga kidogo then unaanza kuishi mtaani) .
Basi mzee mzima nikapa nyumba yangu pale Gikondo karibu na bandari kavu huwa wanakuita MAGERWAA kama sijakosea speeling basi nikawa nimepata nyumba nakuanza maisha nikiwa single kabisa sina hata mtoto wa kusingiziwa nje maisha ya kaanza hapo ( RWANDA hadi sasa hakunaga mambo ya kupanga chumba kimoja kule ukipanga unatakiwa upange nyumba nzima ) maisha yakawa yanaendelea ni kazini nyumbani taratibu vijana wakaanza kunizoea majirani wote wakaanza kunizoea pia sasa sikujua walikuwa wanavutiwa na nini kwangu ila baadae niligundua kuwa walikuwa wananipenda kwasababu naongea kiswahili hivyo nikiwa naongea wanafurahi japo sikuwa na uhakika kama wananielewa au vipi? Akafikia hata wakifanya sherehe zao majirani lazima wamletee barua ya mwaliko mimi nikihudhuria wanafurahi sanaa walikuwa wananiita mswahili. Neno la kwanza kujifunza la kinyarwanda ilikuwa salama AMAKURU yani habari yako.
Maisha yakaendelea pale kazini, ikawa ni mwendo wa kazi kwenda mbele hadi kufikia mwaka 1990 hapo yani nikawa na miezi sita na siku kadhaa kigali miezi yote hiyo nilikuwa sijatoka nje ya mji wa kibali.
Niseme mwaka huo ndo nilianza kupata ufahamu juu ya maisha halisi ya Wanyarwanda mtaani kwangu ikawa nikialikwa kwenye sherehe nakuta watu wale wale (naomba nieleweke hapo kwa mfano unaishi mtaa moja kuna kaya nyingi tu lakini ule mtaa ukawa kama kuna mgawanyiko flani hivi yani ukiitwaa kwa mzee john unamkuta mzee Amosi yupo hivyo kwa mzee Amosi unakuta mzee john yupo halafu mtaani kuna watu wengine hawashirikishwi kabisa japo wapo mtaani hapo.) hii ikawa unanitatiza ikabidi nianze kufanya utafiti wangu kwa siri ikiwemo kuwauliza watumishi wenzangu pale ubalozini.
Pale ubalozi kulikuwa na dereva ambao alikuwa anasaidia anahudumu pale ubalozini,siku moja nikamuuliza kuhusu hilo jambo alichonijibu ni kuwa hicho kinachotokea na ndo maisha halisi ya Wanyarwanda yani Watusi na Wahutu hawafungamani katika mambo mbalimbali akasema kuwa kuna hali ya ubaguzi wa hali ya juu hasa Wahutu kuwabagua Watusi ambao ni wachache sanaa na hilo ndo nilipokuwa nilishuhudia kwa takribani kipindi cha mwanzoni ila nikawa siajelewa mtusi yupo na mhutu yupo na unamtambuaje mtusi na mhutu unamtambua aje ukawa mtihani sasa kwangu.
Baada ya kulielewa hilo sawasawa ndo ikawa sababu ya mimi kukacha tena kwenda kwenye sherehe za majirani kwani nilihisi kinachotengezwa hapo si jambo jema ikafikia mahala jirani akiniiona nimesimama na jirani mwingine ana nuna au ananipita bila hata kutusalimia ikawa inanishangaza kwakweli CHUKI YA UKABILA NI MBAYAA SANAA.usiombe.
Maisha yakaendelea kama kawaida ila nikaona Nihamie mtaa mwingine kuwakomoa wale majirani, nikawa nimehama pale nikahamia mtaa mwingine nikajitahidi nisiwe na mazoea kama ya awali nikawa ni kazi ,nyumba ,matembezi mjini kurudi nyumbani na kulala.
Hatimae mwaka ukapita ukaingia mwaka wa pili ya ni 1992 hapo ndipo kuna kipindi rwanda kukawa na mambo ya ajabu sanaa yani mnaweza mkawa mmelala wanakuja watu wana silaha, mapanga na mashoka usiku wanawamsha wote mnawekwa kwenye foleni unasikia huyu ni ing'otanyi ukiambiwa hivyo ujue jamaa watakuchukua wanaondoka na wewe ndo kwa heri na ukujifanya kubisha pale pale unageuzwa asusa yani unakataa katwa mapanga watu wanakuona ,ila niligundua waliokuwa wanafanyiwa hivyo wengi wao waikuwaWatusi wakawa wanadai kuwa huwa wanatoroka kwenda kupata mafunzo ya kijeshi polini na wanarudi kimya kimya uraiani kuchora ramani ya uvamizi kuisaidia kikundi cha waasi wa RPF.kwa miaka hiyo uvamizi wa RPF maeneo ya mipakani ulikuwa wa mara kwa mara hadi kufikia jeshi la rwanda kuhamia mipakani kulinda ila mashambulizi hayakukomaa japo majeshi ya serikali yalikuwa tunajitahidi kuzima uasi
Sasa turudi kwa wale watu wanaokuja usiku na bunduki na magruneti na mapanga kusaka watu wanaowaita ing'otanyi ,badaae nikagundua kuwa wale jamaa wanaitwa interahamwe yani kwa kiswahili wavamizi wa pamoja hapa naomba niongelee jambo moja muhimu sanaa kwa faida ya wasomaji, dalili ya kwanza kabisa ya uvunjifu wa amani au vurugu za kikabila au vita ni pale utakapo ona vikundi vya kisiasa, au vya kidini vinakuwa na walinzi au vikundi vya ulinzi halafu wanamilishwa bunduki halafu mkuu wa jeshi la polisi au majeshi anakaa kimyaa hakemei wala kutoa katazo lolote ukiona hivyo Unachotakiwa kufanya uza mali zako zote hamia nchi unapoona wewe ni salama kwako mapema sanaa.
Kilichotokea interahamwe walikuwa kwa mfano kama green gard wa Ccm au red bregard wa chadema , mara ghafla wakawa wanaonekana mtaani wamevaa nguo za chama chao cha MRND wakiwa na silaha kabisa za kivita wanatembea mtaani wanaimba nyimbo za kujipamba chama chao na rais wao hii maanake nini ukiona hivi juu chama tawala hakina imani tena na jeshi hivyo wakaona bora silaha zinaoagizwa na serikali wapewe makada wa chama wajilinde wenyewe, makada wakawapa interahamwe, interahamwe wakawa wNaogopeka kuliko hata polisi au jeshi wakiingia dukani kwako wakichukua mkate au siagi haruhusiwi kuhoji, kuhoji tu umekula kwako utachakazwa kwa kipigo vibaya sanaa sasa ikawa ukiwa na kesi hata kama aliekuonea ni interahamwe ukipeleke kesi polisi hakuna kitakachoemdelea ,kama umemkariri nenda kwa bosi wake huwa anakuwa Kada wa chama mfano mabalozi unamuelezea pale kwa kutia huruma ndani ya dakika sufuri anaitisha gwaride kama huyo aliokuonea ni wa eneo hilo ukimtambua anamcharaza vibaya fimbo mbele za watu ata kama kakupora kitu lazima arudishe hapo hapo ikawa inankishangaza sanaa binafsi nikiwa eneo la nyehere-gikondo kuna moja alinipora saa nikaenda kwa kada akaitwa akanirudishia tena bila ubishi kama kauza au katupa analipa pesa atakayoitaja kada (balozi) haijalishi hicho alichokupola kina dhamana gani.
Leo nimejitahidi kuandika ndefu nitaendelea kesho nimechoka sanaa........itaendelea.
Sent using
Jamii Forums mobile app