Sio kwamba muziki wetu uko juu bali gharama nafuu za data zilitubeba, Afrika Kusini ndiye mrithi mpya wa nafasi ya Tanzania kushindana na Nigeria

Sio kwamba muziki wetu uko juu bali gharama nafuu za data zilitubeba, Afrika Kusini ndiye mrithi mpya wa nafasi ya Tanzania kushindana na Nigeria

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kwa sasa amapiano inapewa sana promo hapa Bongo na mbaya zaidi hata hao wanaimba amapiano hawaitwi Afrika Kusini ama kutrend vilivyo huko bondeni.

Hapo zamani mpinzani mkuu wa Nigeria alikuwa Tanzania lakini hii ilikuwa kwajili ya silaha yetu ya bei rahisi ya data, kwa sasa mambo yamebadilika kabisa, hakuna video yoyote iliyofikisha views milioni 5 tangu mabando yapande na hazifiki hata videos zilizofikisha views milioni 3 zinahesabika kwa vidole, kiufupi kisu chetu kimekuwa butu.

Kwa hali hii ni dhahiri kabisa nafaai yetu ya kuwa taifa la pili baada ya Nigeria imekwenda na maji, mrithi atakuwa ni Afrika kusini ambae wasanii wetu wameanza kuiga amapiano yake.
 
Nigeria hafanyi mziki kushindana na nchi yoyote iLe afrika kashapita hizO levo iLa tunajaribu kujilinganisha anao tu kiukweLi hatuwawezi labda kwa vyuwazi tu.
 
nigeria hafanyi mziki kushindana na nchi yoyote iLe afrika kashapita hizO levo iLa tunajaribu kujilinganisha anao tu kiukweLi hatuwawezi labda kwa vyuwazi tu
Tanzania kuwa nafasi ya pili kidogo ilifanya tuthaminike na pia hata wasanii wa nigeria hasa wa kati waliweza kuja huku kwetu kutafta ma views za kumwaga.

Lakini pia tuliweza kuwa na heshima yetu tulipokuwa tukiwapokonya baadhi ya tuzo kuja kwetu, sio kitu rahisi hiki.

kwa sasa tunatia aibu sana, huwezi amini tangu october hakuna msanii wa bongo kapata walau views milioni 5, hii kwa wanaoandaa tuzo wataona ni kiashiria cha mziki wa Tz kushuka
 
Huu ni uzi wa ngapi unazungumzia haya mabando yako?
 
Kwani tuliwahi wazidi wa S.A kimziki? Maana wao wapo kwenye ramani kitambo since enzi za channel O
 
Mziki wa kitanzania ni upi huu?maana amapiano asili yake sio hapa,Taifa lililopoteza utamaduni wake(mziki ni moja wapo)ni Taifa mfu,mziki wetu sasa umepoteza kabisa uasili wetu,mziki wa kitanzania uliopendwa na dunia na kuigwa na wengi (kumbuka Tatunane,solo za Tabora jazz,etc etc)mpaka wanamziki nguli wa DRC waliiga(Lagos &Nairobi by night).nchi hii kuna sehemu tulipotea na sasa tumepotea kabisa
 
Back
Top Bottom