Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Mimi huwa mara zote napenda kusema ukweli. Niwe kazini, barabarani au nyumbani ukweli ndio ngao yangu.
Kwa hakika Mimi sitamchagua Magufuli wala mwana CCM yeyote kwa ngazi yoyote ile katika uchaguzi huu.
Ila kwa hali inavyoonekana Magufuli atashinda tena kwa kura za ndio. Hii imesababishwa na mambo mawili
1. Jinsi alivyominya upinzani (demokrasia).
2. Upinzani kushindwa kumsimamisha mgombea mmoja.
Membe apate kura, Lissu apate kura, Mzee wa ubwabwa naye apate kura. Labda ile sheria ya 50% ingetumika hapa nchini kidogo kampenyo kangeonekana.
Magufuli atashinda , ila nikiwaza kama mtumishi wa umma ninayelipwa mshahara mdogo na ninategemewa naumia sana.
Ndani ya utumishi wangu wa miaka 5 na mwezi mmoja nimeshindwa kujiendeleza kielimu, pesa sina. Nimejenga kajumba pembezoni mwa jini na kununua kigari cha kutolea mkosi ambacho nakitumia weekend tu mara nyingi kwa visafari vya church. Kazini siendi nayo mara kwa mara kwasababu ya kubana matumizi.
Maana naona hali ya watumishi sisi itakuwa mbaya, kuacha kazi tunashindwa kwasababu ya mafao yetu mmeyashikia. Vinginevyo mwezi wa saba mwaka huu ningemwaga manyanga nikalime kwetu Njombe.