Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 70,916
- 141,437
Sipendi kuchanganya l na R katika uandishi, muda mwingine inabidi niepuke kutumia baadhi ya maneno ili nisiyakosee, naomba kueleweshwa haya maneno yanaandikwaje kwa ufasaha.
Je ni lipi sahihi
kachumbali au kachumbari?
Kulogwa au kurogwa
Mkwala au mkwara?
Nitaongezea nitakayokumbuka.
Empty cdPolee sana..empty set!
Hata walimu wenyewe siku hizi wamekua kizazi cha facebook hawajui wapi ni L wapi ni RShule hufundisha kuandika inavyotakiwa, lakini kuna mifala pakuweka L wao huweka R. Na penye R wao huweka L lakini wakiwa kwenye exam huandika sahihi kabisa.
Sahihi ni kusali na kuswaliKusali / kusari??
au
Kuswali / kuswari??
(Nikiwa na maana kitendo cha kufanya ibada)
Sahihi ni Tafsiritafsiri?
tafasiri?
tafasili?
fasili?
fasiri?
nipe usahihi hapo
kiswahili kipana mamaSahihi ni Tafsiri
Fasili/fasiri maana yake nini?
RadhiRadhi/ ladhi lipi sahihi
Mkristo/ mkristu, yote ni sahihi. Nimeona kristu hutumiwa zaidi na wakatoliki, na wengine husema kristo.ongeza pia
mkristo?
mkristu?
tafakuri
tafakari?
Tafakari na tafakuri nnavojua mie yote ni maneno sahihi ila maana zake ni tofauti.ongeza pia
mkristo?
mkristu?
tafakuri
tafakari?
Tazamaje ni Tizama au Tazama?
Kweli kiswahili ni kipana, ndio nalijua kwa mara ya kwanza.
tafsiri- Translate
tafasiri- Meaning
fasiri - Translation
usahihi huu hapo