Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Inaendelea.......

Sasa hapa ntaelezea tukio ambalo lilitokea hapa hapa ubalozini tukiwa kazini hatuna hili wala lile tena siku yenyewe j3, ni hivi kwanza naombanizungumzie jambo la kikazi kidogo unajua balozi ni mtu mwenye mambo mengi sanaa ya siri na ya wazi ndo maana nchii nyingi zilizoendelea hupenda kuwapeleka mabalozi ambao ni watu ambao ni mawaziri na wanadiplomasia kweli kweli wengine huwa ni watu wazito jeshini, au wameshawahi kukaa kwenye vitengo vya usalama wa nchii ,sasa ipo hivi unaweza ukawa unafanya kazi ubalozini ukawa unamuona balozi kama mara mbili hivi kwa week au hata mara tatu kwa mwezi si kwamba hayupo anakuwepo ila anakuwa na mambo mengine sanaa.

Sasa huyu mama kama nilivyosema awali ni mwanamama mweupe ila shupavu aise sijawahi ona ntaelezea matukio mawili aliyoyafanya humu hadi nikamvulia kofia , wala si mwongeaji sanaa sasa siku hiyo alikuwepo ofisini tukiwa tunaendelea na majukumu yetu kama kawaida ghafla tukasikia kelele kwa mbali kama kuna watu wamekimbizwa kelele nyingi sanaa kundi kubwa la watu wakawa wanakuja usawa wa ubalozi wetu, ubalozi ulikuwa imeangaliana na ubalozi wa malawi kama sio mozambique kuna Askali alikuwa analinda pale wa nchi yao ila kwetu walikuwa wanalinda walinzi wa kampuni za pale pale kigali ,watu wakawa wazidi kusogea sasa, ubalozi wetu ulikuwa na geti fupi la kama futi sita hivi, sisi tukawa tumejitokeza uwani kuangalia kulikoni ghafla tukaona watu wanaruka kuingia ubalozi wa jirani na akina dada wawili wanaruka kuingia ubalozi wetu na muonekano wao ulikuwa wakitusi mpaka hapo tukaelewa nini kinachoendelea na kwanini wanakimbizwa wauawe si vinginevyo sasa hapo ndo niliposhuhudia ujasiri ambao sijawahi uona kwa mwanamke yeyote toka nizaliwe

Wakati wale watu wanatishia kuingia ubalozini, Balozi akatokea ofisini kwake akawa anawaangalia tu bila kuongea chochote huku kushikilia redio call na ndo mara ya kwanza kumuona balozi ameshikilia redio call ikawa wanaangaliana balozi anawaangalia na wao wanamuangalia sisi wanaume kwa mabinti tumeshakimbia tupo gereje ndogo tunachungulia madirishani ila
Tunachungulia nakusikia kinachoendelea nje, sasa wao wanaimba na kupiga kelele za kutaka balozi awatoe hao mabinti balozi yeye akawa anaongea na redio call ,hebu vuta picha kibaka kakimbilia kwako halafu wananchi wanazunguka nyumba yako wanakwambia wanakupa dakika 4 uwe umewatoa la sivyo wanarushs magrouneti humo sasa hali ilikuwa kama ilivyo kuwa siku hiyo vurugu na makelele yakawa yanaendelea ubalozi mzima tumezungukwa ghafla akaruka njemba moja imejazia kweli kweli na panga lake, ikawa inamfuata balozi wala mama hukukimbia kurudi ndani alisimama hapo hapo, nilichosikia aliapokuwa anaongea kwenye redio call upande wa pili kwamba sasa mmeamua kuichokozaa tanzania kwa makusudi na umewatuma watu wako waje kuwaua watanzania ila tusilaumiane ila alikuwa anaongea kwa kinyarwanda balozi alikuwa anabonga kinyarwanda kama chake vile, ile njemba ikawa inazidi kumfuata ikafanya kama inatanyanyua panga kumkata shingoni, ndo akawa badala ya kujali kinachoendelea pale ndo akawa anazidi kulumbana na alikuwa anaongea nae na alikuwa kwenye redio call, njemba ikashusha panga taratibu ikawa inaisugua panga lake kwenye matiti yake yule mama (balozi) akalivuta lile panga akalitupa nje ya fensi aisee ile njemba ili kasirika ikawa inatukana kwa kinyarwanda vibaya ila kumpiga haimpigi ghafla ilipigwa filimbi yule njemba akarudi nyuma akapanda geti ikarukia njee na wenzake wakawa wanaimba tutarudi tanzania tunaficha ing'otanyi yani Watusi. Mara balozi dakika hiyo hiyo akawasha gari akafunguliwa geri akaondoka alikoelekea hatujui sasa ikawa kimbembe kwa tuliobaki mle na wale akina dada.uongo mbaya wale akina dada walikuwa visu hatariii ila Mbele ya kifo sikukumbuka hilo .

Jioni ikafika kila mtu akaondoka tukawa tumewaacha wale akina dada na mlinzi mle ubalozini mimi nikawahi geto kwangu mapema sikutaka siku hiyo kuzunguka mitaani nikalala bila hata kula, hamu unaotoa wapi ya kula wakati mchana umeponea chupuchupu .asubuhi tuliporudi tulikuta balozi amewachukua na ameondoka nao alipowapeleka hatujui mpaka leo huwa najiuliza aliwapeleke wapi mji ule uliojaa damu za watu.

Naomba swala matokio niishie hapa kwani matokeo madogomadogo mengi yalikuwa mengi sanaa sasa tutaendelea na hatua ya mwanzoni mwa mwaka 1993 ....sasa tunaingia katika hali ya hatari kuwahi kushuhudia katika maisha yangu yote.

Itaendeleaaaaaa.......... Usiku.



Sent using Jamii Forums mobile app
Mambo yanazidi kuwa 🔥🔥
 
Sijui ni umaskini? Kutokujali na kupuuzia kwa serikali?? au tu kutokujua hatari waliyokuwemo raia wa Tanzania pale ubalozini, yaani mimi nafikiri ilitakiwa zishuke helicopter za JWTZ pale ziwachukue raia na kurudi. Safari ya uokoaji kwa usafiri wa malori ilikuwa ni ya hatari kubwa sana, maana kuyasoma tu waliyokuwa wanayapitia siku za mwisho za kuokolewa pale najisikia vibaya sana sijielewielewi nafikiria wahanga wale walikuwa na hali gani, ni jehanum ya duniani.
Umasikini ulikuwa mkubwa Sana mwaka 94
Nakumbuka vitu vizuri vyote vilukuwa Ni vya msaada..mfano visu..vikombe.. blanket..n.k vilukuwa Ni ni vya msaada (tulikuwa tunaita kisu Cha mkimbizi..kikombe Cha mkimbizi..n.k
 
Sehemu kubwa ya story hii ni fiction. Madereva wa trucks wote walikuwa escorted back na diplomats waliondoka bila kudhuriwa iweje yeye mtumishi mwenye hadhi ya diplomat (kumbuka kuwa degree holder wakati huo halikuwa jambo la mchezo mchezo) akimbilie Burundi kwa kuunga unga?
Degree imeandikwa wapi ?
Au unasoma story tofauti na hii
 
Hoteli rwanda ni movie tu ile, tulia ntaelezea mambo ambayo hujawahi kusikia popote pale hii sio hadithi ni ushuhuda wangu mwenyewe .kwa macho yangu mwenyewe.





Sent using Jamii Forums mobile app
Bossless nitafute asee nikurushie kitu na world remit kutoka Norway hapa. Yani leo nimeamua kusoma story/ushuhuda wako mda wote huo naipitaga tu nikaamua asee yani ni bonge. Haki ya nani nakurushia laki moja na nusu.
 
We ndo mpumbavu unashindwa kutofautisha stashahada na shahada halafu unajiona mjanja kumbe empty, ukipigwa ban utakuja na iD nyingine humu kulalamika unaonewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah bossless cheka sana. Eti ukipigwa ban utakuja na ID nyingine kulalamika. Yani kama mimi nikipigwa ban nakujaga na ID nyingine yangu Maghayo kulalamika. Mods wameshanijua wananipigaga ban zote kwa wakati mmoja
 
Back
Top Bottom