Sio Mchechu tu hata uteuzi wa Peter Ulanga hamna kitu kabisa

Sio Mchechu tu hata uteuzi wa Peter Ulanga hamna kitu kabisa

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Huyu alikuwa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote. Ameutumikia Mfuko kwa takribani miaka kumi lakini baada ya kuondoka tu yeye ndiyo Mfuko ukaanza kujulikana.

Yule dada aliyempokea nafasi Justina Mashiba angalau anaonekana kufanya kazi - kwa muda mfupi anaufanya Mfuko uonekane. Juzi juzi katika kazi zao alionekana hadi akipanda bodaboda kwenda kuzindua mawasiliano huko Tabora uswekeni.

Peter Ulanga hujifanya Mzungu mweusi, Kiingereza kingi lakini anajua kujimanage yeye mwenyewe tu. Ule Mfuko aliufanya kama Kampuni yake. Hakuwa anataka kuajiri kabisa kabisa.

Yeye alikuwa na ile Menejimenti yake ya watu watano basi wanafanya kazi hata za Maofisa wa chini ili wajilipe vizuri.

Hakuna alichokifanya cha kujivunia nchi hii (kama kuna kitu kakifanya leteni ushahidi hapa). Huyu bwana anapelekwa TTCL kwenda kuiua kabisa.

Kwa kifupi SSH akitaka TTCL ipae alitakiwa atafute damu changa kwenye sekta ya mawasiliano - alipaswa kutoa watu wazuri Voda au hata Halotel wabadili Menejimenti yote ya TTCL kwa kuondoa wale wazee na kuingiza damu mpya! Old dogs do not learn and bring new techniques.

Menejimenti mpya iwezeshwe pia. Ukweli Peter Ulanga alishajiishia huko na ndiyo maana yeye mwenyewe aliamua kumkimbia JPM kabla ya kushukiwa kama mwewe.

Kwa hiyo SSH kwa Peter Ulanga na Mchechu hamna kipya ulicholeta hapo. Bora hata Mchechu aliyofanya BOA Bank na hata NHC yanajulikana wazi - mazuri na mabaya yake, huyu Peter Ulanga ni mjanja sana sana, ni mchafu aiyependa kuonekana mchafu.

Subirini miaka miwili mitatu ijayo kama mtaona TTCL inainuka mtarudi hapa kuja kunisoma tena!
 
Huyu alikuwa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote. Ameutumikia Mfuko kwa takribani miaka kumi lakini baada ya kuondoka tu yeye ndiyo Mfuko ukaanza kujulikana...
Hivi kwenye raia millioni 60 hatuna watu wengine? Maana majina ni yaleyale kwa nafasi zilezile. Wengine wanastaafu na kupewa majukumu mengine. Hakuna watu wengine?
 
Hivi kwenye raia millioni 60 hatuna watu wengine? Maana majina ni yaleyale kwa nafasi zilezile. Wengine wanastaafu na kupewa majukumu mengine. Hakuna watu wengine?
Mamlaka ya uteuzi, either imeshauriwa vibaya (na washauri wake) au Washauri wake ,wameamua kumwachie shughuli yake. urais ni taasisi yenye watu wenye weledi, lakini inaonekana hii sasa Ndiyo wanaita "New wine in old bottle".

Mama ni mtu safi awe makini na washauri wake,watakuangushia jumba bovu.
 
Peter Ulanga iletwe CV yake hapa!
 
Mh. Rais amefanya uteuzi wewe unakuja hapa kusema hamna kitu kama nani? Mwandikie Rais hayo maneno yako tuone kama unajua kutoa ushauri basi uwe na tija.

Unabeba hisia zako na dhana za hovyo hovyo unakuja nazo hapa. Acheni Mh. Rais afanye kazi na wale anaoamini watalisaidia hili taifa. Kila msitu una mbweha wake!
 
Nilijua tu Peter utaibukia hapa! Kafanye kazi uniprove mie wrong! Acha kubweka bweka!
 
Back
Top Bottom