Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Bossless nitafute asee nikurushie kitu na world remit kutoka Norway hapa. Yani leo nimeamua kusoma story/ushuhuda wako mda wote huo naipitaga tu nikaamua asee yani ni bonge. Haki ya nani nakurushia laki moja na nusu.
nipo hapa ndugu nicheki in bobo kwa I'd ya bongoman
 
Inaendelea.......

Sasa hapa ntaelezea tukio ambalo lilitokea hapa hapa ubalozini tukiwa kazini hatuna hili wala lile tena siku yenyewe j3, ni hivi kwanza naombanizungumzie jambo la kikazi kidogo unajua balozi ni mtu mwenye mambo mengi sanaa ya siri na ya wazi ndo maana nchii nyingi zilizoendelea hupenda kuwapeleka mabalozi ambao ni watu ambao ni mawaziri na wanadiplomasia kweli kweli wengine huwa ni watu wazito jeshini, au wameshawahi kukaa kwenye vitengo vya usalama wa nchii ,sasa ipo hivi unaweza ukawa unafanya kazi ubalozini ukawa unamuona balozi kama mara mbili hivi kwa week au hata mara tatu kwa mwezi si kwamba hayupo anakuwepo ila anakuwa na mambo mengine sanaa.

Sasa huyu mama kama nilivyosema awali ni mwanamama mweupe ila shupavu aise sijawahi ona ntaelezea matukio mawili aliyoyafanya humu hadi nikamvulia kofia , wala si mwongeaji sanaa sasa siku hiyo alikuwepo ofisini tukiwa tunaendelea na majukumu yetu kama kawaida ghafla tukasikia kelele kwa mbali kama kuna watu wamekimbizwa kelele nyingi sanaa kundi kubwa la watu wakawa wanakuja usawa wa ubalozi wetu, ubalozi ulikuwa imeangaliana na ubalozi wa malawi kama sio mozambique kuna Askali alikuwa analinda pale wa nchi yao ila kwetu walikuwa wanalinda walinzi wa kampuni za pale pale kigali ,watu wakawa wazidi kusogea sasa, ubalozi wetu ulikuwa na geti fupi la kama futi sita hivi, sisi tukawa tumejitokeza uwani kuangalia kulikoni ghafla tukaona watu wanaruka kuingia ubalozi wa jirani na akina dada wawili wanaruka kuingia ubalozi wetu na muonekano wao ulikuwa wakitusi mpaka hapo tukaelewa nini kinachoendelea na kwanini wanakimbizwa wauawe si vinginevyo sasa hapo ndo niliposhuhudia ujasiri ambao sijawahi uona kwa mwanamke yeyote toka nizaliwe

Wakati wale watu wanatishia kuingia ubalozini, Balozi akatokea ofisini kwake akawa anawaangalia tu bila kuongea chochote huku kushikilia redio call na ndo mara ya kwanza kumuona balozi ameshikilia redio call ikawa wanaangaliana balozi anawaangalia na wao wanamuangalia sisi wanaume kwa mabinti tumeshakimbia tupo gereje ndogo tunachungulia madirishani ila
Tunachungulia nakusikia kinachoendelea nje, sasa wao wanaimba na kupiga kelele za kutaka balozi awatoe hao mabinti balozi yeye akawa anaongea na redio call ,hebu vuta picha kibaka kakimbilia kwako halafu wananchi wanazunguka nyumba yako wanakwambia wanakupa dakika 4 uwe umewatoa la sivyo wanarushs magrouneti humo sasa hali ilikuwa kama ilivyo kuwa siku hiyo vurugu na makelele yakawa yanaendelea ubalozi mzima tumezungukwa ghafla akaruka njemba moja imejazia kweli kweli na panga lake, ikawa inamfuata balozi wala mama hukukimbia kurudi ndani alisimama hapo hapo, nilichosikia aliapokuwa anaongea kwenye redio call upande wa pili kwamba sasa mmeamua kuichokozaa tanzania kwa makusudi na umewatuma watu wako waje kuwaua watanzania ila tusilaumiane ila alikuwa anaongea kwa kinyarwanda balozi alikuwa anabonga kinyarwanda kama chake vile, ile njemba ikawa inazidi kumfuata ikafanya kama inatanyanyua panga kumkata shingoni, ndo akawa badala ya kujali kinachoendelea pale ndo akawa anazidi kulumbana na alikuwa anaongea nae na alikuwa kwenye redio call, njemba ikashusha panga taratibu ikawa inaisugua panga lake kwenye matiti yake yule mama (balozi) akalivuta lile panga akalitupa nje ya fensi aisee ile njemba ili kasirika ikawa inatukana kwa kinyarwanda vibaya ila kumpiga haimpigi ghafla ilipigwa filimbi yule njemba akarudi nyuma akapanda geti ikarukia njee na wenzake wakawa wanaimba tutarudi tanzania tunaficha ing'otanyi yani Watusi. Mara balozi dakika hiyo hiyo akawasha gari akafunguliwa geri akaondoka alikoelekea hatujui sasa ikawa kimbembe kwa tuliobaki mle na wale akina dada.uongo mbaya wale akina dada walikuwa visu hatariii ila Mbele ya kifo sikukumbuka hilo .

Jioni ikafika kila mtu akaondoka tukawa tumewaacha wale akina dada na mlinzi mle ubalozini mimi nikawahi geto kwangu mapema sikutaka siku hiyo kuzunguka mitaani nikalala bila hata kula, hamu unaotoa wapi ya kula wakati mchana umeponea chupuchupu .asubuhi tuliporudi tulikuta balozi amewachukua na ameondoka nao alipowapeleka hatujui mpaka leo huwa najiuliza aliwapeleke wapi mji ule uliojaa damu za watu.

Naomba swala matokio niishie hapa kwani matokeo madogomadogo mengi yalikuwa mengi sanaa sasa tutaendelea na hatua ya mwanzoni mwa mwaka 1993 ....sasa tunaingia katika hali ya hatari kuwahi kushuhudia katika maisha yangu yote.

Itaendeleaaaaaa.......... Usiku.

Sent using Jamii Forums mobile app
mimi kipindi hicho nilikuwa nafanya biashara ya dagaa na samaki kitoka visiwani kupitia muganza chato kisha biaramlo rusaunga nyakaura benako zama hizo pakiitwa njia panda ya kwenda karagwe rwanda burund

soko letu lilikuwa kutoka rusumo mpakani mpaka soko lilipokuwa klomita 15 hivi lakini kabla ya kwenda sokoni tulikuwa tukilala njia panda (benako)tukifika siku ya j 3 jioni tukiwa subilia wanayarwanda wavuke hili kesho yake tufanye biasha ya samaki kisha tununue majinzi nakuludizetu

sikuhiyo awakuonekana mpaka usiku tukashangaa kunani kipindi hicho cm hakuna mala magali ya mizigo ya kutoka dar kwenda rwanda burundi yakawa yanazidi kupaki haya vuki matukasikia kupitia sauti ya ujerumani wakisema rais wa rwanda na burundi wapigwa kombora ndani ya ndege wakitokea tz na wote wame kufa

redio ujerumani ikimuoji mtangazaji wa kinyarwanda kabendela shinani akisema sasa watu wanauana sana hasa watusi wanachinjwa sana na wahutu kuanzia mpakani mpaka mpakani mwa rwanda na uganda na drs

takaamua kushuka mpakani kufika kuangalia ng,ambo misululu wa watu unalazimisha kuvuka kuja tanzania polisi walishindwa kuwa zuiya wakaanza kuingia kwa nguvu wengine wana watoto wadogo wengine wamevimba miguu kwa safari ndefu

msululu mwingine wa magali madogo yalio pakia vitanda meza na watoto magali haya yakielekea kahama karagwe mwanza shinyanga runzewe nk

hapo mpakani kuna mto unaitwa rusumo mkubwa sana unaotoka rwanda kumpaka vikitolia kuangalia tukaona maiti zimefungwa kamba na kukatwa vichwa wanawake walio kuwa na mimba walikuwa wametobolewa matumbo yao mto ulikuwa umejaa damu maiti hizo zilienea juu ya maji ziwani nakumbuka

msululu wawatu ulikuwa umetokea kigari rwanda mpaka mpakani rusumo tanzania umbali wa kilomita 150 watu walio ingia tanzania walikuwa wakimbizi 600,000 nakumbuka kama sikosie walijengewa makambi yao pale benako na UN kwa kweli ni habari ndefu sana siwezi simulia yote kuna baadhi ya watu utawasikia wakisema bora vita kuli maisha haya sisi tulio ona vita hiyo kwa macho tunawashangaa sana nimalizie pale benako kambini kwa wakimbizi walikuwepo watoto wasio na mama wala baba tena wadogo miaka 3 5 7 10 wakiomba omba na wakapewa jina la kinyarwanda maibobo

nakumbuka nilienda rwanda mwaka 2015 nikakuta pale kabuga na majerwaa kuna viana wengi wakubwa miaka 20 kuendelea hawa jui ndugu zao wala wazazi wao wakawa wanasema kuwa hawezi kuoa wala kujenga bali hela yao wananua nguo tu viatu na kunywa pilimsi na kuishi kama wafaransa na kuishi wa maisha ya kujiandaa ali moto ukiwaka wasepe wewe ulie waka uzi huu bado uaishi rwanda au tz?
 
Mtoa mada Muongo, Balozi wa Tanzania mwaka 1994 hakuwa mwanamama, alikuwa mwanaume akitwa Salehe Boi Tambwe. Acha story za kutunga.
tunamsebili aje kukanusha au kukubali lakini aje kwa hoja
 
Mtoa post haya masimulizi mazuri sana japo yanafuatiliwa na wenda wazimu wengi, ndo maana comments nyingi ni za kukatishana tamaa (hayo ni matokeo ya mnyukano wa maisha huku mtaani).

Jambo zuri nimeliona ni pale unapotahadharisha uwepo wa vikundi vya usalama visivyo tambulika kisheria, kujipa mamlaka ya kiusalama kuliko hata polisi. Na umetoa mifano kwa Tanzania bila kupepesa, rejea kile kinachoendelea huko Kilimanjaro kwenye mikutano ya Mbowe anapovamiwa na vijana wasio polisi, mauaji ya baadhi ya watanzania ambao hatima ya matukio hayo haijulikani na haifanyiwi kazi yoyote.

Pengine kwa uliyoyashuhudia huko Rwanda, unaanza kuona dalili zake hapa kwetu... Tunayo mengi ya kujifunza kutokana na story hii. Endelea kutupa uhondo, hatubanduki hadi tukutane kwenye biashara yako ya chuma chakavu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wasiujulikana waliokuwa wanampa support JPM kipindi cha utawala wake walikuwa kama Intarahamwe.
Tundu Lissu alipigwa risasi hadharani na hakuna chombo chochote cha polisi kili react.
 
Wakuu hii stori ni nzuri, ila kuna kaujumbe Bossless anatufikishia, maana kila akiandika stori yake kuna mistari huwa anaweka na kuisisitiza mara kwa mara.

Ahsante mzee tunakuelewa, Mungu ibariki Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiki kitu nimekigundua pia.
Dalii mbili za nchi kuanguka
1: vikundi vya kisiasa vya ulinzi.
2: pesa kukosa thamani.
 
Baadae nilikuja gundua kuwa alikuwa anaongea na mkuu wa interahamwe ( jina lake nimelisahau jamaa babe liuaji hatari sijui kama bado lipo hai, kama bado yupo hai hajasakwa na kufikishwa ICC basi haina haja ya kuendelea kuwahukumu wengine) ila jamaa hilo ndo lilikuwa kama Li-mkuu la majeshi kigali nzima huyo ndo top akisema ua umekwisha akisema acha umepona, unajua mabalozi lazima wawe na koneksheni kubwa sanaa wakati mwingine kwa upande wa serikali, waasi (kama wapo) na wapinzani. Mtakufa wote lakini balozi atapona, atalindwa atasindikizwa na kuwekwa sehemu salama. Nyinyi mnahenyeka tuu na vipassport vyenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni kweli tuliona 2020 jinsi Tundu Lissu alivyopona round ya pili kutoroka baada ya uchaguzi kwa msaada wa balozi wa ulaya
 
mimi kipindi hicho nilikuwa nafanya biashara ya dagaa na samaki kitoka visiwani kupitia muganza chato kisha biaramlo rusaunga nyakaura benako zama hizo pakiitwa njia panda ya kwenda karagwe rwanda burund

soko letu lilikuwa kutoka rusumo mpakani mpaka soko lilipokuwa klomita 15 hivi lakini kabla ya kwenda sokoni tulikuwa tukilala njia panda (benako)tukifika siku ya j 3 jioni tukiwa subilia wanayarwanda wavuke hili kesho yake tufanye biasha ya samaki kisha tununue majinzi nakuludizetu

sikuhiyo awakuonekana mpaka usiku tukashangaa kunani kipindi hicho cm hakuna mala magali ya mizigo ya kutoka dar kwenda rwanda burundi yakawa yanazidi kupaki haya vuki matukasikia kupitia sauti ya ujerumani wakisema rais wa rwanda na burundi wapigwa kombora ndani ya ndege wakitokea tz na wote wame kufa

redio ujerumani ikimuoji mtangazaji wa kinyarwanda kabendela shinani akisema sasa watu wanauana sana hasa watusi wanachinjwa sana na wahutu kuanzia mpakani mpaka mpakani mwa rwanda na uganda na drs

takaamua kushuka mpakani kufika kuangalia ng,ambo misululu wa watu unalazimisha kuvuka kuja tanzania polisi walishindwa kuwa zuiya wakaanza kuingia kwa nguvu wengine wana watoto wadogo wengine wamevimba miguu kwa safari ndefu

msululu mwingine wa magali madogo yalio pakia vitanda meza na watoto magali haya yakielekea kahama karagwe mwanza shinyanga runzewe nk

hapo mpakani kuna mto unaitwa rusumo mkubwa sana unaotoka rwanda kumpaka vikitolia kuangalia tukaona maiti zimefungwa kamba na kukatwa vichwa wanawake walio kuwa na mimba walikuwa wametobolewa matumbo yao mto ulikuwa umejaa damu maiti hizo zilienea juu ya maji ziwani nakumbuka

msululu wawatu ulikuwa umetokea kigari rwanda mpaka mpakani rusumo tanzania umbali wa kilomita 150 watu walio ingia tanzania walikuwa wakimbizi 600,000 nakumbuka kama sikosie walijengewa makambi yao pale benako na UN kwa kweli ni habari ndefu sana siwezi simulia yote kuna baadhi ya watu utawasikia wakisema bora vita kuli maisha haya sisi tulio ona vita hiyo kwa macho tunawashangaa sana nimalizie pale benako kambini kwa wakimbizi walikuwepo watoto wasio na mama wala baba tena wadogo miaka 3 5 7 10 wakiomba omba na wakapewa jina la kinyarwanda maibobo

nakumbuka nilienda rwanda mwaka 2015 nikakuta pale kabuga na majerwaa kuna viana wengi wakubwa miaka 20 kuendelea hawa jui ndugu zao wala wazazi wao wakawa wanasema kuwa hawezi kuoa wala kujenga bali hela yao wananua nguo tu viatu na kunywa pilimsi na kuishi kama wafaransa na kuishi wa maisha ya kujiandaa ali moto ukiwaka wasepe wewe ulie waka uzi huu bado uaishi rwanda au tz?
Walikufa watu wengi wasio na hatia
 
Watu wasiujulikana waliokuwa wanampa support JPM kipindi cha utawala wake walikuwa kama Intarahamwe.
Tundu Lissu alipigwa risasi hadharani na hakuna chombo chochote cha polisi kili react.
Chacha Wangwe yeye alifanyiwa vile na kina nani?
 
Kuna askali alikuwa amesimama upande wangu alikuwa ana RPG na bunduki akawa anaweka vizuri rocket Ili alivurumishe kwenye vile vichaka akinipa Ak47 halafu ananionyesha niendelee kufyatua risasi kwa mbali kupitia tundu la bodi ya gari (yani nilivyoishika ile chuma Kama dakika mbili tu nikajikuta yani nimepata ujasiri mkubwa bila kutarajia hapo ndo nilisema mwanzo nami nikawa nimepigana angalau Vita kidogo yule mwanajeshi akavurumisha lile li rocket Polini mle ndo risasi zikawa zimepoa safari ikawa inaendelea kwa kasi .QUOTED

HAPO MWAMBA ULINIFURAHISHA MAANA NAONA NA WEWE HUKUTAKA UACHWE MBALI NA WEWE UKAWA RAMBO🤣🤣 KAMATIA MU EIKEI FOTISEVENI
 
Itoshe ku sema sterling wa hii story ni balozi wa tanzania rwanda huyo mwanamama simba jike ...amefanya matukio yakibabe mno yaani respect maza alikua hodari yaani unyama mwingi
 
Back
Top Bottom