Stanslaus Mbwiliza
Member
- Oct 1, 2019
- 8
- 2
Katika hafla ya kuwaapisha wakuu wa mikoa, Mhe. Spika amewaasa wakuu wa mikoa kuacha kujiita marais wa maeneo wanayoyaongoza akidai kufanya hivyo kunawafanya kujiona kama Rais.
Binafsi sioni tatizo kujiita jina la unayemwakilisha eneo husika. Lililo la msingi kwao ni kumwakilisha Rais kwa kutoa maamuzi sahihi kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo iliyopo.
Hawatakiwi kubana haki za msingi za wananchi na viongozi walio chini yao kwa sababu nyepesi binafsi. Wanatakiwa kuwa viongozi wanaoshaurika, wasikivu na wanaokubali kukosolewa na watu wenye mtazamo tofauti.
Wakitekeleza majukumu yao ipasavyo wananchi watawaamini na kuona kweli wanamwakilishi ipasavyo mheshimiwa Rais, na ziara za Rais haziwezi kupokelewa kwa mabango mengi ya kero zinazowakabili wananchi wa eneo husika.