Sio kila neno ni la kufupisha inaboa sasa!

Hii hali inaboa sana

Japo kuna baadhi ya maneno ni yapo na yanaeleweka ukifupisha mfano (ktk) ni katika au (n.k) ni nakadhalika

Sasa kuna watu wanakera wanafupisha neno *Dogo* wanaandika (Dog) sasa inamaana gani!?, na vile vi fupi zaidi eti K, P
Ni matunda ya kizazi cha BRN
 
Na baraza la kiswahili wapo kimyaaa, utasikia jumamosi wanaongelelea tuuuu eti kiswahili kimepanuka, hawayaoni madudu haya na kuyakemea, Tanzania bwanaa.....
Hawaelewi kua tutaharibu kiswahili chetu tunaweza tengeneza lugha ingine
 
Ukiingia kwenye mitandao ya facebook na insta utakutana na maneno ya aina hiyo mengi sana, wengine wameanza kuyaleta jf pia.
 
Kuna mzee mmja msomi mkubwa tu alinifupishia neno hili (mpm sn) sikuelewa mara moja alimaanisa nini aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…