Sio kwa Ubaya! Ila VunjaBei atapata hasara ya mauzo ya Jezi za Simba kipindi hiki

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kwa namna hali ilivyo tu, ukiangalia unagundua kila kitu kuhusu Simba SC hakiendi sawa tangu miezi ya mwisho ya Barbara kuelekea kuondoka Msimbazi.

Ni kama Mo kasusa timu, wachezaji hawana mori, mashabiki wamechoka siasa basi kila kitu vangarati pale Lunyasi.

Sasa ukija kwenye hili la Jezi ndo kabisaa! Mechi zimebaki chache msimu uishe unaleta jezi mpya halafu inachelewa kuingia sokoni bila sababu za msingi. Kulikuwa na haraka gani ya kutambulisha Jezi wakati bado haijafika?

Bahati nzuri tu ni kwamba Simba hawahusiki na mauzo ila hali ni tete pande zote. Timu inafanya vibaya, mashabiki ambao ndio wanunuzi hawana mzuka kwisha habari hapo.

 
Mimi nafikiri kuna kitu nyuma ya pazia, mfanyabiashara anaweka mzigo ili apate faida, lakini hii stahili ya vunja bei mimi ninaiangalia kwa jicho la 3, ina maana uyu bwana apati hasara? Na kama anapata hasara mbona yuko kimya na wala ashtuki?

Hivi ni kweli uyu bwana ile b.1 ya tenda ya kuuza jezi aliiweka kwenye account ya simba au kuna siri kubwa hapo nyuma ya pazia? Mbona anaonekana kama vile ajali chochote jezi zichelewe au zisichelewe yeye anaona poa tu, na hii ni mara ya pili logistic ya kuleta jezi inakuwa na matatizo kwa upande wake, Nina mashaka makubwa na hili dili la kuuza jezi la vunja bei kuna sehemu aiko sawa.
 
Yupo kimya kivipi wakati akipata hasara anasema?
 
WASIOZIJUA YANGA NA SIMBA WATALIPA UZITO HILI SUALA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…