Sio siri tena! Tumia mbinu hizi tatu kuua ushindani unaokabili biashara yako

Sio siri tena! Tumia mbinu hizi tatu kuua ushindani unaokabili biashara yako

Joined
Aug 28, 2024
Posts
9
Reaction score
22
Kuna njia kuu tatu tu za kuua ushindani kwenye biashara yako

Moja kuwa bidhaa ya bei nafuu kuliko zote sokoni ....
Mpaka sasa sijui ni mbinu gani bora ya kupambana na bei sokoni
Mtu akikushinda kwenye bei ni majanga ...

Pili, Ni kuwa na uwezo wa kufikisha bidhaa au huduma kwa wateja ndani ya muda mfupi
Bidhaa inayofika kwa wakati kwa wateja inauzika zaidi

Tatu ni kuwa na bidhaa bora kuliko zote sokoni.
Ubora wa bidhaa au huduma utakunufaisha sana sokoni ....

Ukiweza kuchanganya vitu vyote vitatu kwa pamoja ...

Utakuwa haukamatiki sokoni ....

1. Bei nzuri

2. Huduma kwa wakati

3. Bidhaa bora

Hata kama biashara yako ni ndogo namna gani,
Jitahidi sana uifanye kama ni big brand ( biashara kubwa )
Ni kazi ngumu lakini inawezekana sana..

#payless +255 654 208 515
 
Ukishakuwa na bidhaa ya bei ndogo pia ubora wake uwa ni mdogo..

Wewe ungewaambia tu wahakikishe bidhaa zao wanapata hata kwa magendo basi lazima utoboe.
Unauza bei ile ile ila faida kubwa kutokana na kukwepa kodi
 
Yote hayo kama huna kauli nzuri itakuwa biashara haramu.
 
Ukishakuwa na bidhaa ya bei ndogo pia ubora wake uwa ni mdogo..

Wewe ungewaambia tu wahakikishe bidhaa zao wanapata hata kwa magendo basi lazima utoboe.
Hapo tuko pamoja
Biashara za Africa ujanja mwingi na mpaka kuna damu pia
Kampuni ina supply bidhaa halafu dereva anakuambia kuna mali hapa nauza bei ya kutupa zimepigwa kiwandani, unanunua
Sasa hata ukiweka bei ya chini sana kuliko wengine utatoboa kiwizi wizi

Wengine wanatoka waliko na kwenda kuvunja au kuiba huko akirudi ni mtu mwema kama sio yeye
Anampa mke wake dukani vocha za mamilioni auze baada ya kutakatisha alichoiba
Huwezi kushindana na watu kama hao
Biashara za bila uaminifu hizo
Nimefanya sana biashara ila siri ni kuwa na biashara zilizopo sokoni chache kuliko zingine utaendelea sana

Tafuta biashara zisizo na ushindani mkubwa hapo ulipo
Yaani mpo wachache
 
Usitamami mali ya mtu kuna watu wakiulizwa chimbuko la mali zao hawawezi kusema maana zimejaa dhulma na damu
 
Back
Top Bottom