Sinunui jezi na wala sitaenda uwanjani kuitazama Simba SC msimu huu

Kahindi95

Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
31
Reaction score
100
Wanajamvi, mimi ni shabiki wa simba, naipenda simba.

Lakini kwa yanayoendelea kwakweli nimevunjika moyo, nimeamua sinunui tena jezi wala sitapoteza pesa zangu kwenda tena uwanjani kwa msimu huu wote.

Nimetazama hizi mechi mbili kwakweli nina maswali mengi sana yasiyo na majibu!

1. Hivi simba inashida gani na makocha? Kwamba kila msimu tumekuwa watu wakufukuza makocha tu? Miaka mitano yote hatujawahi kupata kocha bora wa kuifundisha timu yetu? Makocha wote tuliopata wanamatatizo au simba ndio inamatatizo?

2. Kwahiyo tuliacha kumnunua Manzoki tukaenda kununua Mzungu?

3. Mnauhakika huyu Mo anania njema na simba kweli?

4. Kwanini kila mchezaji mzuri tunayemtaka huwa hatumpati? Na tunazidiwa kete hadi na yanga?

Mf: Djuma shabani, Aziz Ki n.k

WACHA NIPUMZIKE KUSHABIKIA HII TIMU NITAFUTE SHUGHULI NYINGINE ZA KUFANYA
 
Misimu yote unayoongelea Simba kacheza Robo Fainali za Africa mara tatu kupitia makocha watatu tofauti.Simba ni timu inayosaka mataji ndiyo maana ikitokea kocha akashindwa kudeliver anatimuliwa lakini kiundani kinachowakuta Simba ni sawa na kile anachokutana nacho Al Ahly akikutana na Simba tena kwa Mkapa.

Take it easy by the way team ikifanya vibafa wewe hupati hasara kama huyo Mo unayedhani anaichezea Simba
 
Watakao kuunga mkono ni wajinga wenzako..! Shabiki wa maana hawezi kususia Timu.

Sasa Dejan Georgijevic ana kosa gani, au Djuma Simba SC wa kazi gani ambayo Kapombe hawezi.

Ungeshauri nini cha kufanya Kiufundi ndo mambo ya maana, usipoenda watakwenda wengine yaani.
 
Wakati Yanga inaandaa timu kwa ajili ya derby nyinyi mkaona mtumie muda huo kuzurura mara Egypt mara Arusha mkaenda kupiga picha na viongozi wa CAF, nadhani sasa akili zimewarudia.

Lete mdhunguuuuu, lete mdhunguuuuu.😀😀🤣🤣
 
Sasa usipoenda wewe uwanjani kuna shida gani?
Uwanja unahitaji mashabiki elf 60 tu kujaa wala hauhitaji wanasimba wote wawe pale wengne mtaangalia kupitia azam Tv
 

Kutokununua jezi au kutokwenda uwanjani huipunguzii kitu Simba. Sisi wenye Simba yetu tutakwenda na kuisapoti timu yetu
 
Acha kutupigia kelele, huna pesa wewe! Wenye pesa tutakwenda uwanjani.

 
Unajua maana ya derby
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…