GE2025 Sinzo Khamis Mgeja: Nashukuru kwa chama changu kuniamini, nipo tayari endapo Wajumbe watanipa ridhaa

GE2025 Sinzo Khamis Mgeja: Nashukuru kwa chama changu kuniamini, nipo tayari endapo Wajumbe watanipa ridhaa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
197
Reaction score
233
Sinzo Khamis Mgeja, mtoto wa Mwanasiasa maarufu nchini, Khamis Mgeja ni mmoja wa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walioteuliwa na Kamati Kuu (CC), kuwania Ubunge wa Viti Maalum kupitia (Umoja wa Wanawake (UWT), Kundi la Wazazi Bara.

Mgeja amepata kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga na Mjumbe wa NEC Taifa ambaye kwa sasa yuko nchini India kwa matibabu.
WhatsApp Image 2025-07-30 at 14.40.50_aa274390.jpg
Akizungumza baada ya uteuzi huo, Sinzo ambaye kitaaluma ni Mwalimu, alisema amepokea kwa furaha uamuzi huo kwani chama kimemuamini na yuko tayari kukitumikia kwa moyo na uwezo wake wote endapo wajumbe watampa ridhaa.

Mwalimu Sinzo amesema endapo akipewa ridhaa ya kuchaguliwa na wajumbe ni wakati muafaka wa kushirikiana na wazazi wenzake na chama chake cha CCM kutatua changamoto zinazowakabili wazazi

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na masuala ya uchumi na maendeleo na kuporomoka kwa maadili kwenye baadhi ya jamii hasa vijana.

Kada huyo ambaye ni mjumbe wa Kamati Ndogo ya Elimu na Mazingira wilaya ya Kisarawe, alisema kupitia kauli mbiu ya ‘Kazi na Utu Tunasongambele endapo atafanikiwa kupata nafasi hiyo, atachapa kazi kwa kushirikiana na wenzake kuhakikisha Rais Samia Suluhu Hassan anafikisha malengo ya kuipeleka Tanzania kwenye Dira ya Maendeleo ya miaka 50 ijayo.
WhatsApp Image 2025-07-30 at 14.40.49_8acbd1dc.jpg
“Nina kishushukuru sana chama changu kwa kuniamini na kuniteua kuwa miongoni mwa wagombea wa nafasi za ubunge wa Viti Maalum. Nina imani nikipata ridhaa nitaitendea haki nafasi yangu,” alisema Sinzo.

Kamati Kuu (CC) ya CCM, imekamilisha kazi ya kufanya uteuzi wa awali kwa wagombea ubunge wa majimbo, viti maalum na ujumbe wa baraza la wawakilishi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mafunzo NEC, Amosi Makalla alikiri kuwa uteuzi huo ulikuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya wagombea waliojitokeza kuliko wakati mwingine wowote wa chama hicho.
 
Kumbeeeee ndo mana kizee kinapumulia oksijeni na maplasta mwili mzima kilijitoa ufahamu kikawa kichawa kikongwe kumbe kina jambo lake🤣🤣🤣🤣🤣 nyie nchi hii

Nilitaka kushangaa huyu mzee ana nini jibu nishapata sasa
 
Back
Top Bottom