Sio mara ya kwanza serikali ya awamu ya 5 kukataa ripoti

Sio mara ya kwanza serikali ya awamu ya 5 kukataa ripoti

Mandesy

Senior Member
Joined
Mar 22, 2018
Posts
115
Reaction score
125
Ombwe la serikali kukataa kuichapisha ripoti ya IMF hivi karibuni sio jambo la kwanza kufanywa na serikali ya awamu ya tano.

Kabla ya IMF, mtakumbuka kwamba serikali ya awamu ya tano iliipa kazi kampuni ya kimataifa ya Moodys kufanya tathmini ya uchumi na uhimilivu wake wa kukopeshwa (Sovereign Credit Rating) mwaka jana.

Baada ya kumaliza kazi hiyo, ambayo serikali ililipa takribani dola million 1 kwa ajili ya kazi hiyo, serikali ilikataa findings za ripoti hiyo.

Pamoja na kupewa alama B, bado hali ya uchumi wetu ilionyesha negative outlook kwa kuwa nchi imekuwa na sera zisizotabirika za uchumi. Hatua hii iliikasirisha serikali na kuizuia kampuni hiyo kuchapisha ripoti hiyo.

Hatua hii ilileta beef kubwa na kuleta uhasama. Nasikia waliwaambia waandike ripoti nzuri isiyo na doa ili kuendeleza propaganda za kuwadanganya watanzania wakati uchumi umeathirika.

Hii iliifanya Tanzania kutokopesheka kwa wakopeshaji wa bei nafuu ndo maana wakakimbilia Credit Suisse pamoja na Uchina ambako hawajali vigezo na wanakukopesha tu ili ukishindwa basi wanajua cha kuchukua.

My Take: Serikali ya awamu ya tano inaendelea kuwa kaidi kwa kujifanya wanajua kila kitu. Kwanza wamekuwa wabishi sana pale ambapo wanapoambiwa kuwa wameharibu uchumi wa nchi kwa sera za ajabu ambazo sio endelevu.

Jambo la pili, naona wapambe wa mkuru wanaendelea kumpotosha kwa kujifanya wao ndio kila kitu na wakamdanganya kwamba yeye ndiye rais msomi kuliko wote duniani kwa PhD ya mwaka 2014 ya kujanjajanja. Yule supervisor wake (jina tunalo) sasa amepandishwa cheo na kupewa egesho serikalini baada ya kusota miaka na miaka chuo kikuu akipambana na supps za wanafunzi (HEWALA BWANA).
 
Ili mtu umalize Masters Degree na Doctorate, ni lazima ENGLISH iwe imelala kichwani kisawasawa, maana kuna REASEARCH THESIS kuandika, kuna kui DEFEND RESEARCH yako na mengine mengi.

Sasa hizo REPORT za CAG pengine watu fulani wakizifungua kurasa wanaona number number tu na makorokocho, yani chenga, hawaelewi chochote, ufafanuzi wanaokuja kuupata wakiona wana JF na MITANDAO ya KIJAMII sambamba na VIONGOZI WA UPINZANI Zitto wanaijadili na kuikosoa kisawasawa ndio wanaelewa mapungufu yaliyopo katika matumizi ya serikali.

CAG anatumia lugha wasioelewa kwenye kuandika REPORT ZAKE, lugha walioizoea watu fulani ni "CCM OYEEEEEEEE PYEEE PYEEEEE".

Sina la kuchangia zaidi kwenye hio point yako ya mwisho. [emoji109][emoji2955][emoji848]
 
Back
Top Bottom