Sio uungwana kumchezesha mchezaji aliyefiwa na mzazi wake

Sio uungwana kumchezesha mchezaji aliyefiwa na mzazi wake

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Beki wa kushoto wa klabu ya Yanga, Chadrack Boka (25) raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amefiwa na baba yake mzazi, kifo kilichotokea Januari 11, 2025, nyumbani kwao Kinshasa DR Congo.

Uongozi wa Klabu ya Yanga umetoa pole kwa nyota huyo wa zamani wa FC Saint loi Lupopo ya DR Congo huku ukiungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na unawataka wanafamilia wote kuwa na subira.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina
 
Attachments

  • 1736772636193.png
    1736772636193.png
    123.1 KB · Views: 4
Boka aliomba mwenyewe kucheza ili kumpa heshima ya kweli Mzee wake

Siyo Boko wa kwanza Lampard, Ballotel Inzagh n. K walipata kucheza wakiwa na misiba ya wapendwa wao
Kafara
 
Mchezaji mwenyewe alionekana kabisa hayuko mchezoni halafu kuna mtu anasema eti aliulizwa kama anaweza kucheza. Tena uto wengi sana walimtukana wakati mechi inaendelea, hayo matusi yake sijui sasa apewe nani.
 
hajaulizwa bali yeye mwenyewe ndio aliomba kucheza
 
Boka aliomba mwenyewe kucheza ili kumpa heshima ya kweli Mzee wake

Siyo Boko wa kwanza Lampard, Ballotel Inzagh n. K walipata kucheza wakiwa na misiba ya wapendwa wao
Watu kama hao tofauti na Simba na Yanga hakuna wanachojua.
 
Hivi kumbe mchezaji anaweza kumuomba kocha awemo kikosini? Basi Musonda anajichelewesha, Ile nafasi ya Dube inabidi aiombe kila mechi
Kwani first eleven ya kila timu si inajulikana mkuu, Yanga kwa mfano Boka au Yao wapo fit utawaachaje nje ya ya kikoso
 
Back
Top Bottom