Sio kweli kwamba kila tatizo hapa nchini litatatuliwa na Katiba Mpya

Sio kweli kwamba kila tatizo hapa nchini litatatuliwa na Katiba Mpya

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Kumezuka kasumba ya wanasiasa hasa wa upinzani kuwaaminisha wananchi kwamba mambo matatizo mengi tuliyo nayo, yanatokana na katiba mbovu tuliyonayo.

Madai haya yanaweza kuwa na ukweli ila ni kwa kiwango kidogo sana. Ukweli ni kwamba hata katiba bora yenyewe huwa ni matokeo ya msuguano wa hoja nzito miongoni mwa wanajamii husika.

Sehemu kubwa ya madai yanayohusu katiba yaliyopo sasa, yamejengwa kwenye tamaa ya kushika dola ndio maana hayawezi kufua dafu mbele ya walioshika madaraka
 
Ni kweli matatizo mengi ya nchi hii yanatokana na ubovu wa katiba. Ni hatari nchi kuwa na uongozi ambao kuwajibika kwa wananchi wake ni option. Viongozi wakiamua wanazima umeme wakiamua wanawasha,wakiamua wanajenga vituo vya afya au hawajengi.Wakijisikia wanawapa maji au wasiwape.Wakijisikia wanaajiri au hawaajiri.

Yaani ile "INATEGEMEA NIMEAMKAJE". Hata familia kuendeshwa hivi ni hatari sembuse nchi?. Miaka 60 ya Uhuru bado watu wanasafiri umbali mrefu kufuata huduma muhimu kama maji,afya na elimu. Ukitafakari mateso haya yote ni kwa sababu ya kauli mbiu ya "hata tusipowaletea maji mtatufanya nini?".

Ni hatari kikundi cha watu wachache kujimilikisha rasilimali za nchi. Katiba Mpya ni kama Oxygen. Umuhimu wake sio wa kupuuzwa.Wenye kuipenda Tanzania na siyo "Vyama vyao" nadhani wamenielewa.
 
Kumezuka kasumba ya wanasiasa hasa wa upinzani kuwaaminisha wananchi kwamba mambo matatizo mengi tuliyo nayo, yanatokana na katiba mbovu tuliyonayo...
Kwa ufupi, iko ivi ili nchi iendelee mbele kinachoitajika ni mfumo wa uhendeshaji.

Na mfumo huo ndio tunaliita misinfi wa kiutawala ambacho ni KATIBA MAMA.

kwa maana hiyo katiba ndio mwarubaini wa matatizo yote na ndio chanzo ya matatzo tuliyonayo kwa sasa.
 
Kumezuka kasumba ya wanasiasa hasa wa upinzani kuwaaminisha wananchi kwamba mambo matatizo mengi tuliyo nayo, yanatokana na katiba mbovu tuliyonayo...
Ni kweli, Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume halitatuliwa na katiba mpya.
 
Kumezuka kasumba ya wanasiasa hasa wa upinzani kuwaaminisha wananchi kwamba mambo matatizo mengi tuliyo nayo, yanatokana na katiba mbovu tuliyonayo...
Philosopher gani anapumba hivi? Define constitution au hata google basis uache uvivu na uzembe huku ukijipachika vyeo usivyovijua
 
Kumezuka kasumba ya wanasiasa hasa wa upinzani kuwaaminisha wananchi kwamba mambo matatizo mengi tuliyo nayo, yanatokana na katiba mbovu tuliyonayo...
Kwahiyo unaona tuendelee na katiba mbovu iliyopo! Watanzania bwana!
 
Kumezuka kasumba ya wanasiasa hasa wa upinzani kuwaaminisha wananchi kwamba mambo matatizo mengi tuliyo nayo, yanatokana na katiba mbovu tuliyonayo...
Katiba NI suluhisho lakila kitu.Nikweli isiyofichika. Ndugu yangu Philosopher ..jaribu kuangalia Tu Sheria ndogondogo zinaelekeza vipi. Je zinafuatwa? Uchuni WA NCHI na mwananchi moja moja haviwezi kukua Kama Tu katiba yenu nimbovu.

Maana yake nini; tunaowachagua kutuongoza wanatoa maamuzi watakavyo wao sio maelekezo ya katiba..unakumbuka Sheria Kama sio kumi NI zaidi zilipitiahwa Bungeni Kwa masaa matatu Tu.

Huoni nikukosa katiba madhubuti.anyway Muda haunitishi. Ila Katiba nzuri itakayo wadhibiti viongozi NI KILA kitu. Uwe na siku njema.
 
Kumezuka kasumba ya wanasiasa hasa wa upinzani kuwaaminisha wananchi kwamba mambo matatizo mengi tuliyo nayo, yanatokana na katiba mbovu tuliyonayo...

Nyani wale wale agenda zile zile:

IMG_20210909_073543_851.jpg

Kwenye reli hatutoki ng'o!
 
Katiba NI suluhisho lakila kitu.Nikweli isiyofichika. Ndugu yangu Philosopher ..jaribu kuangalia Tu Sheria ndogondogo zinaelekeza vipi. Je zinafuatwa? Uchuni WA NCHI na mwananchi moja moja haviwezi kukua Kama Tu katiba yenu nimbovu...
Mkumbuke watanzania do wale wale hata mkija na katiba mpya! Nchi imeshindwa kuwafanya raia kuwa kwa kutumia raslimali vizuri! Pia mkumbuke hao wanaolilia katiba mpya wengi wao ni wanasiasa wanaojifanya wanajua kila kitu na wachumia tumbo kama akina zito,mbatia na chadema!
 
Kumezuka kasumba ya wanasiasa hasa wa upinzani kuwaaminisha wananchi kwamba mambo matatizo mengi tuliyo nayo, yanatokana na katiba mbovu tuliyonayo...
Kwani Mkuu unajua maana ya Katiba?

Katiba ni kama muongozo(menu) ya namna ya kuitumia simu yako hapo unapoenda kuinunua dukani,sasa wewe kusema siyo kila jambo la nchi litawekwa sawa na katiba basi unafeli sana.

Kenya ni moja ya Nchi zenye Katiba bora kabisa Afrika na unaweza kuona mambo yao yanavyokwenda pia Afrika ya Kusini..
 
Mkumbuke watanzania do wale wale hata mkija na katiba mpya! Nchi imeshindwa kuwafanya raia kuwa kwa kutumia raslimali vizuri! Pia mkumbuke hao wanaolilia katiba mpya wengi wao ni wanasiasa wanaojifanya wanajua kila kitu na wachumia tumbo kama akina zito,mbatia na chadema!
Acheni visingizio vyepesi hivi,iwe wanaoililia ni wanasiasa ama nani ila mwisho wa siku ni jambo zuri na muhimu kwa Taifa letu..

Kwani wanasiasa hao ni raia wa Uzbekstan ama TZ?
 
Tufanye mabadiliko kwenye vitu vyote tuache hilo la tume huru! Tuendelee kubaki madarakani ila katiba iwe inawawajibisha viongozi, mihilimili mikuu ya serikali itenganishwe na tasisi ya urais! Kwakufanya hivyo nchi itasonga mbele na ccm itadumu.
 
Ni kweli matatizo mengi ya nchi hii yanatokana na ubovu wa katiba. Ni hatari nchi kuwa na uongozi ambao kuwajibika kwa wananchi wake ni option. Viongozi wakiamua wanazima umeme wakiamua wanawasha...
Kwa kuongezea: uliona wapi kiongozi anatamka hadharani, tena kwa jeuri kwamba asiyetaka tozo ahamie Burundi as if hii nchi ni mali yake na hakuna wa kumfanya kitu, na bahati mbaya sana Watanzania kwa ujinga wao kama wa huyu mleta mada, wanafikiri wafaidika na hili jambo ni upinzani. Ilifikia mahala rais wa nchi analazimisha kwamba msiponichagulia huyu maji na umeme sileti hapa daah...
 
Yaani acha tu mkuu. Ila ninachompendea Mungu hajawahi kunyamazia manung'uko ya Haki. Ndio maana mimi binafsi kwa kuijua nafasi ambayo Mungu kaniweka "kiroho" kuna wakati huwa nalazimika kujizuia sana "kung'unika" hususani pale ninapoona watu wanakuwa "treated" kama "mbwa koko". Yaani nikinung'unika tu,achilia mbali kuamua kuteta na Mungu aisee surprise yake huwa ni balaa. Kuna watu maishani mwao hawatakuja kunisahau kamwe. Yaani ile mtu unapigwa ngumi halafu anayekupiga humuoni. Uzuri Mungu huwa ananipa kazi ya kuwaonya na kuwatahadharisha kwanza. Wakipuuza kifuatacho mimi nakuwa
"mtazamaji tu". Mungu yupo jamani.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom