Sio kila kiongozi anayekufa anakuwa ameuawa, tuache mazoea


Umeandika kwa summary sana...

Ungeweka timeline ya matukio haswa siku chache kabla ya kukutwa na umauti na siku umauti umemkuta...

Ili watu wajue huo mshtuko wa moyo huenda ulipelekewa na nini?
 
Unakuta mtu huyo kiongozi mwenyewe anamuona tu kwenye TV au kumsikia kwenye RADIO ila inapotokea kifo chake anatoa maelezo utadhani alikuwa ni jirani au mtu wa familia yake πŸ˜€
Na hilo ndio tatizo kubwa kwa baadhi ya waafrika wenzetu. Zamani nilifikiri ni mawazo ya watanzania, lakini baadae nikagundua kuwa ni mawazo ya waafrika wengi hata wale ambao sio watanzania.

Kwa mfano kuna wakongo wanaoamini kuwa hayati mzee Kabila alisetiwa na mwanae Joseph Kabila πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kama alivyosema mdau hapo juu, kuwa afrika kila kifo kinaonekana kimepangwa.
 
Princess Diana
Hata Princess Diana ni sisi waafrika pamoja na magazeti yetu ndo tulikazana kuwa aliuwawa nk. Ila wazungu wenyewe hilo hawakuliwekea maanani ndo maana hadi leo hauwezi kusikia wanafuatilia kuhusu waliohusika na mauaji yake.
 
Umeandika kwa summary sana...

Ungeweka timeline ya matukio haswa siku chache kabla ya kukutwa na umauti na siku umauti umemkuta...

Ili watu wajue huo mshtuko wa moyo huenda ulipelekewa na nini?
Mimi nimeandika kwa kifupi tu mkuu. Ukisema niandike maelezo yao yote nafikiri watu wengi watashindwa kusoma. Maana itakuwa ni gazeti na sio maelezo mkuu.
 
Nonsense
 
Hata Princess Diana ni sisi waafrika pamoja na magazeti yetu ndo tulikazana kuwa aliuwawa nk. Ila wazungu wenyewe hilo hawakuliwekea maanani ndo maana hadi leo hauwezi kusikia wanafuatilia kuhusu waliohusika na mauaji yake.
Naona leo umeamka na Waafrika.
Haya ni matusi mabaya sana.

Mimi nashangaa kwa nini moderators wa JamiiForums wanaezaje kuachia Bandiko kuu kama hili, yaani kichwa bila kiwiliwili.

Kwa kifupi naweza kudadavua hivi.

Unataka kuzima na kufifisha mjadala mzima wa Kifo cha Magufuli. Period. That is a hidden narrative.




...kama mmoja wa mhudhuri hapo juu alivyoelezea, kwamba "Umezunguka mbuyu" . Yaani umeandika porojo jingi kutaka tu, "Kututukana Waafrika" mbali ya hayo kwamba tumpuuze Luhaga mpina, na watu wote ambao wanadhania vifo hivyo ulivyovitaja vilikuwa na mkono ndani yake. Hiyo sio sawa hata.

Kwanini tusidhani vifo vya Wakuu "wenye mamlaka" vina mkono ndani yake? Yaani, ikiwa kwamba watu wana sintofahamu ama woga wa wakuu wengine kuuwawa, tukahoji, tupate ufunuo na kurekebisha,labda,utaratibu wa Kiusalama kwa Viongozi n.k n.k kuna kosa gani? Yani Serikali ambayo inategemewa kutoa kielelezo kimoja na kutoa sintofahamu, ndio kwanza inaleta vielelezo kibao. Kwa nini tusihoji?

Kwanini Serikali iachie hizi "narratives" za uongo zibakie hapa Jukwaani? Yani wao hawaoni kuwa inahatarisha Usalama wa Taifa? Hawaoni kuwa watu watajitungia tu dhana zao?
 
Mkuu mbona umepanic?

Kwa vile Magu amekufa juzi huku ukiwa umeshazaliwa ndomaana unaona kuwa hayo mengine hayana nguvu au maana kujadiliwa. Lakini sisi tuliokuwepo wakati wa vifo hivyo tuliona fukuto la shutuma kali za vifo vyao.

Haya mambo ya kushutumu hayakuanza juzi wala jana. Ndomaana tunaona kama vile imekuwa ni utamaduni.
 
Nikweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…