Sio vita vyetu' - Mkataba wa Trump wa silaha za Nato kwa Ukraine waibua hasira za MAGA

Sio vita vyetu' - Mkataba wa Trump wa silaha za Nato kwa Ukraine waibua hasira za MAGA

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Baadhi ya wanachama wa kihafidhina wa vuguvugu la Donald Trump la "Make America Great Again" wamejibu kwa hasira mipango ya rais ya kuiuzia Nato silaha, wakisema ni usaliti wa ahadi yake ya kukomesha ushiriki wa Marekani katika vita vya kigeni.

Siku ya Jumatatu, Trump alisema atatuma silaha kwa Ukraine kupitia Nato, huku pia akitishia Urusi kwa kutoza ushuru zaidi ikiwa makubaliano ya kumaliza vita hayatafikiwa ndani ya siku 50.

Wabunge wa chama cha Republican, Marjorie Taylor Greene, mshirika mkuu wa Trump, na mwanamikakati wa zamani wa Trump Steve Bannon ni miongoni mwa waliokosoa uamuzi huo, huku Bannon akiwaambia wasikilizaji wake wa podikasti kwamba Ukraine ni "vita vya Ulaya".

Ikulu ya White House imesisitiza kuwa Ulaya itagharamia silaha hizo zinazotengenezwa na Marekani.

Katika mahojiano na gazeti la New York Times, Greene - mwanachama aliyejitenga na Bunge kutoka Georgia ambaye amekuwa mmoja wa wafuasi waaminifu zaidi wa Trump huko Capitol Hill - alisema hatua hiyo inakinzana na kile alichowaahidi wapiga kura kwenye kampeni.

"Siyo Ukraine pekee; yote ni vita vya nje kwa ujumla na misaada mingi kutoka nje," alisema. "Hili ndilo tulilofanya kampeni. Hili ndilo nililoahidi pia kwa wilaya yangu. Hili ndilo ambalo kila mtu alilipigia kura. Na ninaamini kwamba tunapaswa kudumisha barabara hiyo
 
Back
Top Bottom