Sio utamaduni wa wanaume wa Kitanzania/Africa

kweli kabisa kibongo bongo ni ngumu sana tena sanaaaaaaaaa halafu hizi ndoa zetu mara umefumwa na msg ya nyumba ndogo mara mmechuniana mara mmegombana ndio baadae mtu uje kumfumgulia mlango wa gari halafu na wake zetu hawa utakuta mnataka kwenda safari pamoja anajiandaa saa nzima wewe unasubiri tu matokeo yake mnachelewa unakasirika hata kukumbuka kumwambia kapendeza au kufungua mlango wa gari unasahau

mie kuna siku nilimfungulia mlango wa gari tulikuwa tunatoka kwenye sherehe ya ofisini ili niwachekeshe staff wenzangu nakumbuka siku ile wife alisema "leo jua litatoka usiku"
 

U made my day bra ha ha ha ha
 
Hivi kwa nini kumfungulia mke wako mlango wa gari? Hii ndio njia yetu ya kuonyesha mapenzi?? :kiss: Au ndo kwa hisani ya watu wa marekani??
 

yaani Funzadume nimecheka mpaka machozi....yaani wewe una vituko sana!
 
Hivi kwa nini kumfungulia mke wako mlango wa gari? Hii ndio njia yetu ya kuonyesha mapenzi?? :kiss: Au ndo kwa hisani ya watu wa marekani??

jamani mila/desturi zetu hizi ni ngumu sana, mie mr kuna wakati huwa anapika na amefundishwa kazi za nyumbani kwenye malezi yake, kuna cku mama yake alikuja kututembelea kuamka asubuhi akakuta mr anaandaa breakfast mie naendelea na shughuli zngine....yalikuja maneno hapo kwamba namtawala mwanae lakini hapo hapo huyo mwanae kwao alikuwa anafanya kila kazi ya ndani kumsaidia mamake na yeye ndio alimfunza hivyo, imekuja kaoa anataka mambo yote aweke nyuma.....
 
Katika mahusiano, hatufanyi vitu kwa mujibu wa tamaduni zetu. Tunafanya jambo lolote linalotufurahisha na linalowafurahisha wenzi wetu. Kama ikitokea lipo katika tamaduni basi ni good coincidence, ila lengo sio ku-practice tamaduni, ni kufanya yale yanayoburudisha nafsi zetu.
 
U made my day bra ha ha ha ha



mie alikuwa amshanizosha hiyo ya kunifungulia mlango, lakini inapotokea tupo na mama yake utaona hafanyi hiko kitendo, kuna cku tupo na mama yake, wanaagana mie nipo upande wa pili nasubiri kuja kufunguliwa kama kawaida nashangaa mtu ameshawasha gari naulizwa mbona huingii?..nika note tukiwa na mama hawezi nifanyia hivyo anajua mwenyewe sababu, nilimpiga marufuku kuanzia hiyo cku alivyoniacha naduwaa tu.
 

:smile-big:au mlango wa gari ni mbovu lazima ufunguliwe kwa nje
 
To be frank i love those stuffs, but saa ngapi tunafanya? hata tukifanya ujue hakuna anayetuona ni sisi tulio ndani ya nyumba. Ila nawashauri kila mtu aongee kuhusu mapenzi yake anayotaka afanyiewe na mwenzie ili ubadilike kutoka kwenye style hii na kurudi kweny style nyingine. Nina imani hakuna linaloshindikana
 

noted. . ila katika dunia hii ya utandawazi...yale mema yanayoweza kutumika kama njia ya kuonesha upendo kwa mwenzio yatumike.. Mbona zamani mke'mtarajiwa' alikuwa anaenda kutembelea wakwe na kusaidia kazi kama kupika na kuchota maji...!! ni utamaduni wa wanawake wa kidhungu?
 

Teh teh teh!
 
loh.....anifungulie mlango wa gari?
Nitamkimbiza...
Sijazoea hayo mie
 
Wakati mamchumbia yote hayo nilikuwa namfanyia, sasa akafika hatua akawa anakataa kushikwa mkono, ukimletea zawadi ya maua hata hasante hakuna, ukija na kiroba cha mchele ndo anafurahi, basi taratibu nikaacha. Tunalisongesha kimtindo.
 
Hahahaha anaogopa watu wakijua kesho atashindwa kumega binti mwingine utambania ridhiki...


enheee hilo nalo neno, wakati fulani nilipotembelea kwa mara ya kwanza nchi moja ya latin America na kuona jinsi wapenzi wanavyo kuwa wakiwa pamoja nilidhani naangalia romantic movie, yaani wala hupati shida kuelewa kuwa hawa ni wapendanao ni full kushikana mikono, kisses na ma-care ya kutosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…