1120ulimwengu
JF-Expert Member
- May 23, 2013
- 252
- 422
Kwanza jifunze matumizi ya punctuation marks.Namba mbili jifunze matumizi ya herufi kubwa na ndogo.Tatu jifunze namna ya kuandika aya moja kikamilifu kabla ya ngingine.Inashangaza mtu anayetaka uteuzi hajui kuandika!!!!Ndugu zangu Watanzania,
Rais na Mkuu wa Nchi ndiye kiongozi namba moja katika Nchi kupewa Ulinzi Mzito na mkubwa kila mahali awapo. Ndio jicho lote la vyombo vya ulinzi na usalama huelekeza na kupeleka umakini wake alipo Rais. Ulinzi wote wa kuonekana na usioonekana na wa kila aina ya teknolojia ni lazima uwekezwe kumzunguka Rais.
Rais hupewa walinzi makini, madhubuti, hodari,shupavu,imara , wazalendo na wenye mafunzo ya aina ya juu sana na aina tofautitofauti katika ulinzi wa Rais. Huzungukwa na walinzi ambao wapo tayari kufa kwa ajili ya kumlinda Rais.wapo tayari kuwa ngao ya RAIS zidi ya kihatarisha chochote kile cha usalama wa Rais awapo popote pale.
Sasa inapotokea Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu anatembea na kuzunguka Nchi mbalimbali na maeneo mbalimbali akiwa na silaha kiunoni pake ikiwa inaonekana hadharani kwa watu. Inakuwa ni tatizo kubwa sana kwa Rais Mwenyewe. Kwa sababu hata kama Rais akitaka kuwa na silaha kiunoni pake anaweza kufanya hivyo pasipo hata kuionyesha wala mtu yeyote yule kuiona.
Kwani viongozi wangapi wanatembea na silaha viunoni Mwao? Kwanini hawazioneshi na kuziweka hadharani? Sasa kwa huyu Rais kijana kufanya hivi inakuwa siyo jambo zuri wala la busara wala la kiuongozi wala la kiungwana katika Dunia hii ya Leo.
Ambayo mtu anaweza kukudhuru hata kwa kutumia kalamu tu ya kuandikia au nyaraka tu ambazo ukapewa uzisome. Ndio maana Majeshi yote Duniani kwote kwa sasa yanawekeza sana katika Teknolojia ya juu.huko ndiko ushindani umehamia na siyo katika kutembea na silaha kiunoni inayoonekana kwa watu.View attachment 3242595
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Sambamba na hilo koma kufatilia mambo yasiyokuhusu.Haujui mhusika amekoswa kuuwawa mara ngapi na imperialists wa kifaransa wanamuwinda kwa kiasi gani!Traore sio SAMIA hawa ni mbingu na ardhi!Uzalendo wa Traore haukaribiani na wa unayemchawia hata kwa 1%.
Mwisho kabisa wakati unawaza kutosha kwa anayepwaya kwa miaka mingine mitano-wenzako duniani wanafanya mambo makubwa ndani ya wiki tatu tuu!!! Fanya uchawa ulipwe ama upewe uteuzi kwenye nchi maskini,kimaskini uwaongoze maskini kifua mbele!!!