BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Kwa namna hali ilivyo tu, ukiangalia unagundua kila kitu kuhusu Simba SC hakiendi sawa tangu miezi ya mwisho ya Barbara kuelekea kuondoka Msimbazi.
Ni kama Mo kasusa timu, wachezaji hawana mori, mashabiki wamechoka siasa basi kila kitu vangarati pale Lunyasi.
Sasa ukija kwenye hili la Jezi ndo kabisaa! Mechi zimebaki chache msimu uishe unaleta jezi mpya halafu inachelewa kuingia sokoni bila sababu za msingi. Kulikuwa na haraka gani ya kutambulisha Jezi wakati bado haijafika?
Bahati nzuri tu ni kwamba Simba hawahusiki na mauzo ila hali ni tete pande zote. Timu inafanya vibaya, mashabiki ambao ndio wanunuzi hawana mzuka kwisha habari hapo.