Sio utamaduni wa wanaume wa Kitanzania/Africa

NGULI

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2008
Posts
4,801
Reaction score
643
1. Kumfungulia mwanamke garia apandapo au kushuka na kumfunga mkanda kabla ya gari
kuondoka

2. Kumshika mkono kwenye hadhara wakati wa kutembea e.g evening walk au kwenye
ocassion kubwa inatokeaga siku ya harusi tu.

3. Kumsifia pale panopostahili e.g nguo imekupendeza kweli....u look excellent on those
clothes. U had wonderful presentation I rly like it.....

4. Kumpigia simu muda wa mchana kumtakia mlo mwema na kujua siku yake inakwendaje.
Au kumwachia ki-note asubuhi kwenye fridge au nyuma ya mlango chenye ujumbe wa
mapenzi e.g u luk so peaceful, beautiful and at peace when u sleep

5. Kumpa au kumnunulia maua katika vipindi tofauti
 
Wanawake nao wanapenda kufanyiwa vitu hivyo ulivyovitaja. Si vibaya tukifanya hivyo kwani kuna mambo mengi si utamaduni wetu lakini tunafanya! Sioni ubaya wowote ukimfanyia mpenzi/mke wako mambo hayo!
 
Siyo utamaduni wa kiafrika kweli lakini wanaume wetu hufanya sana tu hayo uliyoorodhesha maana dunia ni kijiji na kuna mwingiliano wa tamaduni.
 
sio utamaduni wao kwa hiyo unatuambia tusitarajie na tukifanyiwa ni bonus tu au?
 
Hakuna kitu kinachoitwa utamaduni wa Mwafrika au Mtanzania.
 
Yaani kuna majamaa wengine kukushika hawataki, ukiwashika wao mbele za watu tena kwa mapenzi ya dhati, utasikia noma niachie, tutashikana ndani...jamani kama upo kwenye mapenzi kwanini uogope mamcho ya watu??
 
Watu waache unafiki.Kama una mapenzi na mtu wako, unaogopa nini kuonyesha au unasubiri wengine wamuonyeshe huyo mwandani wako halafu uje ulalamike?
 


Natamani ningekua nafanyiwa hayo ningekua mwenye furaha sana..
 
Yaah right.........
What is your suggestion anyway

Tuwafanyie hivyo vitu inapendeza kweli mimi nafanya mazee nilitaka ile heading iwe swali nikakosea nime edit nikashindwa
 
Ni njema ktk kuimarisha mapenzi na mahusiano kwa ujumla.
 
Yaani kuna majamaa wengine kukushika hawataki, ukiwashika wao mbele za watu tena kwa mapenzi ya dhati, utasikia noma niachie, tutashikana ndani...jamani kama upo kwenye mapenzi kwanini uogope mamcho ya watu??

Hata mie kusema ukweli huwa naona noma...ukiniuliza sababu sina! Labda pengine ni malezi! katika kukua kwangu sikuwahi kumuona baba akimbusu mama mbele yangu/yetu....lakini I know wanapendana na hata sasa katika uzee wao wapo pamoja! Hata kwa majirani pia sikuwahi kuliona hili!

Lakini katika vitendo hivyo pia kunaweza kuwa na tatizo la kisaikolojia hasa yanapofanyika mbele za watu tu na mkiwa wenyewe ndani hayafanyiki!
 
From what I have seen, huo sio utamaduni wa mwanaume regardless of race, nationality and or age. That is why wanaofanya hivyo huwa wana-appear a bit different katika kila jamii. And did I say it ??????? , they even show it on TV which tells me it is somehow strange..............
 
Yaani kuna majamaa wengine kukushika hawataki, ukiwashika wao mbele za watu tena kwa mapenzi ya dhati, utasikia noma niachie, tutashikana ndani...jamani kama upo kwenye mapenzi kwanini uogope mamcho ya watu??
Wengine wanafika mbali kabisa wanaona soo hata kuongozana.
 
lazima tukubali kuwa sio hulka yetu kwa sisi watanzania kuyafanya hayo mbele ya watu!lakini isitoshe siwezi kuwa conviced kuwa ukiyafanya hayo tu basi ndio unadhihirisha mapenzi mazuri na matamu kwa mwenzio.Tukumbuke kuwa hata hao watanzania wenzetu wanaofanya hayo wasifanye kwa shinikizo la kuonekana tu na kumbe si kutoka moyoni!tusiwe artificial na kuendekeza mambo ya kuiga!be natural and real na itapendeza tu!
 
tuepuke kuiga sana mambo na asili ambazo si za kwetu!cha kuiga always hakinogi, always be natural!kuna haja gani ya kuyafanya hayo huku moyoni nikiwa naumia na kujuta?????
 
Yaani kuna majamaa wengine kukushika hawataki, ukiwashika wao mbele za watu tena kwa mapenzi ya dhati, utasikia noma niachie, tutashikana ndani...jamani kama upo kwenye mapenzi kwanini uogope mamcho ya watu??

Hahahaha anaogopa watu wakijua kesho atashindwa kumega binti mwingine utambania ridhiki...
 
Wengine wanafika mbali kabisa wanaona soo hata kuongozana.

Hahahahahaha kweli mkuu anamtanguliza wife/demu mbele yeye anakuja nyuma anaangalia watu wanavyo mthaminisha
 
kuna wengine hawana mawasiliano kabisa utakuta mme karudi kutoka job anakuta kikaratasi kimeandikwa unga, sukari, majani ya chai na mafuta ya kula yameisha halafu nae anachukua kalamu anajibu sina hela no kuongea. Ila tubadilike kidogo tuzungumze yanayotuhusu na wenzi wetu

kuna familia utakuta wanaenda kanisa moja ila kila mtu anatoka kivyake na hata kurudi hivyo hivyo utadhani wamelazimishwa kukaa pamoja

Mbona kwenye uchumba hayo yote yaliyoorodheshwa yanafanyika ila kwenye ndoa tunasema sio tamaduni zetu tubadilike (pamoja na mie) dunia sasa ni utandawazi na ni kijiji tuige mazuri kutoka kwa wenzetu maana kila siku tunashindia mitamthilia lakini hata atuigi yale mazuri kwenye mapenzi
 
Mie mwenyewe kusema kweli nilikuwa naona kama vile siko Confortable mzee kunipitishia mkono kiunoni au kushikana mikono na hata kunikiss mbele za watu najitahidi kuonyesha kama am ok kumbe moyoni lol :biggrin1:..not sure kama ni ushamba ,najua yote hii inachangiwa na malezi toka mwanzo katika familia zetu:gossip:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…