Wakati mwingine siku chache baada ya kushiriki ngono bila ya kutumia kinga unaweza kuhisi miwasho kwenye uume na hata maumivu kwenye njia ya mkojo. Mara nyingi wanaume huingiwa na wasiwasi wakifikiri kwamba wameambukizwa gonorrhea.
Ukweli wa jambo hili upoje?
- Tunachokijua
- Sio kila muwasho unaotokea kwenye via vya uzazi huashiria uwepo wa maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Kuwashwa kwa uume kunaweza kuchangiwa na mambo yafuatayo;
- Mzio (Allergy) na kondomu, unaweza kutumia kondomu ila ukapata miwasho. Hali hii inaweza kutokea pia hata kwa mwanamke.
- Sababu nyingine huenda kweli ikawa ni magonjwa ya zinaa kama vile klamidia unaosababishwa na bakteria, Kisonono (gonorrhea) na pia malengelenge (warts). Miongoni mwa dalili za uwepo wa magonjwa haya ni maumivu kwenye njia ya mkojo, maumivu kwenye njia ya haja kubwa, miwasho pamoja na kutokwa uchafu kwenye via vya uzazi.
Aidha, ni muhimu kuchukua tahadhari zote za kujilinda pamoja kwenda kupima katika vituo vya afya pindi unapojihisi kuwa na dalili husika.