Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Kwanini umechelewa kuleta haya mambo miaka yote hii

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata CIA huwa wanatoa taarifa zao za missions walizofanya hata kama ni za mauaji baada ya miaka zaidi ya kumi baada ya kujiridhisha hizo taarifa hazitasababisha madhara yoyote juu yao au katika jamii watakayoizungumzia.
 
Ndugu.
Humo kichwan umebeba mengi sana kuhusu 94, tupe uhondo huu.
Huenda JF miaka kadhaa ijayo ikawa ni moja ya chanzo cha habar mbali mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mada nzuri sana humu ndani hasa kuhusiana na changamoto za kisiasa, toka 2007 hadi 2012 kulikuwa na mada nzito nzito, sasa walivyokuja hadi kuanzisha chit chat ndio kabisa zimehamia archive hazionekani.
 
Interehamwe in Rwanda versus UVCCM in Tanzania.
Habari zenu wakubwa kwa wadogo.

Kwanza napenda kutoa pole na shughuli za kutwa kwa wale wahangaikaji wote kama mimi ambao kila siku lazima tutoke ili tuweze kujipatia riziki halali kila siku iendayo kwa mungu. Tuseme wote asante mungu.

Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada,mdaa huu wakati naandika huu ushuhuda wangu binafsi ambayo nimeishuhudia kwa macho yangu mawili nchini rwanda wakati wa vita ya kikabila ,wenyewe hupenda kuiita mauji ya halaiki.

Stori inaanza wakati ndo nimemaliza masomo yangu ya uhasibu ngazi ya stashahada mwaka 1989 (sintotaja chuo hicho) nikajaribu kuomba kazi wizara ya mambo ya njee mungu si Athumani nikapata kazi ubalozi lakini nikapaangiwa kituo changu cha kazi kigali-Rwanda, kama sijasahau ubalozi Tanzania ulikuwa maeneo yanaitwa KICHUKIRO ,kwa sasa sijui kama bado upo palepale au vipi sina uhakika.

basi mwezi wa sita baada ya kukamilisha taratibu zote nikaanza safari ya kwenda Rwanda kituo changu cha kazi kipya,ajira mpya na mara ya kwanza kusafiri nje ya Tanzania... Safari ikaanza kwenda kuanza maisha mapya nchi ya watu ,mbali na ndugu jamaa na marafiki nikiwa sijui chochote kuhusu nchi hiyo..

Angalizo. naomba tuvulimiliane ni long stori kidogo na yanaweza jitokeza makosa ya kiundishi na kifasihi.... Ntaelezea mambo mengi sana ya kutisha ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe ambayo hadi leo nimejitahidi kuyasahau lakini imeshindika kabisa.

Safari inaanza pale Mnazi moja nakumbuka enzi zile kulikuwa hakuna mambo ya Booking. unawahi alfajiri na mapema unatafuta basi lako unapanda tu unasubiri safari ianze.

Basi nikiwa na mabegi yangu na shilingi za kitanzania 60 elfu(nilipewa kwa ajili safari na kujikimu na passport ) tu ,naianza safari ya kwenda Kahama, safari ikaanza midaa ya kama saa moja kamili asubuhi (jina la basi lile nimelisahau ila nakumbuka lilikuwa rayland) kipindi hicho barabara ni vumbi tupu changarawe la vumbi hadi linaingia kupitia madirishani, baada ya safari ya uchovu mwingi hatimae saa nane usiku tunaingia singida stand. Mimi mgeni sijui niende uelekeo gani ikumbukwe miaka ile nyumba za wageni zilikuwa za kuhesabu basi ikabidi tushuke pale stand tukawa tunakula mikate na chai na wengine chai na kahawa.

Basi mimi nikarudi kulala kwenye gari,alfajiri na mapema gari likaanza safari tena nakumbuka tulifika stand kuu Kahama kana saa tatu usiku hivi. yani tulitumia kama siku mbili hivi Dar-kahama .leo hii dar - Kahama unatumia siku moja umefika halafu utasikia mtu anasema nchini hii bwana hakuna maendeleo kabisa daa!!!

Tumefika Kahama stand tumepokelewa na wapiga debe enzi hizo wao ndo walikuwa kama mawakala wa magari makubwa anakubebea mzigo hadi kwenye gari unalipa nauli yeye anachukua chake mnaachana hapo hapo hapo ni usiku inabidi kupata gari ya kwenda boda ya Rwanda na Tanzania Rusumo hapo unavuka Mpaka, kuna mto mkubwa unaitwa mto Rusumo unapita kwenye daraja la chuma kama lile lile liloejengwa na wanajeshi pale njia panda Kawe unavuka ng'ambo ukagonga passport ,cha kuchekesha pale kulikuwa hakuna magari ya abiria makubwa.

Magari ya abiria kutoka boda hadi kigali mjini yalikuwa hakuna, ilikuwa inakubidi upande roli la mizigo au abiria mjichange kwa makundi mkodi magari madogo kama tax ila mnabananishwa humo hatari na mizigo juu, kutoka boda hadi kigali ilikuwa kama mwendo wa masaa nane hivi kuingia kigali mjini.
Hatimae baada ya kubadilisha fedha zetu kuwa mafaranga tukapata usafiri wa kutufikisha kigali nakumbuka kundi langu kwenye gari tulilokodi nilipanda na wazaire watupu hivyo kelele zilikuwa nyingi hadi tunaingia kigali wanaimba nakuongea sanaa ubishi mwingi mara mpira mara siasa ili mradi makelele tu.

Saa tisa mchana nikawa tumewasili kigali town enzi hizo sijui lolote kuhusu mji huo zaidi ya address na namba za simu ikabidi niangaze angalau kupata simu lakini wapi,aise kinyarwanda sijui na wao kiswahili kigumu kila nae mujliza ila kupata mawasiliano sikupata msaada ikabidi nikasogolea kwenye stand ya mabus madogo nikamuulize konda kuwa nataka kwenda ubalozi wa Tanzania akaishia kucheka tu niligundua hakunielewa lugha .

Nakumbuka nilikaa stand pale hadi saa kumi na mbili bila bila ikabidi niulizie sehemu pakulala hapo nikaeleweka nikaambiwa lazima upande bus nipelekwe sehemu inaitwa NYAMIRAMBO na nikaambiwa pia kuwa kuna waswahili wengi nikapanda bus hadi nyamirambo nikashushwa tu stand konda akanionyesha kuna hoteli moja ilikuwa imeandikwa nakumbuka inaitwa kama sijasahau ilikuwa inaitwa IMHALA ila nyamirambo ilichanganya kigodo naweza fananisha Magomeni enzi zile.


Nikaenda nikalipia chumba nikaomba kuelekezwa eneo la kula nikaelekezwa, nikaenda nikala halafu nikarudi kujilaza nikipanga namna ya kuingia kesho u abalozi wa Tanzania kuanza majukumu mapya .

Itaendelea...........

Muendelezo bonyea link hizi.

Sehemu ya nne
Sehemu ya tano

Sehemu ya sita
Sehemu ya saba

Sehemu ya nane
Sehemu ya tisa

Sehemu ya kumi
Sehemu ya kumi na moja





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaendelea...........

EeeeMRND ......eeeeee...MRND..eeeee..MRND ....eeeeee...MRnd.. ishaka rya banyarwanda , eeeee...eeee
Eeee MRN ishaka ryubumng'e na mahoro na majambele ya rubanda tweshe turagushigikie ...eeeeMRNd ikomera.×2

Huo hapo ni wimbo wa kinyarwanda wa chama tawala Cha MRND nikaona kabla hatujamalizana na rwanda wote muujue huu wimbo ,Kama nilivyosema mwanzoni kipindi hicho ulikuwa unapigwa redioni masaa 24 kwa siku hakuna kupumzika .nachotaka kusema hapa ni kwamba wimbo huo ulipigwa maksudi ili kuwakaririsha watu waamini kuwa hakuna chama kingine Cha kuwaletea maendeleo zaidi ya chama cha MRND na hakuna mbadala ,huu wimbo ulipigwa redioni Hadi wazungu wakawa wanaujua achilia mbali watoto ukabadilika ukawa Kama wimbo wa taifa yani unaweza kukamatwa na interahamwe ukalazimishwa uimbe huo wimbo Kama ukishimdwa unakula vibao vya kufaa mtu ikalazimika Sasa lazima kila mtu aukariri uujue angalau beti hiyo moja huwa si usahau Hadi Leo (matumiz mabaya ya redio yakawa yameniathiri ) haijalishi we ni mwenyeji au mgeni.imbaaa

Haya Sasa tumalize na Rwanda.......

Tukawa tumelala pale boda usiku asubuhi tukawa tunasogea kwenye kidirisha Ila uongo mbaya sikumbuki sawasawa Kama siku ile nililala usingizi au vipi huwa sina kumbukumbu sawasawa nilistukia tu kumekucha watu Wana nawa nyuso nami nikaenda kunawa uso tukawa foleni kugonga passports zetu kuwahi kupanda maroli upande wa pili ,taratibu zikakamilika

Saa mbili kamili nikawa tumeiacha ardhi ya Rwanda rasmi tunaingia ardhi ya Burundi nikasema ASANTE MUNGU ,safari ikaanza kwenda bujumbura safari ikaanza huku tukiwa na baadhi ya warundi tukawa tunapiga stori kuhusu zile maiti za mtoni usiku Ila wao wakawa wanasema zile maiti zimetoka mbali Sanaa vijiji vya mbali Burundi bado Hali sio mbaya Sanaa japo kulikuwa na tension kubwa rais wao nae alikuwa kwenye ndege iliyomuua rais wa Rwanda Habyarimana. nikajiapiza kuwa kamwe haitotokea Mimi nikanyage ardhi ya Rwanda Tena hadi nakufa hata Kama Vita itaisha nikaambiwa nirudi kazini tena ,hata ningeteuliwa kuwa balozi kamili na ndo ingekuwa mwisho wa hiyo kazi siko hiyo .( Ila miaka ya 2000' ) nilitembelea Kigali tena zaidi ya Mara mbili kibiashara lakini mwenyewe.)

tukaingia Burundi MAROLI yakaenda kupaki eneo la Gitega Kama sijakosea Ila ise nako kulikuwa na kituko ambacho kiliniacha hoi yani niliona magari kadhaa yanapishana mjini yakiwa na matundu ya risasi na polisi hawana time nayo magari ya raia tu nikawa nawaza hapaNapo sipo.tukalala asubuhi safari ikaanza rasmi kuelekea boda ya Tanzania tukavuka boda nikawa ndani ya motherland nikavuta pumzi ndefuu nikasema uuuuaaahhhhhh Asante mungu.
Kuna kitu sitaki kumaliza bila kukisema baada ya kumaliza kuvuka boada ya tanzania Kuna kamwendo kakutoka boda Hadi kuna sehemu madereva huwa wanakula na Kama kupumzika kunaitwa kwa MAMA SHILINGI Sina uhakika Kama bado kupo Kuna mgahawa hivi Sasa pale watu tukawa tunashuka ili kula nikakosa sahani ya kulia ya kuwekea ubwabwa ikabidi yule mama muuzaji anipe kikombe cha chai ili nitumie Kama Sahank na kweli nikachotewa ubwabwa nikawekewa nikawa na kula huwa nikikumbuka nachekaa sanaAaaaa...ubwabwa kwenye kikombe duuuhhh.

Nafikiri Sasa nikawa ndani ya Tanzania ..rasmi ya Rwanda yakawa yameishia hapo.

Sasa kwakuwa niliahidi kuwaletea stori yangu hadi kufika Tanzania,kuacha kazi,kujiingiza katika biashara ya chuma chakavu huko Zambia ,kufungwa jera Ndola n.k Basi niwaombe Kwanza nitengeneze simu yangu kwanza ikiwa imepona Basi ntaiendeleza Kama sehemu ya pili ya maisha yangu kujifunza tu.

Mwisho naomba niwashukuru wote kwa kunifuatilia,kunikumbisha,hata wale mliinidhihaki lakini mkawa mnanifuatilia Kiaina,Asante Sanaa..

Stori hii naamini itakuwa imewavutia wengi sio mbaya kuipeleka kokote Kama sehemu ya kujifunza lakini usisahau kutoa credit kwa Bossless mwenyewe ambae ndo mmiliki wake halali.

Asante kwa viewers na comments za kutosha. USIKU MWEMA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee mbona kazi haswaa
 
Kuna ndugu yangu alinisimulia kisa cha Rwanda alikuwa huko baada tu ya kumaliza form 4 Uganda. Ilibidi atoroshwe kwenye land Rover ya UN cafunukwa na magunia ya mkaa, unaambiwa walikuwa wanashindia kiazi ulaya/mviringo kimoja tu. Kuelekea mpakani ktk kizuizi keep Moja issue ya njemba pia kwake ilijitokeza, huyu nani Mtz, passport wapi taja majina matatu mara Tano bila kukosa spelling ndio akarusiwa.
 
Hizi silaha zilinunuliwa nchini china zililetwa rwanda makontena na makontena kwa ufadhili wa mfanya biashara ambaye alikuwa kiongozi wa interahamwe wakati huo george rutaganda.
No ni Felician Kabuga alikua The don behind.
Silaha zote za kilimo alikua ni yeye anauza.
Mzigo ukaingizwa kukiwa na machete( mapanga)
Rutaganda ye alikabidhiwa tu akasimamie watu waingie shambani kukata miwa.
Ndo balaa lote likaanzia hapo.
 
No ni Felician Kabuga alikua The don behind.
Silaha zote za kilimo alikua ni yeye anauza.
Mzigo ukaingizwa kukiwa na machete( mapanga)
Rutaganda ye alikabidhiwa tu akasimamie watu waingie shambani kukata miwa.
Ndo balaa lote likaanzia hapo.
Ni sahihi kabisa
 
Nadhani ameshahukumiwa,afya yake ya mwili na akili haipo sawa,umri pia umeenda sana
 
Kwa kweli angemtaja tu angalau tumpongeze ukizingatia kuwa huyo balozi alikuwa ni mwanamke na leo ni siku ya wanawake duniani. Huyo mwanamke ana ujasiri wa ajabu kupita hata wanaume wengi wa kutoka pande hizo tuliowazoea kuwaona na kuwasikia kwamba ni wapenda ulojo.
Pitia list ya mabalozi kipindi utaona jina lake..
 
Back
Top Bottom