Sioni faida yoyote kuzaa mtoto ambaye hatokuwa chini ya himaya yangu

Sioni faida yoyote kuzaa mtoto ambaye hatokuwa chini ya himaya yangu

Nilikuwa kwenye mahusiano na mke wa mtu, ambapo bidada baada ya kunogewa alishauri tuzae mtoto, ambapo atabeba mimba yangu, na kumuhadaa mumewe kuwa ni mimba yake, pia na mtoto atakayezaliwa atatumia jina la mumewe.

Kutokana na ushawishi, ilibidi nimkubalie na kwa sasa yuko karibuni kujifungua.

Kinachonitesa katika nafsi yangu kwa sasa, ni hapo mbeleni nitakapokua namuona mtoto, nikijua kabisa ni mtoto wangu lakini sina maamuzi naye, kwa sababu hatokuwa anatumia jina langu, naye pia hatojulishwa kuwa mimi ni baba yake; Inakuwa kama vile, mbegu nilimwaga kwenye mwamba.

Kwa hali hiyo, sioni faida yoyote kuzaa mtoto ambaye hatokuwa chini ya himaya yako.
Wakat mmekubaliana hayo.. hii akili ulikuwa umeweka chini ya uvungu au?
 
Nakushauri mkuu.. fanya ufanyavyo mtoto afanane na wewe mkuu hauna jinsi.. maana ndio itakuwa salama yako
 
Biological father damu nzito kuliko maji ipo siku mambo yatakua hadharani, ila hv inakuaje mpaka utoke na mke wa mtu
 
Kuna boya nae aliona kapaaaata Mke... tukisema vijana wasioe mnatuona mazuzu,,haya sasa Mke wa mtu kaliwa na ujauzito kabeba.

Nakusihi huyo mtoto sio wako pia..

Umepigwa tu changa la macho mzee.... huyo mshenzi hana maana yoyote anakuchota tu akupige mizinga..
 
Kinachonitesa katika nafsi yangu kwa sasa, ni hapo mbeleni nitakapokua namuona mtoto, nikijua kabisa ni mtoto wangu lakini sina maamuzi naye, kwa sababu hatokuwa anatumia jina langu, naye pia hatojulishwa kuwa mimi ni baba yake; Inakuwa kama vile, mbegu nilimwaga kwenye mwamba.
Halafu awe mumefanana copyright hapo ndipo utakapozidi kuumia.
 
Ivi ukifikiria kabla ya kutenda au ni tamaa mbele unasubiri mauti😂
Nilikuwa kwenye mahusiano na mke wa mtu, ambapo bidada baada ya kunogewa alishauri tuzae mtoto, ambapo atabeba mimba yangu, na kumuhadaa mumewe kuwa ni mimba yake, pia na mtoto atakayezaliwa atatumia jina la mumewe. Kutokana na ushawishi, ilibidi nimkubalie na kwa sasa yuko karibuni kujifungua.

Back
Top Bottom