winnerian
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 379
- 603
1. HAKI NA USAWA vikubalike na viongozi waliopo. Wajione ni wananchi wa kawaida katika nchi ya Tanzania na sio wamiliki wa nchi ya Tanzania. Watambue uwepo wa watu wenye mawazo mazuri zaidi ya wao hata kama yanapinga mawazo yao. HAKI NA USAWA unazalisha familia yenye upendo na mshikamano pamoja na nguvu, vivyo hivyo kwa Taifa.
2. UPENDO NA MSHIKAMANO Iwe ndio njia kuu ya kutatua tofauti za makundi mbali mbali katika Taifa letu. Meza ya maridhiano madogo madogo isiachwe ikaoza maana ndio tiba ya mengi katika taifa lolote lile. Taifa ni kama nguzo kuu ya nyumba iliyopo aridhini ikiwa maji yatatwama kwa muda mrefu nguzo ile itaoza na kuangusha nyumba nzima.
3. SIFA NZURI NA BUSARA vizingatiwe katika kuwapata viongozi wetu. Uchama, udini, ukanda, urafiki, undugu ukitumika kupata viongozi basi lazima ieleweke wazi tunadidimiza nchi nzima katika shimo la umaskini na vurugu. Watoto wetu lazima waje kuwatumikia wageni katika aridhi yao wenyewe wakati sisi tutakua tumeoza katika makuburi yaliyosakafiwa kwa simenti na tilez kwa juu. Watashindwa kujitetea mbele ya watesi kwasababu tulishindwa kuishi kwa haki na usawa tukiwa haki. Fikiria mara mbili mbili kabla ya kutenda dhuluma (ccm)
4. SHERIA NA KANUNI iwe ndio kiongozi mkuu wa kila mmoja wetu. Hisia zetu pamoja madaha yetu (ego) inafika mahali vyote hivi vinakuwa ni kwa mihemko mibaya na baada ya kuhemka tunajutia. Hivyo kama SHERIA NA KANUNI ikifuatwa na kila mmoja wetu kuanzia mwanchi kitongojini hadi raisi wa nchi basi ni rahisi sana kupata maendeleo ya kweli.
5. KATIBA MPYA NI MUHIMU. Katiba mpya itakayotoa dira ya Taifa kwa miaka hata 100 ijayo ni lazima ikaundwa. Na hili ili liweze kutimia kwa usahihi lazima mambo manne yaliyotajwa hapo juu yatimie kwanza. Tumeshuhudia namna ambavyo viongozi wetu kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi wemeendelea kutokuheshimu katiba ya nchi. Ni huzuni kwa wachache wanoelewa maana ya kuwa na kwenu na kuona baba hakiharibu kila mali na kila kilichomo ndani bila kujali hatima ya watoto wake.
6. VIONGOZI PIA WATAMBUA KUNA SIKU WATAKUFA NA KUACHA ENZI ZAO WALIZO NAZO SASA. BUSARA NA HEKIMA ITAWALE MIOYO YAO NA HISIA ZAO. CHUKI BINAFSI KWA KIONGOZI ISIPATE NAFASI.
Wapo ambao ni wenzetu katika miili lakini sio wenzetu katika mioyo yao na roho zao, wakiwa wanatafuta kuwa miungu watu hawatakumbuka HAKI wala USAWA. Chuki na ubaguzi zinawatala hata ukitazama sura zao utaona namna ambavyo zimejawa na simanzi pamoja na huzunil, uchungu na visasi maana moyon hawana furaha kwa yale maovu wanayoyatenda na kuyafanya.
KAMA NINGELIKUWA RAISI LEO NINGALIHAKIKISHA MFUMO WA HAKI NA USAWA UPO IMARA KULIKO BENKI KUU YA TANZANIA
IPO SIKU TUTAKUFA NA KUOZA NA MALI HIZI ZOTE TUNAZOWEKA SASA ZITAOZA PIA ILA HAKI NA USAWA ITADUMU MILELE .