Sioi Solomon awaburuza Mahakamani, ICBC Standard Bank, Stanbic Bank Tanzania Ltd, Waziri wa Fedha na Mwanasheria Mkuu

Kesi za namna hii zitaligharimu Taifa pesa nyingi sana, kila mtu aliebambikiwa kesi akiamua kudai Fidia ni harara kubwa sana kwa Jamhuri, hakuna sababu ya kuwaweka watu ndani tena kwa miaka mingi kama hakuna evidence za makosa
Nina uhakika hujasoma na hujui kilichoko kwenye hizo documts ni kitu gani
 
Aliyeidhinisha mkopo (watumishi wa serikali) ndiyo walitakiwa washitakiwe halafu kina Sioi wawe mashahidi ikibidi.
Sasa mambo yalifanywa kinyume kwa sababu za kisiasa.
 
Haki itendeke dhuruma na ushetani vimepitwa na wakati. Mahakama ya mafisadi tumehukumu wangapi wako jela.
 
Hivi unajua kinachodaiwa au unakurupuka? Hizo pesa zililipwa kwa Serikali ya Uingereza ila Sioi anasema ni haki ya Serikali ya Tanzania hivyo zilipwe kwenye serikali ya Tanzania na siyo yeye anaidai Serikali ya Tanzania!
 
Je inahusiana na ile ya kuwekwa ndani miaka kadhaa bila uchunguzi kukamilika, kisha DPP anatamka "serikali haina nia ya kuendelea na kesi". Watuhumiwa wanaachiwa.
Kizungu hasa kinapokuwa cha kisheria naona kinaleta shida! 80% ya great thinkers wameingia chaka!
 
Kesi za namna hii zitaligharimu Taifa pesa nyingi sana, kila mtu aliebambikiwa kesi akiamua kudai Fidia ni harara kubwa sana kwa Jamhuri, hakuna sababu ya kuwaweka watu ndani tena kwa miaka mingi kama hakuna evidence za makosa
Ukweli mtupu.....
 
hii lugha ya malkia itasababisha UVCCM washindwe kutukana vizuri.
 
Badala ya kumpongeza JP angalau mawaziri wengine walirudisha pesa,Ruge na huyu mhindi walitiwa nguvuni,unamulaumu?

Vipi mzee wa Msoga Kwanza Jambo lilitokea kipindi chake,pesa mpaka wa Ikulu walichota, mawaziri wake,Halafu eti kuzuga akakamata vijana wa BOTπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Rugemalira hajafungua kesi ya kuidai serikali Bali anaisaidia serikali kulipwa pesa zake.
Shida nayoiona watu hawasomi hiyo case na hawataki kusoma
Hata hii ya sioi nayo watu hawajasoma hoyo case
Wewe ni mgeni Galilaya hujui kinachotokea. Subiri ujio wa yesu kwa mara ya pili
 
Iwekwe sheria ukikaa ndani zaidi ya mwaka bila ushahidi ulipwe fidia hii itaepusha wahuni kutumia madaraka yao vibaya kuumiza watu
 
Yeah ndio maana nimekubali vita ya ufisadi ilikuepo ila nachosema ilikua biased yaani wezi 20 afu unakamata wawili pekee!!

Mfano hii kesi ya EGMA gavana wa BOT au waziri wa uchumi wanaponaje? Mgimwa na Mkullo walitajwa ila mbona sijasikia waziri yeyote akikamatwa?? Hivi kweli Shose na Sioi waiibie serikali bilion 12 bila "wazee" kuwaandalia njia?

Na ndio maana kuna uzi humu wa Lissu kuwa kumkamata Seth haitoshi maana wizi ni mnyororo so kma unataka kumaliza ufisadi ni kukamata mnyororo wote kuanzia katibu wa Rais mpaka teller aliyetoa hela kwenye masandarusi!!
 
Mbona anashtaki Standard Bank ilipe serikali ya Tanzania? Naona wengi hamjasoma document kabla ya kucomment
Waliocomment hapo juu wote hawajasoma document. Huyo nimetafsiri kwamba anataka hela iliyolipwa kwa Mwingereza irudishwe kwani hakuwa mwathirika wa hii voidable contract. Ila sijui chochote kuhusu sheria
 
Hivi unajua kinachodaiwa au unakurupuka? Hizo pesa zililipwa kwa Serikali ya Uingereza ila Sioi anasema ni haki ya Serikali ya Tanzania hivyo zilipwe kwenye serikali ya Tanzania na siyo yeye anaidai Serikali ya Tanzania!
Mkuu kumbuka hata Ruge amekuja na lengo la kuipambania serikali, mwisho wa siku Ruge anachake pale sawa na SIOI. Kula mtori nyama utazikia badae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…