chavalla
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 451
- 354
Watu wengine wajinga sana,
Jana nimekaa na jamaa mmoja siti jirani kwenye basi tokea tunaanza safari kutoka Dar ubungo terminal tunaenda Morogoro .
Basi Jamaa ananunua vitu anakula kula hanikaribishi hapo tupo kibaha akanunua korosho, apple, karanga, juice hata kusema karibu Hakuna yeye no kula tu, ,
Tulipofika Chalinze akaenda kununua nyama choma, mara mahindi ya kuchemsha ,
mara ndizi za kuiva , karanga mara hiki mara kile na anashushia tu juice na maji mwenyewe hata kuniangalia yaani hats kuniuliza kitu wala kusema karibu. Mimi nipo zangu tu nasoma magezeti na kuchat ktk mitandao ya kijamii, facebook, instagram, whatsapp ...
Tumefika Mikese nimetoa power bank yangu nataka kuchaji simu,, kumbe naye simu yake imezima charge.
eti ndio akaniuliza hiyo ni power bank??
mimi nikamjibu hapana ni Dawa ya Meno.
Hakunisemesha tena mpaka tumefika tumefika Morogoro .
Tumeshuka Morogoro msamvu stand terminal tumeshuka wote kumbe naye anaelekea Mazimbu akaniuliza tena kumbe tupo safari moja ya Mazimbu ??
nikamjibu hapana hatupo pamoja mi naelekea Gongolamboto ...
Hakuniuliza wala kunisemesha tena