May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Ni kama kumejitokeza bidii ya kujaribu kuipa mitazamo hasi karibu kwa kila jambo au mradi ulioasisiwa na Mwendazake.
Kwa mfano mradi kama wa Bwawa la Julius Nyerere, mimi ni kati ya Watu waliokuwa wanapinga kuwekeza matrilioni ya pesa za Walipakodi kwa mradi unaotegemea maji, ambayo tayari uzoefu unaonesha kutetereka kwa miradi kama hiyo iliyotangulia.
Kwa mradi wa kununua Ndege, SGR n.k. huko nilikuwa hamsini hamsini na sikuwa msimamo wowote rasmi. Lakini kwa kuwa miradi hii ilishaanza sioni tena kama kuna haja ya kuitazama kwa upande mmoja tu wa hasi.
Zaidi ni kama kupoteza muda maana tayari ipo inaendelea, kwa nini sasa tusijaribu kuiangalia sasa kwa mitazamo chanya, kwamba kwa kuwa tayari ipo sasa nini kifanyike kuanzia hapa kwenda mbele.
Nini kifanyike Ndege tulizokwishanunua ziwe na manufaa badala ya hasara. Kwanini tusijifunze kwa Wenzetu wa Ethiopia? Kama wao wanaweza kwani sisi ni Viazi sana kwamba hatuwezi kufanya chochote?