Sio fair, Wanaoshinikiza Rais Mama Samia afikiri kama Magufuli sio uungwana

Hapana...nafkri kuna baadhi ya mifano sio halisi kwa baadhi ya mazingra, majukumu mama yalikuwa wazi kikatiba...hivyo asingeweza kutaka yake yeye yapitishwe bila baraka za Hayati, hivyo nafkri kipindi ni VP na sasa ni nyakati mbili tofauti.

Naunga hoja mkono kuwa aachwe afanye vyenye anaweza yeye kwakuzingatia vitu vitatu....BUSARA, UTU NA KATIBA[emoji120]
 
Umesema vizuri mkuu. Hoja hii Gwajima kaiweka vizuri zaidi, kwamba pamoja na hili, ni lazima tuwe na vision ya taifa kama ya miaka 50 hivi.
 
Mkuu sidhani hilo kama ni tatizo kwakuwa hayo uliyoainisha hapo ndio hizo approach nilizozungumza hapo juu anazotumia tofauti na Mwendazake.
Ila yanayotekelezwa kwa sasa yatabaki kama awali isipokuwa maono yake ya kuendea jambo lile lile yatakuwa tofauti na Mtangulizi wake..,
Mm nadhani Mama hv sasa anafanya yote hayo kwakuwa bado anawahitaji Wapiga kura kwa Mhula mwingine hivyo lazima acheze na Mdundo wa anaowaongoza, kinyume na hapo Mama halisi tutarajie kumuona kuanzia 2025!
 
Huenda ikawa hivyo...thou wanasiasa walowengi chakula chao ni PUBLIC EMPATHY
 
Shukuran sana mama. Kwa kweli utaratibu wa watu kukulinganisha na kutaka ufanye kama mtu mwingine sio uungwana kabisa.
 
Dah....hili mbona halina mjadala...mama mwenyewe kathibitisha kuwa yeye na JPM ni kitu kimoja 🤭
 
Kuna shule ya busara inayosema kuwa Mama Samia ndio chaguo la Mungu tofauti na wale waliomtangulia. Hakulazimika kutoa rushwa kwa mtu ili awe rais, alishakubaliana na umakamu tangu 2015.

Hana sababu ya kuwa na makundi yaliyoumiza watu ili awe alipo sasa hivi. Namna alivyoupata urais inatakiwa iwe na msukumo wa kutenda haki kwa kila anachokifanya.
 
It won't be possible for those wanting to see it happen.
It's just a beginning; as time goes they are going to be caught in a supprise.
They should realize and accept the fact that that ERA has gone and it's never ever comin' back; we're in a new beginning hence they should learn to dance to the current tuning.
 
Mataga wanataka nini hasa?
 
Mods nisaidie kurekebisha tittle. Afikiri = afikiri

Kwenye utawala wa Magufuli aliingiza watu wengi kwenye utawala kwa njia mbaya hasa kwenye chaguzi zetu. Hilo kundi linaloshinikiza huyo mama afanye kama Magufuli, ni ili atumie mbinu zilezile chafu ambazo wanajua ndio salama ya madaraka yao. Wanajua fika akiacha ushindani halisi nafasi zao zitapotea, na iwapo hilo litatokea ni aibu kwao.
 
Huyu mama alichokosea ni kumbakisha Kasimu Majaliwa

Huyo mama akitaka aachane ni hilo kundi linalomshinikiza afauate ya Magufuli, ni kuruhusu tu ile ripoti ya BoT ya CAG ya Jan-March isomwe, hapo kila tofali litakaa vizuri.
 
Mama alishakosea kwa kusema kuwa yeye na JPM ni kitu kimoja, hivyo msilalamike akitakiwa kujibu tuhuma na madhambi ya JPM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…