Sioni aibu kukiri! Paul scholes

Suala la nani ni mchezaji bora wa muda wote halina majibu jumuishi ya nani ni zaidi.
Mfano mimi ninaamini Gaucho ndo kila kitu huku mwingine kwake ni Messi, Cr7, Pele, Ronaldo, Romario, Maradona n.k

Hivyo kila mtu yuko sahihi kuamini kile anachoona ni bora kwake na kukiweka bayana.
 
View attachment 2288217

Huyu ni fundi aitwae paulo Scholes, kaona alitoe la moyoni kuhusu mchezaji huyu kuwahi kutokea.
Namuunga mkono lakini pamoja na yote hayo ni huyo huyo Paul Scholes katika mechi hiyohiyo uliyopost picha hapo juu, aliachia mkwqju hapa na kiburugwa na kuiwezesha United kwenda Fainal ya Uefa 2008
 
Christiano Ronaldo endapo ingetokea acheze dhidi yake angesema zaidi ya hivyo.
 

Huyo gauch ana mafanikio gani kumzidi messi? Au kumzidi hata zidane?
 
Hakuna kitu kama icho, hiyo itakua mahaba niuwe kama ambavyo mashabiki wa zidane, gaucho n.k, but kimoyoni wanajua nani mkali zaidi ya hawa.
Na watakuwa wanakiri mmoja baada ya mwingine , Leo ni Scholes kesho atakuja Cristiano mwenyewe akiri Messi ni Bora kuliko yeye
 
Hakuna kitu kama icho, hiyo itakua mahaba niuwe kama ambavyo mashabiki wa zidane, gaucho n.k, but kimoyoni wanajua nani mkali zaidi ya hawa.
Kila mtu ana mtazamo wake,usitake watu wafanane mitazamo.
 
Huyo gauch ana mafanikio gani kumzidi messi? Au kumzidi hata zidane?
Umeanza ubishi wa vijiweni.kwani walikua na mashindano gani wanayoshindana ili leo uwalinganishe kimafanikio?.Kila mtu alicheza kwa wakati wake kulingana na mipango ya mwalimu na kikosi slichokua nacho sasa huo ushindani wamafanikio unaouleta unasababishwa na nini?
 
Mimi ukiniambia unatakamani nani arudi kwenye enzi zake nitakuambia natamani Gaucho na Zidane walikuwa wananipa Raha sana kwenye suala Zima la kuuchezea mpira
 
Huyo gauch ana mafanikio gani kumzidi messi? Au kumzidi hata zidane?
Mafanikio yanapimwa ktk nyanja nyingi. Kama wewe utajikita kwenye kufunga magoli na kutoa pasi za mwisho za magoli basi Messi ni bora kuliko Gaucho.

Ila ninakuhakikishia mpira sio kufunga tu magoli maana kuna siku nyingine hayo magoli hayapatikani, sasa kwa muktadha kama huo huwa unafurahia kipi?. Nadhani ulishapata majibu.

Kuna wanaoamini Gaucho ndo nabii na mtume wa mwisho la mpira wa miguu maana aliyoyafanya uwanjani hayajawi fanywa na yeyote kwa kiwango alichofanya.

Kwa hiyo suala la nani ni mchezaji bora halina jibu la moja kwa moja maana kila mtu ana mtazamo wake.

Ni sawa na kusema kati ya mwanamke mweusi na mweupe yupi unampenda. Hapo kila mtu ana jibu lake au useme kati ya mnene na mwembamba yupi unampenda pia kila mtu atakuwa na jibu lako.

Mwisho japo si kwa umhimu, haitakuja kutokea hata siku moja wote duniani tukasema flani ndo mchezaji bora kuliko wote kuwahi kutokea hapa duniani.
Amechukua vikombe vyote vikubwa kuanzia ngazi ya vilabu hadi timu ya taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…