Sio utamaduni mzuri kushabikia utajiri na matajiri bila kujali wameupata vipi

Sio utamaduni mzuri kushabikia utajiri na matajiri bila kujali wameupata vipi

Cordy bnei shirk

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2017
Posts
331
Reaction score
252
Utandawazi tunauvulia nguo na kuuoga kisawasawa bila kuzingatia misingi. Leo hii wananchi wengi wanapendezwa,kuhamasishwa,kutamani utajiri pamoja na matajiri hasa kwenye mali za kujionesha na kuona kila mtu anastahili kufika hapo

Andiko langu limetokana na kuona video ya tajiri flani hivi mtu mzima ambae kamualika influencer aje kwake akampa zawadi na pesa pia akamuonesha collection yake ya magari mapyaa ya kifahari kwenye gereji yake inayowakawaka.

Kikawaida na kiungwana mtu kama yule na historia yake angekausha tu na magari yake kimya kimya bila kuwakumbusha watu msala wake. Ila sababu watanzania hatupo hadhiri tunamsifia na kumuona role model na kutamani pale alipo huku yeye bila aibu akiwa proud kusema kua ni “ Kweli alikua fundi viatu na sasa amefika hapo”

Mi nimekaa hapa na pombe zangu nauliza kwanini mtu mzima tajiri kama yule atafute influencer ajitangaze uwepo wake?kitu gani amekosa mpaka atamani spotlight sasa hivi? Kwanini influencer akaelezea historia yake kwa ufupi?

Je inaweza ikawa ana hofu na jambo flani hivi ila anatafuta kuonekana ili apate mtetezi? Washkaji zake wamezeeka na kufa hivo yuko mpweke anataka validation kwa vijana wa kisasa na yeye aonekane? Au ni effect tu ya social media ambayo kila mtu inamkuta?

Anyway tutafute pesa ila ni kitu kibaya kuwapa promo nzuri matajiri janja janja.

Nchi haijengwi na janja janja tupende na kusupport na kutamani matajiri wote ambao wana leta value endelevu kwenye jamii na kukemea kwa nguvu zite matajiri wanaofaidika na udhaifu wa mfumo wetu.
 
Back
Top Bottom