Uchaguzi 2020 Sioni utulivu wa CHADEMA mara baada ya uchaguzi huu wa 2020

Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2013
Posts
2,496
Reaction score
1,800
Kabla ya uchaguzi Mkuu ujao, Chadema wamekuwa wakiishi na kufanya kazi na Tundu Lissu kama Mwanasheria Mkuu wa Chadema, na Mjube wa Kamati Kuu.

Kumekuwa na tofauti ndogo ndogo ambazo ni kawaida katika chama chochote ambacho sio Chama Dola.

Tofauti hizi zitajitokeza wazi baada ya Lissu kujua nguvu yake kwa umma, Lissu wa baada ya uchaguzi sio wa leo. Lissu baada ya uchaguzi ni kiongozi alieuzwa kwa Watanzania na kupigiwa kura. Kwa sisi ambao tumemfuatilia Lissu kwa karibu na muda mwingine kuzungumza nae hasa kabla hajaenda kwenye matibabu, naamini hatokubali kuongozwa na kutofanywa sio mtu muhimu kama zamani. Alikuwa muhimu tu wakati anahitajika au kufanya chama kikimuagiza. Kuna kipindi alionekana anaongeza gharama kwa chama na kesi zake.

Tundu Lissu kitabia na uchanganyikaji wake na viongozi, unatofauti na Kitchen Cabinet ya Mbowe. Kwa hiyo hayuko na hajawahi kuwa katika Kitchen Cabinet ya Mbowe. Matokea ya uchaguzi huu yatamfanya azamie jikoni kwa nguvu, sasa hatujui kama kina Lema, Jacob, Halima, Mnyika na Ester watakuwa tayari kukaribisha mgeni ndani ya chumba ambae hawaja mzoea chumbani. Mkumbuke video za Lema kabla Lissu hajarudi, zinaweza kukupa picha ya muelekeo.
 
Lissu anashinda urais kwa zaidi ya 75% kwenye chama arudi kufanya nini ?
 
Mmehama kutoka kwenye kujadili hoja zake za uchaguzi mnaanza ramli ?
 
CDM haifi kirahisi, chama kimepitia magumu mengi mno na kama hakijafa wakati huu wa jiwe muua demokrasia, basi itabidi nguvu ya ajabu itumike na hata hivyo haiwezekani kwani kuna watu wengi nyuma ya chama.
 
Kabla ya uchaguzi Mkuu ujao, Chadema wamekuwa wakiishi na kufanya kazi na Tundu Lissu kama Mwanasheria Mkuu wa Chadema, na Mjube wa Kamati Kuu.

Kumekuwa na tofauti ndogo ndogo ambazo ni kawaida katika chama chochote ambacho sio Chama Dola.

Tofauti hizi zitajitokeza wazi baada ya Lissu kujua nguvu yake kwa umma, Lissu wa baada ya uchaguzi sio wa leo. Lissu baada ya uchaguzi ni kiongozi alieuzwa kwa Watanzania na kupigiwa kura. Kwa sisi ambao tumemfuatilia Lissu kwa karibu na muda mwingine kuzungumza nae hasa kabla hajaenda kwenye matibabu, naamini hatokubali kuongozwa na kutofanywa sio mtu muhimu kama zamani. Alikuwa muhimu tu wakati anahitajika au kufanya chama kikimuagiza. Kuna kipindi alionekana anaongeza gharama kwa chama na kesi zake.

Tundu Lissu kitabia na uchanganyikaji wake na viongozi, unatofauti na Kitchen Cabinet ya Mbowe. Kwa hiyo hayuko na hajawahi kuwa katika Kitchen Cabinet ya Mbowe. Matokea ya uchaguzi huu yatamfanya azamie jikoni kwa nguvu, sasa hatujui kama kina Lema, Jacob, Halima, Mnyika na Ester watakuwa tayari kukaribisha mgeni ndani ya chumba ambae hawaja mzoea chumbani. Mkumbuke video za Lema kabla Lissu hajarudi, zinaweza kukupa picha ya muelekeo.
Ramli chonganishi
 
Back
Top Bottom