Sinywi pombe Sinywi soda! Ninywe nini nikiwa bar

Technophilic Pool

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2024
Posts
2,597
Reaction score
3,965
Wakuu Nimeamua kuacha pombe kutokana na matatizo ya kiafya.
Lakini soda pia niliQuite tangu 2020.

Sasa napata changamoto nikienda Bar unakuta siwezi kukaa na kampani ya washikaji maana wenzio wanakunywa we unatoa macho.

Hivi ndo nilikuwa natumia lakini naona siyo kabisa

1. Maji
Aisee haya huwezi kunywa saa moja

2.Grand malta
-Hii inanikera inaleta nzi, mapovu kibao

3.Maji na Energy
Nzuri sana unakuwa na kavibe lakini shida haya maenegy kunywa energy mbili si kiaafya siyo poa naona nakunywa sana…

Hebu nipeni vinywaji vinavyoburudisha bila ya kileo
 
We siubaki nyumbani bar unafata nini
 
Agiza Baltika. Ni bia ya kirusi yenye Zero alcohol.
 
Kunywa baktika au tonic water na ka limao au hill water ile sparkling mineral water
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…