SoC02 Sio kweli, ndoa sio tamušŸ˜Ž

SoC02 Sio kweli, ndoa sio tamušŸ˜Ž

Stories of Change - 2022 Competition

brightmind

Member
Joined
Dec 24, 2018
Posts
72
Reaction score
103
Mwalimu T, Rafiki yangu kipenzi wa enzi na tena mhitimu wa ndaki ya Ruaha. Kwa sasa ninafanya naye kazi. Alidumbukia ndoani miaka miwili iliyopita. Bwanaye ni mshehereshaji, mwembamba wa mwili na mkubwa wa maneno. Hachagui neno lipi lianze na lipi lisubiri. Wala hajui hapa aseme lipi na pale asiseme lipi. Ndugu wapenzi wasomaji, niwakumbushe huu si utunzi wa kubuni.

Kama ndoa zingine na mahusiano yaanzavyo, utamu mwingi uliokolea, kuonana kwenye glasi mkiwa mbali na mengine mengi sambamba na hayo, ndivyo pia mwalimu wangu T ilivyokuwa. Ahadi nono kutoka kwa mumewe E kabla na hata siku za awali ndoani. Mwonekano mzuri, uongeaji maridadi, na upigaji pamba makini ulimfanya mwalimu T ajione Julieti kwa Romeo wake.

SIO KWELI, NDOA SIO TAMU. Siku huwa hazigandi, utaficha akili lakini ujinga kamwe hauna stara, tabia husubiri muda wake tu ioneshe rangi halisi. Mwili wa T ulikuwa ukipungua kila uchao, analazimisha tabasamu lakini sura yake kavu kuonesha ule unono aliokuwa nao haupo tena. Hata yale wapendayo wanaume ya kupewa na mama yalikuwa yamesinyaa, nguo zake za zamani zilizomkaa vizuri alianza kuzipeleka kwa fundi kuzipunguza.

SIO KWELI, NDOA SIO TAMU, najua msomaji unajiuliza kama nipo kinyume na ndoa au laa! Lakini nikisema naunga mkono ndoa huo utamu utarudi? Ninafahamu tuna Imani tofauti za dini na ndoa ni taasisi muhimu. Mwalimu T, binti mlokole, mnyenyekevu, aliye adabika na mkomavu wa akili. Kwa T alikuwa mjinga, punguani, takataka na thamani yake ilikuja wakati wa kufanya tendo tu, sio kwa hiari bali wajibu wa T kwani alilipa mahari. ā€œjambo?ā€ nilimwuliza kwani ilikuwa salamu yetu pendwa tukionana. ā€œMungu anasaidiaā€.

SIO KWELI, NDOA SIO TAMU, maji yalipomzidi unga ilibidi anieleze ukweli kwani mimi nilikuwa mwema kwake. ā€œMwalimu M, mume wangu ni pasua kichwa. Yaani hana akili, hana akili kabisa. Kabadilika, kabadilika huyu mwanaume. Zilianza simu za usiku mkuu wa manane, nilikuwa najifanya nimesinzia yeye anaongea na rafiki zake. Dharau zikaingia stashahada akawa harudi usiku baadhi ya siku, baadae dharau zikaingia rasmi shahada na kuanza kuniletea wanawake na kulala nao kitanda nilaliacho nisipokuwepo. Haikutosha shahada ikazaa uzamili na kuanza kunipiga na hatimae akafanya uzamivu matusi mengi, kejeli akiniambia mimi sio kitu, anajuta kunioaā€.

SIO KWELI, NDOA SI TAMU. Sasa haraka turudi akilini, ninaomba tutumie utashi tu na akili ya kawaida, lakini isiwe ya kawaida sana maana itakuwa ya kawaida. Ule uvumilivu katika ndoa huwa unavumilia nini? Pengine ninakuchanganya, haya twende taratibu. Ninamwona, ananivutia, ninasema nae, anakubali. Sasa shangaa jibu lake ā€œUpo tayari kunioa?ā€. Yawezekana haujaelewa vizuri kuoa ni nini. Kuoa ni kumkabidhi mwenzio uhuru wako, na endapo tu utajaribu kuuchukua tayari umeharibu kabisa kama sio kuvunja ndoa.

SIO KWELI, NDOA SI TAMU. Wanandoa tukusanyike hapa haraka, tuongee kama akili tu. Maana akili si mwanamke wala mwanaume. Yaani muda mwenzako anataka utagundua ndoani ni muda ambao wewe hutaki ila kwa sababu upo ndoani lazima kutimiza wajibu. Kuna siku nikawa nasoma sehemu fulani mtandaoni. Swali lilikuwa mwenzako akitaka…..unaweza kumpatia au kumfanyia? Majibu yake ungecheka upasuke bandama. ā€œNDIO, kwa sababu ni mume wangu. NDIO, kwa sababu ni mke wanguā€.

SIO KWELI, NDOA SI TAMU. Wazo ninalo, sijui wangapi mtaniunga mkono. Lengo langu ni mimi na wewe tupate kupata furaha katika ndoa. Sasa usinione mjinga kwa kuwa siwazi kama wewe au kwa kuwa nakuzidi kuwaza na ajabu nikawa nimewaza chini ya kiwango. Potelea mbali hii mitazamo. Ukweli ni kwamba inatakiwa tuoane, NDIO. Nafikiri mshajua sasa mimi ni mfuasi wa ndoa. Lakini kwa kuwa ndoa yang na yako zinakosa amani, upendo na furaha mimi nataka toa mwarobaini. Hadi kufikia hapa, najua umenifuatilia vya kutosha sasa acha nikupe funguo za amani ya ndoa, furaha na mafanikio.

SIO KWELI, NDOA SI TAMU. Siku moja nilicheka sana wakati mwanafalsafa mmoja kijijini kwetu aliposema, ni bora mke na mume wangekuwa wanaishi nyumba mbili tofauti lakini majirani ila wakitakana wanakutana, haha!. Unataka niuliza kama huyo mwanafalsafa anajulikana? Wala usijaribu, maana watu wenye akili nyingi duniani hawaja andikwa popote, wanaojua kuimba sio unaowasikia, waandishi sio hao unaosoma vitabu vyao, hao ni wakati tu umewaruhusu kusimama katika lango. Subiri kwanza msomaji nikumbuke tangu nioe nimefurahia ndoa mara ngapi. Na wewe ukute unakumbuka mzani umelalia kwenye furaha na upendo au BASI.

SIO KWELI, NDOA SI TAMU. Umekufa na utakufa tena, wazazi walikuua, elimu imekuua, na ndoa ndio inayokumalizia kabisa. Ukiona tayari unaanza kubishia hiki nisemacho ujue umekufa hadi sehemu ya kufikiria. Sasa tusitoke nje, kusubiria ushauri au mawazo yangu kuhusu ndoa ni matumizi mabaya ya akili. Ndoa yangu ni kama yako tu, yaani mume na mke, au tuseme mke na mume. Ukitaka usiangamie sehemu yoyote ile tumia akili na moyo wako. Lakini si umeshasikia mambo mabaya hutokea kwa watu wazuri? Wala sikushawishi uwe mbaya ili mambo mazuri yakutokee la hasha! Lakini unaoonaje kama tungeishi kwenye dunia isiyokuwa na ndoa?

SIO KWELI, NDOA SI TAMU. Akili kama yangu ambayo haijaharibiwa naelewa kuwa kuoa ni kukabidhi Maisha na uhuru kwa mwenzako. Usinilazimishe kuoa, sitaki, maana huyu mke niliye nae anatosha. Ndio, usichanganyikiwe, nimeoa lakini nachepuka kwani uhuru katika ndoa yangu haupo, upendo umekauka, hata nilichokipenda sikipendi tena na hata sijui nilikipendea nini, nipo nawajibika tu. Usiniambie sikupenda, nimependa lakini mambo mengine hayawezi kubadilika.

Tunalazimisha tu kuoana, lakini, vipi kama unamwona mtu unampenda mnakuwa na wakati mzuri, upendo ukiisha unaenda zako naye anaenda zake tafuta pengine? Wala hunishawishi eti upendo hauishi, najua unajisemea kama mimi nampenda mwenzi wangu, unajitahidi usimkere, usimwangushe, uwe sawa wakati wote, urudi nyumbani mapema usimwagilie moyo mpaka usiku, eti usisimame na kyuti Lii japokuwa ni mzuri kuliko mke wako au usitoke na Jessy japo anamzidi mumeo kila kitu. Huko ndiko kufa kwenyewe kabla haujafa vizuri. Sawa, njoo na akili peke yake kutoa maoni yako, elimu, dini, tamaduni na mafunzo ulofundishwa kuhusu upendo, Maisha na ndoa weka pembeni. Acha niyeyuke kama

AHSANTENI.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom