Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 25,968
- 36,044
Maandamo yaliyofanyika tarehe 29 October 2025 yalifanikiwa kufanyika kwa sababu maandamano yalikuwa yameunganishwa na tukio kubwa la kitaifa ambalo ni uchaguzi.
Kwa kuwa 29 Oktoba ndiyo ilikuwa siku ya uchaguzi, watu wengi walikuwa tayari wako nje ya nyumba zao, vituo vya kupigia kura na barabarani. Hilo liliunda mazingira ambayo mkusanyiko wa watu uliweza kugeuka haraka kuwa maandamano katika baadhi ya maeneo.
Pia wapo walioandamana kwa mkumbo.
Mbali na hilo , suala la taarifa zilizotoka hapo awali kwamba wanajeshi wapo nyuma ya wananchi kuhakikisha wanawasapoti ndio ilichochea zaidi au ilihamasisha zaidi wananchi kuandamana , haswa yule Captain Tesha kujitokeza waziwazi kuunga mkono wananchi.
Na kweli kwa kiasi fulani maeneo kadhaa wanajeshi waliwapa sapoti wananchi kwa kuwalinda, ila baada ya jeshi kukaa pembeni wananchi walikosa ile nguvu ya kuandamanana .
Ila hatua zilizo chukuliwa kuyadhibiti ndio imefanya mpaka sasa hata nguvu itumike vipi kuhamasisha watu hawataweza tena kuandamana.
Miongoni mwa hatua ambazo zilikuwa mwiba mkubwa kwa wananchi ni ile suala la lockdown, wengi wanategemea kutoka ili wapate mkate wao wa siku, kitendo cha kufungiwa kingedumu hata wiki 2 wengi wangefia ndani kwa njaa, na mbaya zaidi kilichoumiza wengi ni suala la bidhaa kupanda bei mno.
Yani lockdown ya siku 2 tu nyanya zilipanda bei mpaka kufikia elfu 1200 kwa nyanya moja, viazi kisado cha elfu 4 kilifika mpaka elfu 10, nyama ndo usiseme.
Na hata hayo maduka nayo yalikuwa yakifunguliwa kiuoga uoga , wengi walikuwa wanaogopa kutoka nje wakihofia maisha yao.
Wapo wagonjwa ambao wanahitajika kwenda hospitali kwa ajili ya maendeleo ya afya zao , lockdown ingesababisha wengi wafie ndani maana hata kutoka nje kununua dawa haikuwa rahisi.
Kingine suala zima la kuzima mitandao ya kijamii ilikuwa ni mateso makubwa maana watanzania wengi wamezoea kushinda IG, JF,Tiktok nk na wengine hiyo mitandao ya kijamii ndio ofisi zao.
Sasa haya yote kwa ujumla wengi wakiyafikiria inawawia vigumu kusapoti maandamano.
Na huku mtaani taarifa za maandamano ndio hazipo kabisa, taarifa za maandamano zipo mitandaoni tu ila kwenye maisha halisia ya mtaani watu taarifa hizo hawana.