Mfichua siri
Senior Member
- Jun 19, 2012
- 135
- 62
Wadau mwenzenu nimeolewa mwaka 2009 Mwaka 2010 nilijaaliwa kupata mtoto wa kike kwa Operation, Nilishauriwa na Daktari nisizae tena mpaka mtoto atimize miaka walau mitatu ili mshono upone kabisa, mwanzoni mwa mwaka huu kwa kuzingatia masharti ya Daktari nikaanza kusakama mtoto wa pili na wa mwisho, tena nikitumia Karenda ya uzazi nikajikita kutafuta mtoto wa kiume kwa kuonana na mme wangu siku ya 13 na kuendelea toke nipatapo Hedhi lakini haijawahi kujibu.
Nikaona niachane na masuala ya kutafuta mtoto kwa kuchagua jinsia, basi tukaanza kukutana na mme wangu kuanzia siku ya 8 mpaka siku ya 15 toka nipate hedhi lakini hakuna kitu, Mzunguko wa siku zangu ni siku28, mwezi wa nne nilimuona Daktari akanipima na kukuta chuchu zangu zilikuwa bado zinatoa maziwa kwa mbaali hivyo niliambiwa vichocheo vyangu vya mwili ndo vinasababisha nisipate uja uzito ameshanipatia dawa mara kadhaa kwa ajiri ya ku-control vichocheo na maziwa hayatoki tena lakini bado sibebi uja uzito. Ikumbukwe sijawahi kutumia dawa za kuzuia Mimba nilikuwa natumia karenda tu.
Kinachonitisha ni suala la Umri kwasababu nimezaliwa Mwaka 1977. Nina umri wa miaka 36 nimechelewa sana kuanza uzazi kwasababu sikutaka kuzaa kabla ya kuolewa na nilichelewa sana kuolewa kwasababu waoaji walikuwa hadimu japo uwezo wa kujikimu niliupata mapema kidogo, sasa nina frustration zinazidi kila kukicha, nimejaribu kumuomba mme wangu naye akapime labda ndo tatizo lakini anagoma, je yawezekana nimezeeka au? najuuta kuchelewa kuzaa, naombani mnishauri kama kweli at this age and above ninaweza kubahatika mtoto maana mpango wangu ni watoto wawili.