Pre GE2025 Sioni kama ni afya au tija kwa taifa kwa raia wote kupiga kura katika uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Hili suala la raia wote kupiga kura kuchagua viongozi halijakaa sawa, naona kama lina madhara mengi na makubwa zaidi kuliko faida kwa sababu kuna watu wengi wanapiga kura lakini hawaelewei uzito wa kura yenyewe hivyo sio rahisi kwao kufanya maamuzi sahihi. Matokeo yake watu wa aina hii wakiwa wengi maamuzi yao yanaathiri taifa zima vibaya.

Pia soma: Kama tumekata tamaa kiasi hiki kwenye suala la kupiga kura, kuna matumaini ya kupata viongozi bora?

Ingefaa watu waliomaliza kidato cha nne na kupata cheti pamoja na wale wanaolipa kodi ya kipato (income tax) tu ndio wapige kura za kuchagua viongozi. Katika haya makundi angalau tunaweza kupata majority ya watu wanaolewa uzito wa kura yao kwao na kwa taifa zima kwa ujumla.

Hii pia ingesaidia sana kupunguza gharama za uchaguzi zisizo za lazima.
 
Kwa iyo tuache basi hata hata inchi ikiuzwe tuache tu manake kura zetu hazina impact ndo hayo mawazo au sio JF kennedy alisema taifa likiwa la watu wajinga kupiga hatua ni ngumu mnoo bahati mbaya ccm wanatukuza ujinga ndo mana maendeleo yetu ni kujenga na madaraja kupata sifa za kupigiwa kula next election
 
Hoja yako ni kuntu sana, lkn sidhani kama chawa wa ccm wananelewa ulichoandika.
 
Hili suala la raia wote kupiga kura kuchagua viongozi halijakaa sawa, naona kama lina madhara mengi na makubwa zaidi kuliko faida kwa sababu kuna watu wengi wanapiga kura lakini hawaelewei uzito wa kura yenyewe hivyo sio rahisi kwao kufanya maamuzi sahihi. Matokeo yake watu wa aina hii wakiwa wengi maamuzi yao yanaathiri taifa zima vibaya.

Pia soma: Kama tumekata tamaa kiasi hiki kwenye suala la kupiga kura, kuna matumaini ya kupata viongozi bora?

Ingefaa watu waliomaliza kidato cha nne na kupata cheti pamoja na wale wanaolipa kodi ya kipato (income tax) tu ndio wapige kura za kuchagua viongozi. Katika haya makundi angalau tunaweza kupata majority ya watu wanaolewa uzito wa kura yao kwao na kwa taifa zima kwa ujumla.

Hii pia ingesaidia sana kupunguza gharama za uchaguzi zisizo za lazima.
Wazo lako sio baya, ila kama kagenge kanachooita system hakataki kuheshimu kura ni kazi bure.
 
Naunga Mkono hoja, kusema watu wote wapige kura sio sahihi pawekwe vigezo kuanzia elimu, uwe na TIN number na kiasi flan cha kipato Kwa mwaka.

Sir Edward Twining alifanya hvo mwaka 1958 wakati wa uchaguzi TANU aliweka vigezo kuanzia kipato, uwe na ajira/kituo Cha kazi na elimu wale kina yakhe wa pwani wengi walipigwa chini vibaya sana maana hawakua na vigezo...ndo maana ukichunguza malalamiko mengi ya Mohamed said msingi wake unaanzia hapo
 
Sikuwahi kujua hili!
Mohamed Said ni kweli haya yanayosemwa hapa?
 
Back
Top Bottom