Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Mkuu naomba link ya sehemu ya Pili na tatu kwenye stori hii
Angalia ilivyo
Screenshot_20201115-102110.jpg
 
Kwa uzoefu wangu sisi bado sanaa.nchii hii hata aasi CDF hakuna mtanzania atakaethubuti kuingia barabarani kumtetea Mh. Rais. Uoga, unafki na kujipendekeza kila mtu atacheza kwenye nafasi ili awe mshirika atunishe tumbo lake si mnaona yanayoendelea nchini .tawala zilizopita zilitujengea mazingira ya kupuuza na kuacha yapite. Mf. Uchaguzi wa serikali za mitaa watu wamesahau sasa wanapiga kelele tume huru nalo litapita maisha yataendelea. NAKUPENDA NCHII YANGU TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu uliona mbali sana
 
Ndege hio wakati inadunguliwa nilikua Kigali usiku huo. Eneo ndege hio ilipodunguliwa linaitwa Kanombe jirani kabisa na uwanja wa ndege na ikulu ya wakati huo.
1. Mleta uzi ametaja kua ubalozi ulikua eneo la Kicukiro jambo ambalo kama lingekua kweli ukiwa eneo hilo huwezi kuona anga ya eneo la tukio.
2. Ubalozi wa Tanzania ulikua eneo la Kacyiru ni karibu na eneo la tukio na ilisikika milipuko miwili hivi na mwanga sisi hatukuona wingu.
Note: Balozi zote na mashirika makubwa ya UN au ya kimataifa yalikua katika maeneo matatu (Kacyiru, Kimihurura na Kiyovu)
3. Njia waliopita hao ni ndefu sana na unavuka na unavuka wilaya kama tisa hivi kama sijasahau.
4. Diplomats wengi na wafanyakazi wa UN agencies wengi ilikua wakipata shida wanaita wanajeshi wa UNAMIR sijui kwa nini wao hawakuwajua!!!
Nina historia mbaya katika safari nilizofanya kule kati ya 1990-1994.
Mleta mada usichoke kuwahadithia watu humu kuna mengi ya kujifunza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ni vyema ikikupendeza, tufungulie uzi pia utufunze zaidi na Sisi pia kupitia ww na mzee wetu hapa naimani kuna madini mengi sana tutapata
 
Dikteta Mobutu alikuwa mshikaji wake Habyarimana wa kufa na kuzikana. Ukifika eneo hilo yalipokuwa makazi ya Habyarimana nyuma ya nyumba kwenye bustani utaona kibwawa kidogo ambacho simulizi iliyopo ni kwamba enzi za Habyarimana kuliwekwa chatu mwenye urefu na uzito mkubwa sana ambaye alikuwa akitumika kwa mambo ya kishirikina ikiwa ni pamoja na kufanyia kafara. Na huyo chatu alikuwa kapewa na rafikie Mobutu ili kufanyia huo ushirikina. Usiku ule ule Habyarimana alipouawa hilo chatu nalo lilipotea katika mazingira yasiyoeleweka na hadi leo halijawahi kuonekana tena.

Kingine ni kwamba mara baada ya Habyarimana kuuawa mwili wake ulichukuliwa kwa siri na kupelekwa huko Zaire (kwa sasa DR Congo) na Mobuto kuuhifadhi huo mwili wa best yake nyumbani kwake kwa miaka kama mitatu hivi hadi pale na yeye alipokaribia kupinduliwa na waasi wa nchini mwake ndipo akaamua kuuchoma moto!
Duh very interesting aisee
 
Acha tu bro, bossless kanikumbusha moja ya tukio baya sana nililiona kwa macho yangu nikiwa na miaka 10 jamaa walikuwa wawili ilikuwa saa tisa na dk 17, alasiri tarehe 26/4/1994. Utanzania uliniokoa dogo huyo aliyekuwa rafiki yangu alipewa thiodan ile dawa tunayopulizia nyanya shambani dogo akawaambia anasikia kiu wakamwongeza nyingine alikufa namwona hv siku nilipoenda musozi kwa mara ya kwanza niliona picha ya dogo pale ndio maana naamini dogo amelala pale afu babu yake wakaondoka nae sijamwona hadi leo

Yaan ningekuwa na uwezo wale jamaa nikiwakuta jehanamu au mbiguni niwauwe tena[emoji24][emoji24][emoji24] basi tu

Rip Jean, babu huko uliko neema za Mungu ziwe nawe

Sorry bossless kuingilia uzi wako

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah, hvi hawa jamaa walipewa sumu gani hizi mpaka kufikia ukatili wa namna hii aisee
 
Eeh Mungu saidia Tanzania isijetokea vita! Hii story imenipa depression for real! Naweza hitaji therapy. Vita ni mbaya sana. Namtukuza Mungu kwa amani ya Tanzania
 
Askari wa UNAMIR ni kama hawakufanya kitu cha maana kuzuia mauaji yasitokee ilihali tangu 1993 walikua wanajua kua kuna mauaji makubwa yanaandaliwa. Na wakati mauaji waliweza kulinda raia wachache tu waliokua wamekimbilia kwenye hotel moja na uwanja wa mpira. Inasemekana walipewa maelekezo kutoka makao makuu kua hio haikua sehemu ya mission yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bro ukiwa mission area ndo utaelewa maana halisi ya haya mambo. Unapokuwa huku unaambiwa jukumu lako la msingi ni ulinzi wa raia( protection of civilian) lkn kiukweli kaka hamna kitu kama hicho ni maigizo tu. Raia wanaweza wakawa wanachinjwa kijiji jirani kabisa na kambi yenu lkn hamruhusiwi kutoka kwenda kuwasaidia kama lengo letu linavyosema, zaid mtasubl wavamiz wakishaondoka nyie muende kukusanya miili tu ya waliokufa na kuwatibu majeruhi. Hivyo msiilaum UNAMIR kutokufanya chochote kipindi hicho
 
Aisee
Bro ukiwa mission area ndo utaelewa maana halisi ya haya mambo. Unapokuwa huku unaambiwa jukumu lako la msingi ni ulinzi wa raia( protection of civilian) lkn kiukweli kaka hamna kitu kama hicho ni maigizo tu. Raia wanaweza wakawa wanachinjwa kijiji jirani kabisa na kambi yenu lkn hamruhusiwi kutoka kwenda kuwasaidia kama lengo letu linavyosema, zaid mtasubl wavamiz wakishaondoka nyie muende kukusanya miili tu ya waliokufa na kuwatibu majeruhi. Hivyo msiilaum UNAMIR kutokufanya chochote kipindi hicho
 
Bro ukiwa mission area ndo utaelewa maana halisi ya haya mambo. Unapokuwa huku unaambiwa jukumu lako la msingi ni ulinzi wa raia( protection of civilian) lkn kiukweli kaka hamna kitu kama hicho ni maigizo tu. Raia wanaweza wakawa wanachinjwa kijiji jirani kabisa na kambi yenu lkn hamruhusiwi kutoka kwenda kuwasaidia kama lengo letu linavyosema, zaid mtasubl wavamiz wakishaondoka nyie muende kukusanya miili tu ya waliokufa na kuwatibu majeruhi. Hivyo msiilaum UNAMIR kutokufanya chochote kipindi hicho

Nimekuelewa ndugu, na kwa maelezo yako inaonekana unajua mambo mengi yahizi mandate za UN missions.
 
Hivyo msiilaum UNAMIR kutokufanya chochote kipindi hicho
Nyongeza ndogo:

Kwa mujibu wa Head of UNAMIR, Dellaire ni kuwa, Team yake haikuwezeshwa vya kutosha interms of rasilimali watu, fedha na vifa. Pili anasema team yake(including yeye) ni watu ambao hawakuwa na uzoefu wa Missions za Afrika. Tatu kulikuwa na communication delay kati yake na UN, mfano alikuja gundua baadae taarifa na maombi mbalimbali aliyokuwa akiyatuma hayakufikishwa mamlaka husika(deliberate barrier).

Kwa muktadha huo anaamini kuwa kuna mpango maalum ulikuwa nyuma ili mission yao isifanikiwe. Mfn, aliomba Marekani izime mitambo kublock matangazo ya radio Collins(iliyokuwa yakichochezi), Marekani ilikataa kwa hoja kuwa wangepata hasara ya kifedha. So, it was a Mission sent to fail. Mauaji ya Rwanda ni ushahidi wa jinsi gani mifumo ya dunia iko corrupt!
 
Nyongeza ndogo:
Kwa mujibu wa Head of UNAMIR, Dellaire ni kuwa, Team yake haikuwezeshwa vya kutosha interms of rasilimali watu, fedha na vifa. Pili anasema team yake(including yeye) ni watu ambao hawakuwa na uzoefu wa Missions za Afrika. Tatu kulikuwa na communication delay kati yake na UN, mfano alikuja gundua baadae taarifa na maombi mbalimbali aliyokuwa akiyatuma hayakufikishwa mamlaka husika(deliberate barrier). Kwa muktadha huo anaamini kuwa kuna mpango maalum ulikuwa nyuma ili mission yao isifanikiwe. Mfn, aliomba Marekani izime mitambo kublock matangazo ya radio Collins(iliyokuwa yakichochezi), Marekani ilikataa kwa hoja kuwa wangepata hasara ya kifedha. So, it was a Mission sent to fail. Mauaji ya Rwanda ni ushahidi wa jinsi gani mifumo ya dunia iko corrupt!
Asante kwa kujazia nyama kaka
 
Back
Top Bottom